Kosa la kulipa kisasi ni lipi?

Massa

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
647
794
Miaka mingi iliyopita kuna jamaa kwenye ukoo wetu ambaye alikua vizuri kiuchumi alikua na mahusiano ya kimapenzi na dada yetu. Inshu ilipelekea wazazi wa pande zote kutokua na maelewano kabisa. Ilo suala kwa upande wa wazazi wetu liliwauma sana hasa baada ya kwenda kumsihi jamaa aache mahusiano na dada kwa kua wana undugu kwenye ukoo.

Lakini kauli ya jamaa kwa kua alikua na pesa kipindi hicho haikua ya kistaharabu. Na kama mjuavyo dada zetu wakiishapenda unaweza kumuua lakini hawezi kuacha. Siku zikaenda sister akawa kaolewa na jamaa wa mkoa wa mbali na nyumbani kwa kiasi hali ikatulia. Kipindi icho mimi bado mdogo ingawa utambuzi nilikua nao na ugomvi huo naujua sana tu.

Huyo ndugu yetu licha ya kua na mahusiano na dada ila alikua tiari ana mke.

Kwenye ndoa jamaa alizaa watoto wa kike wa kwanza na wa pili. Miaka imeenda watoto wamekua wakubwa maisha kama mbio za vijiti nilibahatika kupata vijicent vya mboga. Mwaka huu nikakutana na binti mkubwa wa jamaa nikatongoza akakubali na tukawa kwenye mahusiano ya kimapenzi kweli. Mimi tiari nina mke na watoto lakini ilibidi nifanye kulipizia tu. Inshu wazazi wake wamejua na wameanzisha ugomvi kwenye familia tena. Walivyoenda kusema kwa wazazi wangu mzee akamkumbusha jamaa.

Sasa hapa anatishia kunifikisha police na binti keshamaliza chuo yupo tu nyumbani. Kosa langu ni kumsaliti mke wangu. Lakini kwa huyo ndugu yangu wallahi sijutii ata kidogo.
 
Ndugu kwa ndugu mnakulana sijaelewa hii kingereza ndo tunaita cross-pollination🤔
 
Ndugu kwa ndugu mnakulana sijaelewa hii kingereza ndo tunaita cross-pollination

Ni kweli ni ndugu kwenye ukoo. Kawaida mimi inabidi nimuite baba mdogo. Lakini kama yeye alimkula mtoto wa kaka yake kwenye ukoo Kwa nini mimi nisile mwanae?. Maana mtoto sio wa dada yangu mimi.
 
Miaka mingi iliyopita kuna jamaa kwenye ukoo wetu ambaye alikua vizuri kiuchumi alikua na mahusiano ya kimapenzi na dada yetu. Inshu ilipelekea wazazi wa pande zote kutokua na maelewano kabisa. Ilo suala kwa upande wa wazazi wetu liliwauma sana hasa baada ya kwenda kumsihi jamaa aache mahusiano na dada kwa kua wana undugu kwenye ukoo.

Lakini kauli ya jamaa kwa kua alikua na pesa kipindi hicho haikua ya kistaharabu. Na kama mjuavyo dada zetu wakiishapenda unaweza kumuua lakini hawezi kuacha. Siku zikaenda sister akawa kaolewa na jamaa wa mkoa wa mbali na nyumbani kwa kiasi hali ikatulia. Kipindi icho mimi bado mdogo ingawa utambuzi nilikua nao na ugomvi huo naujua sana tu.

Huyo ndugu yetu licha ya kua na mahusiano na dada ila alikua tiari ana mke.

Kwenye ndoa jamaa alizaa watoto wa kike wa kwanza na wa pili. Miaka imeenda watoto wamekua wakubwa maisha kama mbio za vijiti nilibahatika kupata vijicent vya mboga. Mwaka huu nikakutana na binti mkubwa wa jamaa nikatongoza akakubali na tukawa kwenye mahusiano ya kimapenzi kweli. Mimi tiari nina mke na watoto lakini ilibidi nifanye kulipizia tu. Inshu wazazi wake wamejua na wameanzisha ugomvi kwenye familia tena. Walivyoenda kusema kwa wazazi wangu mzee akamkumbusha jamaa.

Sasa hapa anatishia kunifikisha police na binti keshamaliza chuo yupo tu nyumbani. Kosa langu ni kumsaliti mke wangu. Lakini kwa huyo ndugu yangu wallahi sijutii ata kidogo.
Na wewe utazaa watoto wakike maisha ni kama mbio za vijiti ndugu zako watamtafuna na watakuwa wameoa
 
Ngoja wanakuja mkuu

DJ waletee ndugu upande wa mwanamke na mkwaju wa (Msondo ngoma-Piga ua,Talaka utatoa)
MC, ndugu hawawezi kuja kwa sasa maana wanauguza vidonda kidogo, sababu hii Chai ya jamaa niyamoto sana. Tuendele kuburudika, wataingia wakati wa kufunga sherehe.
 
Na wewe utazaa watoto wakike maisha ni kama mbio za vijiti ndugu zako watamtafuna na watakuwa wameoa
Hizi ni zile koo ambazo huwa zinasemwa kuwa zina laana ya asili. Hata incest kwenye huu ukoo haitakosekana kama mambo menyewe ndiyo haya. Ni ukoo wa kuuombea na kuupambania sana kiroho vinginevyo hii chain ya aibu itaendelea tu vizazi na vizazi hadi utimilifu wa dahari!

#Breakthechain
 
Back
Top Bottom