Kortini kwa kumuita Robert Mugabe mzee

Kortini kwa kumuita Robert Mugabe mzee

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Afisa mmoja wa polisi amefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baada ya kulaumiwa kwa kusema kuwa rais Robert Mugabe ambaye sasa ana umri wa miaka 92 ni mzee sana kuwa kiongozi.

Thomson Joseph Mloyi pia anadaiwa kumtusi mkewe rais Mugabe, Grace, kuwa kahaba kwa mujibu wa gazeti la kibinafsi nchini humo.

Thomson Joseph Mloyi pia anadaiwa kumtusi mkewe rais Mugabe, Grace, kuwa kahaba.

Bwana Mloyi aliachiliwa kwa dhamana ya dola 100 na anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena tarehe 15 mwezi huu.

Mugabe ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani baada ya kutimia umri wa miaka 92 mwezi uliopita.


Chanzo: BBC
 
Mambo mengine yanachekesha kweli lakini pengine alikosea sana kumuita mzee kwakuwa hiyo level ameshaipita alipaswa kumuita kikongwe
Na huyu mama pia ni kumvunjia adabu na heshima kumuita kahaba kwakuwa yeye hajiuzi alipaswa kumuita mama huruma
 
Back
Top Bottom