KOROGWE : Makada 44 CCM wachukua fomu kumrithi Professor Maji Marefu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,553
Makada 44 wa CCM wamejitokeza kuwania ubunge jimbo la Korogwe Vijijini.

Makada 47 walichukua fomu hizo na 44 kati yao akiwamo mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Thomas Ngonyani wamerudisha leo Agosti 7.

Jimbo hilo lilikuwa likiongozwa na Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu aliyefariki dunia Julai, mwaka huu.

Katibu wa CCM Wilaya ya Korogwe Vijijini, Suraisa Sangusa amezungumza na Mwananchi leo Agosti 7 kuwa, hadi leo saa 12 jioni tayari makada 44 walikuwa wameshawasilisha na fomu kupokewa rasmi.

Amesema kazi iliyobaki ni kwa kamati ya siasa ya wilaya hiyo kuendesha mchakato wa kuchambua kama waliorejesha wamefuata taratibu zote kabla ya kuyapeleka majina hayo katika ngazi ya mkoa kwa ajili ya hatua ya awali ya mchujo.

Hata hivyo, katibu huyo amesema majina ya waliorejesha fomu na kupokewa atayataja kesho.

“Naomba ifahamike kwamba hawa waliorejesha fomu wataingia katika mchujo wa ngazi ya wilaya, mkoa hadi Taifa ili aweze kupatikana atakayeaminiwa na chama chetu kupeperusha bendera ya kuliwania jimbo hili dhidi ya vyama vingine,”amesema Suraisa.

Jimbo la Korogwe Vijijini limebaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake Stephen Ngonyani kufariki dunia mwezi uliopita na jana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililitangaza rasmi kuwa wazi na kuruhusu vyama vya siasa kuendesha mchakato wa kuwateua wanachama wake kuligombea.
 
Dr Mndolwa wa CCM ndio wakati wake wa kudhihirisha kuwa anakubalika, ila Marehemu alikua anamfanyia figisu!
 
Huyo maji marefu afe tena huko aliko ***** umenikumbusha kipindi anajifanya mganga wa kuwashika wachawi alikujaga kijinini kwetu akawachapa sana wazee na kuwamwagia maji na kuwalazimisha kupanda kinyume nyume juu ya mti huku kichapo kinaendelea eti ni mchawi na kila aliekamtwa na kupigwa haikupita mwezi anakufa.. daa tulizika sana wazee kipindi hicho
 
Makada 44 wa CCM wamejitokeza kuwania ubunge jimbo la Korogwe Vijijini.

Makada 47 walichukua fomu hizo na 44 kati yao akiwamo mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Thomas Ngonyani wamerudisha leo Agosti 7.

Jimbo hilo lilikuwa likiongozwa na Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu aliyefariki dunia Julai, mwaka huu.

Katibu wa CCM Wilaya ya Korogwe Vijijini, Suraisa Sangusa amezungumza na Mwananchi leo Agosti 7 kuwa, hadi leo saa 12 jioni tayari makada 44 walikuwa wameshawasilisha na fomu kupokewa rasmi.

Amesema kazi iliyobaki ni kwa kamati ya siasa ya wilaya hiyo kuendesha mchakato wa kuchambua kama waliorejesha wamefuata taratibu zote kabla ya kuyapeleka majina hayo katika ngazi ya mkoa kwa ajili ya hatua ya awali ya mchujo.

Hata hivyo, katibu huyo amesema majina ya waliorejesha fomu na kupokewa atayataja kesho.

“Naomba ifahamike kwamba hawa waliorejesha fomu wataingia katika mchujo wa ngazi ya wilaya, mkoa hadi Taifa ili aweze kupatikana atakayeaminiwa na chama chetu kupeperusha bendera ya kuliwania jimbo hili dhidi ya vyama vingine,”amesema Suraisa.

Jimbo la Korogwe Vijijini limebaki wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake Stephen Ngonyani kufariki dunia mwezi uliopita na jana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ililitangaza rasmi kuwa wazi na kuruhusu vyama vya siasa kuendesha mchakato wa kuwateua wanachama wake kuligombea.
Kuliko fanyika biashara ya utumwa wanapigwa marufuku kuchukua fomu.Ama kweli ma cccm mazezeta haswaa.Mtu anakula mafao mara 2 nyie mpoo tuu mmekipigania chama miaka mingapi?
 
Sema ni kwa vile tu niko mbali, ila humu ndio mwa kufanyia majaribio.

Unaweza kuta katika kujaribu tu nikaupata uwakilishi hivihivi....
 
Bavicha wepesi kusahu,lowassa alijiunga chadema saa 7 mchana,saa 9 mchana kapewa ugombea urais,hakuna kuchukua fomu wa kura ya maoni
sie ccm tuachieni yetu,kazi kwenu nyie mnaotaka dola
 
Na yale majimbo waliyoyafanyia biashara je?
Yale polepole kasema watarudishiwa wale waliojibadili rangi na hakuna cha mchakato kwani nec yao imesharidhia na no question about it! Ccm asili na masalia mpo? Na mtaburuzwa sana safari hii hadi muimbe haleluya! Karibuni kwa mapovu!
 
Back
Top Bottom