Korea ya kaskazini yafanya majaribio mapya ya Silaha

Korea ya kaskazini yafanya majaribio mapya ya Silaha

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,185
Reaction score
24,564
Korea Kaskazini yafanyia majaribio silaha mpya na ya kisasa chini ya usimamizi wa Kim Jong-un
Serikali ya Korea Kaskazini imefanyia majaribio kwa mafanikio, ya silaha ya 'kistratijia, mpya na ya kisasa' chini ya usimamizi wa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
Shirika la Habari la Korea Kaskazini imetangaza kwamba, majaribio hayo yaliyofanyika asubuhi ya leo, yanaifanya silaha hiyo mpya iiongezee uwezo mkubwa wa kijeshi nchi hiyo. Hata hivyo taarifa hiyo hakusema muda wala aina ya silaha iliyofanyiwa majaribio hayo. Hii ni katika hali ambayo Shirika la Habari la Korea Kusini Yonhap limetangaza kwamba hadi sasa halijapata dondoo zozote kuhusiana na majaribio hayo. Majaribio hayo yamefanyika katika hali ambayo tarehe 12 Juni mwaka huu, rais wa Marekani, Donald Trump na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini walikutana nchini Singapore na kutiliana saini makubaliano kadhaa ambapo kwa mujibu wake, Pyongyang ilikubali kuangamiza kikamilifu silaha zake za nyuklia.
Hata hivyo serikali ya Korea Kaskazini imekuwa ikiilalamikia Marekani kwa kukiuka makubaliano hayo, sambamba na Washington kuendelea kufanya maneva mbalimbali ya kijeshi katika eneo, suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Pyongyang. Kabla ya hapo vyombo vya habari nchini Marekani viliripoti kwamba sambamba na kufanyika mazungumzo kati ya viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini katika miezi iliyopita, serikali ya Pyongyang imekuwa ikiendelea kuunda makombora ya mabara kwa kutumia fueli mpya ya majimaji katika viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo.
 
Hakuna kitu kibaya kama umasikini, umasikini huleta chuki, umasikini huleta uasi na umasikini huleta vifo.
.
North Korea wana-experience maisha magumu sana kuliko ya mwananchi wa tandahimba.
.
Wanaimarisha jeshi wakati uchumi ni mdogo What if mataifa yote yakaacha kuwapelekea bidhaa muhimu kama mafuta n.k kwa sanctions za US, China wanawavumilia lakini ipo siku watachoka.
 
ulitaka wafanyeje labda.
 
Waimarishe uchumi wao kwanza ndipo waanze kufanya uwekezaji mkubwa wa billions of money kwenye jeshi lao.
.
Mfano mzuri ni Tanzania tuanze kutumia uranium zile tutengeneze chemical weapons tuwekeze mabilion kwenye vifaa na silaha za kijeshi wakati ni taifa masikini sanaaa.
wakiacha kutengeneza silaha watavamiwa kijeshi, wacha waendelee mpaka pale watakapoamua kufanya mabadiliko.ya kisiasa ili kuondoa uadui kwa mataifa ya magharibi uliopo.
 
wakiacha kutengeneza silaha watavamiwa kijeshi, wacha waendelee mpaka pale watakapoamua kufanya mabadiliko.ya kisiasa ili kuondoa uadui kwa mataifa ya magharibi uliopo.
Mkuu hata sasa wanaweza kuvamiwa na kupigwa vibaya mno na muamerica lakini kuna athari itajitokeza hakutakuwa na "Cold war" tena bali vita halisi yaani WW3.
.
Russia ataingia, China ataingia na wengineo ambao wananafkiana na marekani (Nchi za kiislam). NB: si zote

Wakiingia hao Ukraine ataingia na Soviet country zote zitaingia japan, s.Korea, Canada, Germany, Israel, France, UK, Brazil n.k.
.
Itakuwa ni hatari ndio maana inatumika njia ya mazungumzo, mitambo yao ni hatari hata kwako muafrica likipigwa bomu la nuclear hatubaki kaka atabaki mende tu
 
Mende hatumie oxygen!?
epi4msxe732rioyv4ulk.jpg

Kidugu kina square sijuwi huwa kinachogwa na wembe wa alimasi
 
Back
Top Bottom