Korea Kaskazini yafanya jaribio la ndege isiyokuwa na rubani

HERY HERNHO

Member
Mar 4, 2022
70
313
Korea Kaskazini imesema imefanya jaribio la ndege isiyoendeshwa na rubani yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia na kushambulia ikiwa chini ya maji.

Shirika la habari la nchi hiyo, KCNA, limeripoti hayo hii leo, Ijumaa, wakati kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, akitowa onyo kwamba luteka za kijeshi zinazofanywa kwa pamoja na Korea Kusini na Marekani zinapaswa kusitishwa.

Katika jaribio hilo la Korea Kaskazini ndege hiyo ilisafiri kwa kima cha futi 260 mpaka 500 chini ya maji kwa muda wa saa 59 na kuripua mabomu yasiyokuwa na nguvu za nyuklia chini ya bahari kwenye pwani ya mashariki mwa nchi hiyo hapo jana Alhamisi.

Wachambuzi wanasema nchi hiyo inazionesha Marekani na Korea Kusini, uwezo wake uliozidi kutanuka wa nguvu za nyuklia, ingawa wachambuzi pia wana mashaka ikiwa chombo hicho cha kusafiri chini ya maji kiko tayari kwa matumizi.

65101710_803.jpeg
 
Asante sana Kim. Heshima iwepo. Ifike sehemu South Korea na Japan watafakari upya mahusiano na Marekani.

Siku zote Marekani huchonganisha ndugu.

Baada ya Syria na Saudia kuelewana sasa ni zamu ya N. Korea Vs S. Korea na Japan kuelewana.

Taiwan nayo ipate nakala hii.

Mtu baki asichonganishe ndugu.

Viva N. Korea viva Russia
 
Korea Kaskazini imesema imefanya jaribio la ndege isiyoendeshwa na rubani yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia na kushambulia ikiwa chini ya maji.

Shirika la habari la nchi hiyo, KCNA, limeripoti hayo hii leo, Ijumaa, wakati kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, akitowa onyo kwamba luteka za kijeshi zinazofanywa kwa pamoja na Korea Kusini na Marekani zinapaswa kusitishwa.

Katika jaribio hilo la Korea Kaskazini ndege hiyo ilisafiri kwa kima cha futi 260 mpaka 500 chini ya maji kwa muda wa saa 59 na kuripua mabomu yasiyokuwa na nguvu za nyuklia chini ya bahari kwenye pwani ya mashariki mwa nchi hiyo hapo jana Alhamisi.

Wachambuzi wanasema nchi hiyo inazionesha Marekani na Korea Kusini, uwezo wake uliozidi kutanuka wa nguvu za nyuklia, ingawa wachambuzi pia wana mashaka ikiwa chombo hicho cha kusafiri chini ya maji kiko tayari kwa matumizi.

View attachment 2563836
Ndege hisiyokua na rubani chini ya maji ikashambulia.? Duu hii nayo Kali sana.
 
Hii ya ndege isiyo na rubani ya kushambulia ikiwa chini ya maji ni sawa na mganda mmoja ameniambia kwao matukio ya ujambazi yanatokea mchana wa manane
 
Back
Top Bottom