Koo langu linahifadhi chakula kama kuku

Koo langu linahifadhi chakula kama kuku

Majigo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
5,519
Reaction score
1,831
Jamani hali hii inanisumbua kila ninapokula , kuna chakula hubakia kooni hivyo hunifanya ninywe maji mara kwa mara ili kukulazimisha kishuke tumboni, lakini bado hung'ang'ania kooni na kuniletea harufu mbaya ya kinywa

Madokta nifanyeje ili ninapokula , chakula chote kishuke tumboni?

Sina raha na koo yangu jamani!
 
ngoja tusubiri madokta mkuu, hospitali nitaenda baadae kufata dawa!!
 
Pole sana kwa ushauri uende kwa doctor wa pua,maskio,na koo. Tatizo la chakula kukaa kooni lina aina nyingi sana zaidi ya 30 inategemea labda hutafuni vizuri chakula au una uvimbe kwenye koo na kusababisha kumeza kwa taabu na ukifikiri chakula kimebaki, au gout (goita) hamna anaeweza kujua sababu kwa kuambiwa tu itabidi ukafanyiwe endoscopic ambapo mrija utaingizwa kooni na kuangalia nini tatizo au utapigwa x-ray ya shingo. Nakuombea kila la kheri
 
mkuu mi huwa ninameza kwa pupa mpaka koo huniuma
 
kwenye kuku huwa hiyo hali ina faida gani? Je wewe hutaki faida hiyo? Kuna kitu kinaitwa evolution. Labda ndo inaanzia kwako na vizazi vijavyo vtakuwa hivyo. Kumbuka binadamu tulivyo sasa sio tulivyoanza, kumekuwepo na maboresho kulingna na mahitaji na ugunduzi mbalimbali. Hata Microsoft ana version mbalimbali za Windows
 
Badili utaratibu wa kula kama unajijua unakula kwa pupa maana naona hapa sasa tatizo ni ubongo
 
kwenye kuku huwa hiyo hali ina faida gani? Je wewe hutaki faida hiyo? Kuna kitu kinaitwa evolution. Labda ndo inaanzia kwako na vizazi vijavyo vtakuwa hivyo. Kumbuka binadamu tulivyo sasa sio tulivyoanza, kumekuwepo na maboresho kulingna na mahitaji na ugunduzi mbalimbali. Hata Microsoft ana version mbalimbali za Windows

mkuu faida yake mi siijui, pia mi sitaki hizo faida kwani mimi sio kuku
so unamaanisha kuwa na chakula kooni ni evolution?
 
Ha ha ha, huwa wanakushikia binduki kumeza?

hapana mkuu, hata mimi najishangaa ..najikuta siwezi kula polepole yaani mpaka mishipa ya kichwa hunisimama hata kuniuma sana, kutokana na kula kwangu kwa pupa!
 
unahitaju nidhamu ya kufundishwa kula taratibu na kutafuna hadi kina lainika!

nimekuelewa mkuu
sasa nitawezaje maana nikitafuna taratibu naona kama najitesa vile
ahsante sana kwa ushauri wako!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom