Kongole kwenu Shaban Kisu na DPC Gerson Msigwa

RtsHjcq

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,753
5,504
Wakuu Habarini.

Ijulikane kwamba Taifa huwa na hafla mbalimbali, lakini pia ni lazima kunakuwepo na washehereshaji wa shughuli husika.

Hata kama hamjapongezwa na waTanzania mimi nimeamua kuwapongeza hapa JamiiForums.

Kwanza, kwa nianze kumpa kongole nyingi sana huyu Bw. Shaban Kisu kwa utendaji wake. Nimemfuatilia sana ni mzee mmoja ambaye anayefuata itifaki(protocol) sana kwenye shughuli zake.

Pili nimpe kongole nyingi DPC Gerson Msigwa, yupo kwenye kitengo cha mawasiliano Ikulu pale Chamwino, jamaa mmoja ambaye ana sauti special sana akiwa anazungumza + protocol ya hali ya juu.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu: Kongole nyingi kwa MPOKI, huyu Bwana Mkubwa kwenye vita ya maneno hafai, huyu yupo idara za Harusi, events za wasanii etc.

Vipi kwenu wakuu mna lolote la kuongezea?

Pokeeni salaamu zangu.

Ni hayo tu.
NAWASILISHA.
 
Huyo Shabani Kissu alishawahi pewa ukuu wa wilaya akaboronga! Mpaka leo anasaka teuzi lakini hafiti kwenye uongozi. Huo u MC ndio unamfaa zaidi!
 
Acha roho mbaya, SIJATUMWA.

penye kusifia, tusifie kwani huoni vijana wanaitwa wazee? Hizo ni lugha tu za kimsimu ok ngoja nikuulize.

Wababa wenye familia huko wanapoitwa baby, kwani ni vibaby kweli?
Nawajua hao Wawili Kiutendaji kitasnia na Kitabia kuliko uwajuavyo Wewe, ila ngoja tu nichague Kunyamaza.
 
Nawajua hao Wawili Kiutendaji, Kitasnia na Kitabia kuliko uwajuavyo Wewe, ila ngoja tu nichague Kunyamaza.
Ok Mkuu,nimekuelewa + nimekubali kuwa mwanafunzi wako..

Hizo zilikuwa perspective zangu tuu,japo kiundani siwafahamu kabisa...huwa navutiwa sana na shughuli zao
 
Hujaweka Number Yako Ya Simu Kwenye Thread
Nakukumbusha Unaweza Kuokota Dodo Kwenye Muarobaini!!
 
Ok Mkuu,nimekuelewa + nimekubali kuwa mwanafunzi wako..

Hizo zilikuwa perspective zangu tuu,japo kiundani siwafahamu kabisa...huwa navutiwa sana na shughuli zao

Yaani unavutika na kazi za kina Shaaban kisu za kusifu na kuabudu??.jamani dunia hii bora tufe tu
 
Back
Top Bottom