Katiika washirika 4 wa mdahalo , watatu waliongea mambo ya maana, Balile aliadhirika
1. Balile anasema kazi ya Waandishi wa habari 'ni kuonyesha Panya alipo si kukamata''.
Dakika 5 baadaye anasema Waandishi wa habari wa set agenda ya maridhiano.
Ni kana kwamba hiyo si kukamata panya ni wajibu wao. Nani alisema kazi yao ni kusimamia maridhiano!
Kwa wasioujua Balile ni mmoja wa wenyeviti wa kamati ya kusukuma maridhiano akiwemo Odero.
Mijadala ya maridhiano yeye ndiye kiongozi na kupitia hapo anapona njaa!
2. Anaambiwa mchakato wa kupata majaji Kenya na Tanzania ni tofauti, hajui tofauti, kwa kutojua au uchawa
3. Anaulizwa aliandika nini kuhusu Mo29 anasema nyumba ya serikali iliyoungua akisindikizwa na Polisi.
Akiulizwa kama aliona maiti, anasema yeye si Daktari. Balile alijua nyumba inaungua bila kuwa '' fire fighter'' hajui tofauti ya mtu aliyelala au kufa
3. Balile anasema Tume ya Chande na Lila itabaini waliochochea ! Balile hajiulizi nani alipiga watu risasi
4. Kuhusu utekaji Balile anatetea hoja mbili za CCM na Polisi kwa kuchagua mifano ya hovyo
Balile haelezi maelfu ya waliopotea akiwemo mwenezi wa CCM na Wapinzani
Balile haamini kama kuna utekaji hata kama Tume ya Chande imesema ni moja ya sababu
Balile anaamini wanaoptea ni sababu za mapenzi!! Aisee
5. Balile anaamini Tume ya Chande ilimaliza kazi ingawa hajaona ripoti nzima na wala hakujishughulisha kuuliza
Huyu mtu jana kafungua kichwa chake watu wameona kina nini! Mwenyekiti wa TEF! Nchi hii ina matatizo mengi
JokaKuu