Kongole Khalifa wa The Chanzo

Kongole Khalifa wa The Chanzo

Vijana kadha wa kadha ambao nimepata kuwasiliana nao wanaonekana kum follow Thatboykhalifa. Anaonekana kujipambanua kama Mwandishi anayeamini zaidi katika weledi na maadili ya Uandiahi wa habari kwa kuwa impartial, trustworthy, fearless and inquisitive.

Nimeona clip Moja akidaiwa kuwa yeye ni CUF ( Sina hakika labda ni kweli au si kweli maana hata aliyemtuhumu Halifa kuwa ni CUF hata yeye aliwahi tuhumiwa kuwa ni CUF so labda waliwahi kukutana katika Kazi za CUF). But, yote Kwa yote Khalifa anajitajidi sana nadhani hata kuondoka kwake katika Gazeti la The Citizen kulitokqna na kuandika habari ambayo baadhi ya Viongozi hawakuipenda na hivyo kumletea zengwe.
 
Sababu Zilizofanya Kampuni Iliyosajiliwa Falme za Kiarabu na Rostam Aziz Kuweza Kununua Kampuni ya Gesi Tanzania Kwa Shilingi 26,000 (Tsh. 26,000)

Mnamo Aprili 13, 2026, kampuni ya Orca Energy iliyoendesha vitalu vya gesi vya Songosongo kwa takribani miaka 25 ilitangaza kuwa imefikia uamuzi wa kuuza biashara yake ya gesi Tanzania kwa takribani dola kumi, ambayo ni sawa na Shilingi 26,000 za kitanzania.

Kampuni hiyo ilitangaza kuwa wanunuzi ni ushirika wa wawili yaani kwanza kampuni ya Amber Energy Investment kutoka Falme za Kiarabu, ambayo ndio itakuwa mmiliki mkubwa kwa asilimia 51 ya hisa; mmiliki hasa wa kampuni hii hajawekwa wazi.

Mshirika wa pili ni Taifa Gas, kampuni inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz, ambaye atachukua asilimia 49 ya hisa. Kampuni hii kupitia kampuni zake za Pan African Energy Corporation (Mauritius) na PanAfrican Energy Tanzania (PAET) ndio mzalishaji mkubwa wa gesi inayotumika kwenye viwanda na umeme Tanzania.

Kati ya mwaka 2021 mpaka mwaka 2025 pekee kampuni hii inayoendesha visima kadhaa vya gesi katika eneo la Songosongo iliweza kupata mapato ya takribani dola milioni 513 ambazo ni sawa na Trilioni 1.3 za Kitanzania.

Sasa imekuwaje ‘mmiliki asiyefahamika’ na Rostam Aziz kuweza kununua kampuni hii kwa shilingi 26,000 pekee?

Soma zaidi>>>Sababu Zilizofanya Kampuni Iliyosajiliwa Falme za Kiarabu na Rostam Aziz Kuweza Kununua Kampuni ya Gesi Tanzania Kwa Shilingi 26,000 (Tsh. 26,000) - The Chanzo
 
Jamaa yupo Vizuri, The Chanzo ni Moja Kati ya Platform nzuri kufatilia wako professional sana

Kuna Hawa wingine wanaitwa Nijuze sijui mmiliki ni nani na wao wapo Vizuri
 
Gentleman,

Vyombo vya habari na waandishi wa habari wengi Tanzania, wanafanya kazi zao kwa weledi mkubwa mno na kwakweli wote wanafaa kupongezwa kwa ukubwa na umuhimu wa kazi zao katika ujenzi wa Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu bariki vyombo vya habari na wanahabari wote nchini.
Fyokoriko wewe mpongeze alie TAJWA sio akina balile na kamasi nyingine
 
Back
Top Bottom