Kongamano za ngurumo ya upako

mtzmweusi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
8,640
8,966
Wakuu nipo naangalia channel 10 muda huu kuna kipindi cha huyu mtumishi anaitwa Geor Davie nimeshangazwa na jambo moja makongamano yake yote kuna viingilio tena hela ndefu swali langu ni moja hii ni biashara au huduma? Umepewa bure toa bure
 
Wakati mwingine hupata fikra kuwa wakati wa mwalimu ilikuwa bora kuliko sasa. Serikali ilikuwa na udhibiti wa vitu ambavyo kwayo vilikuwa na manufaa.
Utasijiliza rtd pekee vipindi kam Mkulima wa kisasa, chakula bora nk. Tofauti na sasa ulipie king'amuzi halafu unakwenda tazama wachungaji wa aina hiyo. Mwidho wa siku jamii inanufaika na nini?
Nafikiri jinsi tunavyokuwa na shule pamoja na vyuo vinngi ndio ujinga unaongezeka.
 
Mkuu una uhakika gani kama ALIPEWA BURE?! Hii miujizi hii apewe bure?! thubutu.
 
Wakuu nipo naangalia channel 10 muda huu kuna kipindi cha huyu mtumishi anaitwa Geor Davie nimeshangazwa na jambo moja makongamano yake yote kuna viingilio tena hela ndefu swali langu ni moja hii ni biashara au huduma? Umepewa bure toa bure
yeye hajapata bure, amesotea muda kujifunza na kupata huo ujanja ............
 
Mambo ya Mungu sio biashara umepewa bure toa hiyo karama bure kwa watu
 
Huyu mtumishi ana tittle kubwa.Askofu Mkuu,Nabii & Mtume Dr Mstahiki Mheshimiwa sana Geor Davie haaa haaaa haaa halafu ana walinzi kama Rais wa USA.
 
Haahaaa wajinga wengi wanaliwa pale, pesa ya LEMBELI imeliwa mno na huyu mtu maana mke wa jamaa ni muumini kindakindaki wa NABII MKUU SANA MSTAHIKI MTUME DR GEODAVIE. Sijui sasa anambiwa nini maana ubunge umegonga.
 
Kuweni makini na manabii watakaojitokeza siku za mwisho,wapo wa ukweli lakini wa uongo ni wengi zaidi.
 
Kweli mkuu.. Nigeria miaka kumi halafu useme kapewa bure? Ila ukiona hela ndefu wasiliana na kitwanga itakuwa fupi.
 
Back
Top Bottom