Kongamano ya Katiba mpya UDSM-maadili ya kitaifa vipi?

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
e: Kongamano la Katiba na Hoja ya Mnyika

quote_icon.png
Originally Posted by Didia
Katika kongamano lililoisha juzi UDSM mada kuu iligusa maeneo makuu matatu: Haja, Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya. Wajumbe wote walionekana kukubalina hususani na kipengele cha kwanza-Haja ambapo kila mtu alionesha kuwepo umuhimu wa kupata katiba mpya. Hivyo hapo hakuna mjadala zaidi.

Katika kipengele cha pili kinachozungumzia mchakato yaani katiba ipatikane kupitia njia/utaratibu upi mpaka sasa kuna hoja tatu zinazokinzana. Napenda nizipe majina yafuatayo:

1. Hoja ya Rais: Rais kuunda tume ikusanye maoni na kutoa ushauri ambao utashugulikiwa na vyombo vya kikatiba. Maoni ya wajumbe yalionesha kuwa kauli ya Rais haiko wazi na wengi wanaamini kuwa utaratibu wa tume ya Rais hautaleta matunda yenye kutarajiwa kama historia inavyoonesha.

2. Hoja ya Mnyika: Kupeleka Hoja Binafsi Bungeni, yafanyike marekebisho ya katiba kuingiza ibara itakayo toa muongozo jinsi ya kutunga katiba mpya. Itungwe sheria inayo unda chombo cha kuratibu maoni ya wananchi......

3. Hoja ya Shivji (tunaweza kuiita pia mtazamo wa Asasi za Kiraia): Tume ya Rais isimamie mchakato wa kukusanya maoni, iwe wazi, isiripoti kwa Rais bali kwa wananchi.
Hoja iliyotolewa na Shivji ni kwamba Mnyika akipeleka hoja ya katiba bungeni matokeo yake huenda yasiwe mazuri ikizingatiwa wingi wa wabunge wa CCM. Mtazamo huu unaimanisha kuwa hoja ya katiba ikionekana kuwa himaya ya chama fulani patakuwepo mgawanyiko kati ya wananchi/wadau na huenda pasiwepo msukumo wa kutosha. Mapendezo yaliyotolewa ni kwamba nguvu sasa ihamie (i) kusukuma Rais aunde tume ambayo haita ripoti kwake, bali kwa wananchi. (ii) Katiba isiandikwe na Mwanasheria Mkuu bali wajumbe watakao teuliwa na bunge la mda (Constituency Assembly)


Je, kuna haja ya Mh. Mnyika kuendeleza mchakato wa hoja binafsi? Nini itakuwa athari au faida za kupeleka hoja binafsi bungeni? Je kama unakubalina na hoja za Shivji ni mikakati gani tufanye kufanikisha hilo?


  • Kwakuwa swala lamaudhui (yaani tuwe na katiba ya namna gani ni pana sana, naomba mjadala ujikite zaidi kwenye mchakato i.e njia ipi itumike kupata katiba mpya)
Ahsateni karibu kuchangia.



Hayo maeneo ya rangi nyekundu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Bila mwongozo wa kisheria kuupa mustakabali huu wa kitaifa nguvu ya kisheria, itabaki ni suala la hisani, au utashi wa mtu binafsi, jambo ambalo ni hatari kuliko yote!!!!!!!!!!!
Mheshimiwa Mnyika endelea na azma yako kufikisha hoja hii bungeni ili tupate national commitment ya kisheria, na pia kuwapa wananchi nafasi ya kupima integrity ya wabunge kuhusu suala hili ambalo ni la uhai wa kitaifa kwa vizazi vijavyo, ambalo hatuhitaji kuhusisha vested interests za vyama ama makundi katika jamii. Bila nguvu ya sheria kulinda mchakato huu, kuna makundi yatateka nyara mchakato sas hivi , jambo ambalo kuna hatari ya kuzua mgogoro mkubwa sana wa kitaifa!!!!!!!!!!!!!!
Kama suala la vyama vingi lilivyokuja-njia hiyo hiyo italeta katiba mpya-pressure kubwa kutoka ndani na nje!!!!!!!!!!
Mimi nawaomba wabunge walipe suala hili top priority katika agenda yao ili kunusuru taifa hili!!!!!!!!! Kuna hisia za kweli kwamba jambo hili litaishia kuvutana vutana hadi mwaka 2015 unafika katiba mpya inayotamaniwa haijapatikana!!!!!!!!!!!! Hivi kumbe ndiyo maana Kenya walifuata njia ya kuchinjana kama kuchinja kuku au mbuzi-ni kwa sababu ya uvutano uliochukua miaka mingi.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Hapa Tanzania ziko dalili za wazi,ukisoma between the lines, mijadala inayoendelea, kwamba watu usiowatarajia waki-advocate njia huria za kupata katiba mpya!!!!!!!!!!!!! Katiba Mpya inayotamaniwa na wananchi wa taifa hili ni kama kuleta risasi za moto kuwapiga na kuwaua wenye nchi hii!!!!!!!!!!!!!!! Hivyo siamini kama itakuwa rahisi na mtelemko kama invyoelekea kuaminiwa na supporters wa mchakato huria!!!!!!!!!!!!!!!!!​

progress.gif
Edit Post Reply Reply With Quote Thanks
 
Back
Top Bottom