Kongamano la Uhuru Live Kutoka Nkrumah UDSM

Kongamano la Uhuru Live Kutoka Nkrumah UDSM

Membe naona anajipigia kampeni sasa! Anauliza maswali halafua anatoa majibu rahisi tu ambayo ccm wangeshayatumia kuleta mabadiliko. Sasa sijui anaongea nini wakati yeye ndiyo waziri
 
Magazeti ya Tanzania yanatoa research za kipumbavu According to Membe, hapo pamekaaje wadau?
 
Leo Esther amejawa na jazba za kisiasa mpaka amevuka mipaka yake ya kuwasilisha mada vizuri kama alivyofanya katika kongamano lililopita. Alikuwa na hoja nzuri tu, kama angeziwasilisha kwa utulivu angekuwa mmoja kati ya wachangiaji waliofanya vizuri. Sijui amepatwa na nini leo.
 
Hivi haya Mawazo mazuri ya Makamba jnr anayoengea hapo hawezi kuyawakilisha huko jikoni? Mbona wakiyafata mambo yatakuwa mazuri
Mkuu hawa wamesoma upepo, wamechoka kuzomewa, kwenye audience watajifanya wako pamoja nanyi wakifika kwenye vikao vyao wanapanga jinsi ya kuwaibia. Nimemsikia Membe nae anaongea kwa authority utafikiri ni rais tayari, siasa balaa!!!
 
Kweli zile dakika nane niliona kama sekunde nane,kamanda Esther ni jembe la ukweli.keep it up kamanda.
 
eeehhh Butiku anamwambia Makamba akarudi akasome historia ya ELimu

duuuuuh huyu mzeee anapiga vijembe kimya kimya

Hili lilikuwa swali la kijinga kutoka kwa makamba kuwa eti wazee walikuwa wanafanya nini muda ule kurekebisha ubora wa elimu?
Kalewa hela za madini huyo kwani walikuwa na zitto kamati moja, ndo maana nilipochangia awali nilimkataa huyo na membe kwa sababu hawana jipya.
 
Leo Esther amejawa na jazba za kisiasa mpaka amevuka mipaka yake ya kuwasilisha mada vizuri kama alivyofanya katika kongamano lililopita. Alikuwa na hoja nzuri tu, kama angeziwasilisha kwa utulivu angekuwa mmoja kati ya wachangiaji waliofanya vizuri. Sijui amepatwa na nini leo.
Ana uchungu tu na nchi, mbona,hiyo jazba sijaiona?
 
Kwa hali ilivo sasa Tanzania kuna utulivu 2 amani imetoweka na ndio maana tunashuhudia sasa polisi wakiwaua raia wasiona hatia, kwa kisingizio cha kulinda amani. Matabaka ya wenyefedha nyingi haramu, na matumizi mabaya ya madaraka na Ubinafsi wa watumishi na viongozi wa umma umechochea kwa kiwango kikubwa kuibuka kwa manung'uniko mengi kwenye jamii sasa. wezi wa mali za umma Mafisadi kuingia kwenye uongozi wa umma ni vichocheo vikubwa vya kutoweka kwa amani.
 
ukisoma hotuba ya esther amrelezea vizuri sana
 
Jamani kwa hakika mwanaharakati wa CHADEMA tajwa hapo juu alinikuna vilivyo ndani ya Ukumbi wa Nkrumah nikasikia mwili unanisisimka mithili ya mtu aliepita jirani na kwa mganga wa jadi...

Esther ni nani?, ni binti wa nani katika katika vigogo wa siasa za Tanzania?

Esther amedhihirisha kuwa ni Mwanamama hasiena uwoga wowote kwa jambo la kitaifa na kama anao uwoga basi ni JASIRI maana anaushinda uwoga huo tofauti na wengi wetu tunaolalamikia majumbani mwetu..

Esther aliongelea mambo ya MSINGI sana na ya kitaifa, yanayotia KICHEFU CHEFU lakini kwa magamba ni mambo ya KUJIVUNIA!

Esther kaongelea haki za wanahabari mfano kifo cha Mwangosi, ufisadi wa mali za umma mfano vijisenti, niongezeee, HATA KAMA MTAKULA NYASI NDEGE TUTANUNUA....

Jamani ni muda mwafaka watanzania tusidanganywe, kama alivyosema Deo, Tanzania si mali ya CCM, tuwawajibishe hawa IRRESPONSIBLES....

Nawasilisha....:wof:
 
Easy now before all this praise gets to her head.

Rhetoric alone shouldn't cut it.
 
Jamani kwa hakika mwanaharakati wa CDM tajwa hapo juu alinikuna vilivyo ndani ya Ukumbi wa Nkrumah nikasikia mwili unanisisimka mithili ya mtu aliepita jirani na kwa mganga wa jadi...

Esther ni nani?, ni binti wa nani katika katika vigogo wa siasa za Tanzania?

Esther amedhihirisha kuwa ni Mwanamama hasiena uwoga wowote kwa jambo la kitaifa na kama anao uwoga basi ni JASIRI maana anaushinda uwoga huo tofauti na wengi wetu tunaolalamikia majumbani mwetu..

Esther aliongelea mambo ya MSINGI sana na ya kitaifa, yanayotia KICHEFU CHEFU lakini kwa magamba ni mambo ya KUJIVUNIA!

Esther kaongelea haki za wanahabari mfano kifo cha Mwangosi, ufisadi wa mali za umma mfano vijisenti, niongezeee, HATA KAMA MTAKULA NYASI NDEGE TUTANUNUA....

Jamani ni muda mwafaka watanzania tusidanganywe, kama alivyosema Deo, Tanzania si mali ya CCM, tuwawajibishe hawa IRRESPONSIBLES....

Nawasilisha....:wof:
asante kwa kuyaona hayo bali hapo kwenye red ndipo tatizo lilipo mpaka wengine wamefikia hatua ya kutaka kubadilisha jina la nchi wakidhani na watu wake tutabadilika. Kwa maana kuwa mtz ni kudanganyika!
 
Tukiondoa uwoga yootee haya hayawezi kutokea hapa Tanzania, tatizo letu uwoga na kudumisha fikra za Mwenyekiti... Lakin nina imani kuna watu tunafanya kila liwezekanalo kuondoa uwow huuu...
 
Ester alisisimua sana, ni kwlei. Lakini kwanini iwe hivyo.... Nafikiri kwanza kwasbabu ya kujadili hoja za kitaifa zaidi kuliko uchama, pili kwa kuwa yeye ni mwanamke jasiri. Hivyo basi hii ni dhahiri kwamba wapo wanawake wengi ambao ni majembe. Lakini wengi wenu hampo tayari kufanya hivyo hadharani sijui kwanini. Mfano kwenye maoni ya katiba ktk mikutano karibia yote niliyohudhuria, wanawake wanaochangia ni kama 30% tu ya watu wote, kisa woga. Hii itasababisha hata kile mnachokisema haki sawa kwa wote kisipatikane haraka kwasababu ya woga wenu.
 
esther WASSIRA, so strong, tough and beautiful. Kudos!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom