Shikilia hapo hapo.
Lakini sasa ni lazima muwe na mkakati maalum na mpangilio mzuri wa haya mambo yote mnayofanya, isije ikawa ni moto wa mabua.
Hawa wanaohudhuria makongamano, inaelekea wengi wao tayari ni wanachama wenu au wapenzi wa chama. Hakikisheni hawa wanaiva vizuri kutokana na makongamano hayo, na hawa ndio watakaoeneza habari kwa wananchi wote nchi nzima.
Yasije yakawa madoidoi tu, wanapotoka hapo na wao wasiwe wanajuwa kitu!
Kumbukumbu zenu zinaonyesha maendeleo mnayofanya hadi sasa? Mnayo 'feedback' ya kujuwa wapi pana udhaifu ili mrekebishe mapema?
Mnajuwa mmepata mafanikio kiasi gani hadi sasa, tokea muanze shughuli hizi?
Ni lazima mfanye mambo kisayansi, vinginevyo hata wakati mkiboronga bila ya kufanyiwa faulo yoyote, msigeuke kulaumu wengine kwa lawama zinazowahusu nyinyi wenyewe kwa kutojuwa mnachofanya na matokeo yake ni yapi.
Ushauri ni ushauri tu.