Kongamano la katiba - ARUSHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano la katiba - ARUSHA

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Crashwise, Dec 7, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  leo kuanzia saa saba na nusu kwenye ukumbi wa Manor Hotel kutakuwa na kongamano la katiba mpya litakaloongozwa na viongozi wa chadema kutoka makao makuu...mnaombwa kufika
   
 2. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tunawatakia Kila la kheri. Katiba ni maisha yetu, ndo kila kitu. I hope wanaArusha wataipa umuhimu jambo hilo.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Hili ni jambo la heri CDM lazima washiriki mijadala ya katiba wakisusa upo uwezekano mkubwa katiba mpya ikawa mbaya kuliko hii ya sasa.Yapo mambo mengi sana yanayohitaji kubadilishwa kati ya mambo hayo kubwa kuliko yote ni tume huru ya uchaguzi.

  Tume huru ya uchaguzi inatuhakikishia wapiga kura kwamba mTanzania alipigiwa kura nyingi ndiye anakuwa mshindi na anapata nafasi ya kutuongoza.Tume ya uchaguzi ya sasa ni kituko muundo wake haufai inakaribisha fujo pasipo sababu za msingi.Nina uhakika tangu uchaguzi wa vyama vingi uliporuhusiwa rasmi mwaka 1992 jimbo la Arusha mjini CCM walishinda mara moja tu baada ya matokeo ya ushindi wa Mheshimiwa Makongoro Nyerere kubatilishwa na mahakama CCM ilishinda kwakuwa NCCR iliyumba sana lakini chaguzi zilizofuata upinzani ulikuwa ukishinda kwa kura nyingi lakini tume mbovu na mfumo mbovu wa uchaguzi uliweza kubadili matokeo kinyume na matakwa ya wapiga kura.Uchaguzi wa Mwaka 2010 hali ilitaka kujirudia kama si nguvu ya umma Arusha ingewakilishwa na mbunge aliyeshindwa kwa mara ya tatu mfululizo.

  Matokeo ya uchaguzi jimbo la Ubungo na Kawe jijini Dar yalicheleweshwa kutangazwa nia ikiwa ni kuharibu ushindi wa wapinzani.Unaweza kujiuliza wilaya za Kinondoni au Ilala zenye miundombinu rahisi matokeo yanaweza kucheleweshwa kwa zaidi ya siku nne au tano je wilaya za pembezoni hali ikoje ?.Jibu ni rahisi sana Tume huru ya uchaguzi kama ya jirani zetu Kenya itaondoa uwezekano wa kuchakachua matokeo hence viongozi wabovu hawatakuwa na nafasi ya kutuongoza mwisho mwananchi [mpiga kura] ndiye mshindi kwakuwa atakuwa na uhakika chaguo lake na si chaguo la tume mbovu ya uchaguzi.

  Matokeo ya urais yahojiwe mahakamani kama ilivyo kwa wabunge na madiwani.


   
Loading...