Kongamano la aliyekua Mwanasheria mkuu wa Zanzibar Othman Masoud lavamiwa na jeshi la polisi

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Leo tarehe 18/12/2016 kumetokea kioja chengine Zanzibar baada ya Kongamano lililondaliwa na Vijana wa Vyuo Vikuu wa Chama cha Wananchi CUF – Zanzibar ambalo lilitarajiwa kuhudhuriwa na aliekua Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh. Othman Masoud kuzuiliwa na Jeshi la Polisi.

Kongamano hilo ambalo lilitarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel iliyopo Shangani Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na watu Mashuhuri na Viongozi mbali mbali lilivamiwa na kughairishwa na Jeshi la Polisi kwa kile walichodai kua wamepokea Order kutoka juu ya kulighairisha Kongamano hilo.

Hayo yametokea wakati ambapo waalikwa wa Kongamano hilo walikua ndani ya Ukumbi wa Kongamano wakimsubiri Mh. Othman Masoud ambaye alikua Mgeni rasmi wa Kongamano hilo kuja kutoa mada iliyolenga kuelezea Nafasi ya Zanzibar ndani ya Afrika Mashariki, Fursa ilizonazo na namna ilivodhoofishwa.

Wakati waalikwa hao wakimsubiri Mgeni rasmi huyo ndipo ghafla Defender za Jeshi la Polisi zipatazo 5 zilipovamia eneo la shughuli hiyo huku zikiwa zimejaza askari Polisi waliokua na silaha nzito na mabomu ya machozi.

Kabla ya kufanyika kwa Kongamano hilo mara baada ya Jeshi hilo la Polisi kuvamia maeneo hayo, maafisa wawili wa Jeshi la Polisi waliingia ndani ya ukumbi wa Kongamano na kukagua na baadae kuomba kuzungumza na Vijana walioandaa Kongamano hilo.

Maafisa hao ambao hawakuvaa sare za Jeshi la Polisi walikaa na Vijana hao na kuwaeleza kua wamekuja kwa lengo la kulighairisha Kongamano hilo.

Wakati Maafisa hao wakidai hivyo Vijana walioandaa Kongamano hilo walihoji sababu za msingi za kusimamishwa kwa Kongamano hilo lakini hawakupatia maelezo ya kuridhisha zaidi ya kuambiwa na Maafisa hao kua wamepokea Order kutoka juu ya kulighairisha Kongamano hilo.

Akitilia mkazo maelezo hayo mmoja wa Maafisa hao alisema kua “hatukutumwa kuja hapa kujadiliana na nyinyi bali tumetumwa kuja kuhakikisha kua Kongamano hili halifanyiki. Hivyo hata tukizungumza tutakua tunapoteza mda tu jambo la msingi ghairisheni shughuli yenu na waambieni walioko ndani watoke kwani hata wakikaa pia hamtofanikiwa kwasababu tayari nje tumeshazuia watu wasiingie katika maeneo haya”.

Maafisa hao wa Jeshi la Polisi walisema kua watakuwepo katika maeneo hayo na hawatoondoka na kwamba hawatoruhusu mtu yoyote alie nje kukaribia maeneo hayo.

Wakati hayo yakiendelea kwa upande wao Vijana walioandaa Kongamano hilo waliwaamuru waalikwa waliohudhuria Kongamano hilo kurudi katika maeneo yao na kuwaomba radhi kwa yaliyotokezea.

Vijana hao walisema kua kitendo hicho cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuvuruga Kongamano hilo ni kinyume na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 tolea la 2010 ambayo ibara ya 25 (1) inatoa haki ya Uhuru wa watu kukusanyika na kujieleza.

Pia Vijana hao walisema kua lengo la kufanya Kongamano hilo halikua kutukana Viongozi kama wanavyotukana Vijana wa CCM wala Kongamano hilo halikua na lengo la kufanya siasa bali Kongamano hilo lilikua na lengo la kujifunza kutoka kwa nguli huyo wa sheria. ” hatukutaka kufanya Kongamano hili kwa lengo la kuwatukana Viongozi wa kisiasa kama wanavyofanya Vijana wa CCM katika Makongamano yao, wala hatukutaka kufanya Kongamano hili kwa lengo la kufanya siasa bali tulihitaji kujifunza mambo mbali mbali kutoka kwa Othman Masoud hasa kwa vile sisi ni Wanafunzi ndio maana tukapendekeza Othman Masoud awe Mgeni rasmi wa Kongamano letu. Kama tungehitaji kuwatukana Viongozi wa Kisiasa basi tusingemualika Othman Masoud na kama tungehitaji kufanya siasa basi bila ya shaka tungewaalika Viongozi wa Chama chetu”. Alisema mmoja wa Vijana hao katika mahojiano na redio Adhana FM.

Pamoja na hayo Vijana hao wamesema kua kitendo hicho cha leo ni mfululizo na muendelezo wa utumikaji mbaya wa Jeshi la Polisi ambapo Vijana hao wamesema kua Jeshi hilo limeamua kwa maksudi kutumika kwa maslahi ya Vibaraka wa CCM.

Vijana hao wamesema kua kitendo hicho sio cha kwanza kufanyiwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar na kukumbushia namna ya Jeshi hilo la Polisi lilivyotumia nguvu kubwa katika Uchaguzi wa ZAHILFE na kulazimisha kijana wa CCM kua M/kiti wa ZAHILFE March 2016.

Pia wamesema kua katika Uchaguzi wa SUZA uliofanyika tarehe 5/01/2016, Jeshi hilo la Polisi lilitumia nguvu kubwa na kuvamia maeneo ya Chuo hicho ili kumsaidia kijana wa CCM kuupora ushindi wa alieshinda Uchaguzi huo.

Wakiendelea kufafanua nguvu hizo za Jeshi la Polisi katika kuitumikia CCM Vijana hao wamesema kua Chuo cha Zanzibar University nacho kilikumbwa na sakata la kupinduliwa kwa Serikali halali ya Chuo hicho ambapo uchaguzi wake na raisi na Viongozi wote wa Serikali walikwishaapishwa takribani miezi Mitano nyuma na kufanya kazi kwa mda mrefu lakini pamoja na hayo CCM waliipindua Serikali hiyo na kuitisha uchaguzi mwengine ambao haukuhudhuriwa na hata robo ya Wanafunzi wa Chuo hicho.

Pamoja na madudu yote hayo yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika Vyuo mbali mbali Vijana hao wamesema kua leo hawakua na lengo la kuyazungumzia madudu hayo katika Kongamano hilo bali walikua na lengo la kujifunza kwa Mwanasheria Mkuu huyo wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Walipoulizwa nini watafanya baada ya kuzuiliwa kwa Kongamano hilo la leo? Vijana hao walisema kwamba kwanza kuzuiwa kwa Kongamano hilo hakujawavunja moyo na kwamba wataendelea kufanya shughuli zao kama kawaida na hivi karibuni watatoa taarifa ya Kongamano jengine.

Pia Vijana hao walilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya matumizi yao ya nguvu kwa Vijana na kusema kua matumizi hayo yanaweza kuliingiza taifa katika machafuko pale Vijana watakapochoshwa na matumizi yao ya nguvu.
 
Hofu hii itawaisha lini? Mbona mnatendewa kama ni wahamiaji haramu? Serikali itambue umuhim wa katiba na kuwaamini raia wake.
 
Hawana kazi za kufanya?? Waende wakajishughulishe huko na uzalishaji Mali. Huu si wakati wa mchezo!!
 
Ila polisi wakishirikiana na viongozi wa ccm wanarudisha sana maendeleo ya wananchi wao nyuma, sijui wanaonashida gani watu wakipata maendeleo. Sijapata kuona nchi ambao viongozi wanafurahia umaskini wa raia wake kama Tanzania
 
CCM bila polisi ni wepesi kuliko pamba .

Polisi wanatumiwa vibaya na wanaCCM magu et al
Polisi wanatumiwa vibaya na Matajiri Majaliwa et al.

Ivi polisi hawajiongezi tu na kejeri hizi wanazopewa tena na watu wakubwa wa nchi hii????
Polisi tafakari chukueni hatua akseh mnajidhalilisha
 
Kwa hiyo kwa kufanya hivyo ccm inafikiri ndiyo itapata wafuasi, akili ndoto ni akili ndoto tu
 
Othman Masoud inawezekana chuki yake kwa Muungano imemsahaulisha kirefu cha SMZ!
 
halafu ile si hotel ya kitalii, kama askari wametanda si wameharibu biashara yake, na kuleta uoga, manake wenzetu wakiona askari wamekusanyika hivyo wanakuwa waoga sana, na kuanza itangaza vibaya zanzibar
 
Polisi wanatumiwa vibaya na wanaCCM magu et al
Polisi wanatumiwa vibaya na Matajiri Majaliwa et al.

Ivi polisi hawajiongezi tu na kejeri hizi wanazopewa tena na watu wakubwa wa nchi hii????
Polisi tafakari chukueni hatua akseh mnajidhalilisha
Aibu ya binadamu inahitaji pia kiwango fulani cha elimu , hivi unafahamu kwanini habari ya vyeti feki imetoweka ?
 
Back
Top Bottom