Kondoo wa Korani agawanya familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kondoo wa Korani agawanya familia

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Salimia, Aug 9, 2011.

 1. S

  Salimia JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  SAKATA la kondoo aliyezaliwa akiwa na maneno ya Kiarabu yenye maana ya neno Yasini, neno ambalo ni moja ya aya katika Koran Tukufu, limechukua sura mpya baada ya familia inayomiliki kondoo huyo kugawanyika. Wakati habari iliyoripotiwa na gazeti hili katika toleo lake la Jumapili (juzi) ikieleza kuwa familia hiyo ya kijiji cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, inayomiliki kondoo huyo ni ya Kikristo, ameibuka mmoja wa wanafamilia, Said Massawe na kusema si kweli kwamba familia hiyo ni ya Kikristo bali ni mchanganyiko wa Wakristo na Waislamu. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Massawe alisema hatua ya kusema kuwa familia hiyo ni ya Kikristo pekee, imesababisha manung’uniko ndani ya familia kwa vile haijawatendea haki wanafamilia Waislamu. “Familia yetu ni ya mchanganyiko wa dini mbili za Uislamu na Ukristo. Pale nyumbani alipo yule kondoo, mwenye mji ni marehemu babu yetu Mzee Said Massawe, ambaye mimi ndiye nilirithi jina lake. Babu alikuwa Mwislamu na hata marehemu mkewe, yaani bibi pia alikuwa Mwislamu jina lake ni Mwanaidi Massawe. “Si hao tu, hata baba mkubwa Khalifa Said Massawe anayeishi Monduli ambaye alikuwa pale nyumbani, baada ya kuzaliwa kwa kondoo yule, ni Mwislamu. Alikuwapo pia marehemu baba yetu mkubwa marehemu Suleiman Massawe, ambaye ni Mwislamu. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Waislamu ndani ya familia tupo wengi tu ingawa na Wakristo pia wapo,” alisema Massawe. Alisema mama yake anayeishi katika makazi hayo kwa hivi sasa ambaye ndiye aliyelieleza gazeti hili, kuwa familia yao ni ya Kikristo, Grace Eliumini Massawe (55), alizungumzia imani yake yeye binafsi, kwani ni Mkristo, lakini hiyo haina maana kuwa wanafamilia wote ni Wakristo. “Hivi sasa baada ya tukio, baba mkubwa (Khalifa), ametutaarifu wanafamilia wote lakini kwa vile tukio limetokea wakati wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, tumekubaliana kwamba baada ya funga, wakati wa Sikukuu ya Idd wote tuwe Moshi ili tusome Dua na kumaliza kila kitu kwa jambo hili la ajabu lililotokea,” alisema Massawe. Arnold Swai, aliyepo Hai anaripoti kwamba mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu kutoka nje ya Wilaya ya Hai na Mkoa wa Kilimanjaro, wamezidi kumiminika kwa wingi katika kijiji hicho, ili kumshuhudia kondoo huyo wa ajabu aliyezaliwa akiwa na maandishi hayo ya Korani. Kondoo huyo aliyezaliwa Julai 6 amekuwa kivutio kikubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu, ambapo hadi sasa watu kutoka mikoa ya Dar es Saalam, Tanga na Arusha wamefika kushuhudia maajabu hayo. Akizungumza na HABARILEO, Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, alikiri kumshuhudia kondoo huyo na kueleza kuwa maandishi yanayosomeka ubavuni mwa kondoo huyo ni sahihi kama yanavyosomeka katika Kitabu cha Koran. Alisema maandishi hayo ya Kiarabu ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili ni Yasini, moja ya aya muhimu katika Koran pia ni moyo wa Kitabu hicho. “Aya hii ni moyo wa Kitabu Kitakatifu cha Koran, kinaelezea mambo mengi makubwa hususani nyakati za mwisho … inaonesha ishara kuwa hizi ni siku za mwisho za kiyama,” alisema Shehe Mallya. Alisema aya ya maandishi hayo katika Koran ni moja ya sura zinazoeleza mambo mazito, pamoja na kueleza kuwa Kitabu hicho kinazungumzia siku za mwisho za kiyama, hivyo kila mtu atengeneze maisha yake. Aliongeza kuwa hiyo ni ishara kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu, kwa sababu Kitabu Kitakatifu cha Koran kilishushwa Mwezi wa Ramadhan, hivyo ishara hii katika kipindi cha Mfungo Mtukufu wa Ramadhani ni kubwa. Pia Shehe Mallya aliongeza kuwa neno Yasini ni jina lingine la Mtume Muhammad (SAW) alilopewa na Mwenyezi Mungu, na kueleza kuwa hiyo ni miujiza na bahati kwa dini hiyo. “Haya maandishi katika aya ya Kitabu cha Koran yamejikita zaidi kuonesha hizi ni siku za mwisho za kihama, hivyo wakati huo midomo haitaongea tena ila mikono itasema na miguu itashuhudia, hivyo Mungu akipenda jambo lake liwe linakuwa,” alisema Shehe Mallya. Katika hatua nyingine, Shehe huyo alisema walihitaji kumnunua kondoo huyo kwa lengo la kuwa mfugo wa Msikiti, lakini imeshindikana baada ya mmiliki kukataa kumwuza. Akizungumza na HABARILEO nyumbani kwake, mmiliki wa kondoo huyo, Grace, alieleza historia ya kondoo aliyemzaa na kusema alimpata kama mahari kwa binti yake wa pili, na ndama huyo ni uzao wa pili. Grace alisema katika familia yake yenye jumla ya watoto watano, watatu ni Wakristo na wawili ni Waislamu ambao waliolewa na kubadili dini, na hapo awali mumewe ambaye ni marehemu alikuwa Mwislamu na kubadili dini na kuwa Mkristo. Alieleza sababu za kukataa kumwuza kondoo huyo, akisema bado familia haijajua nini maana ya tukio hilo na kwamba inachukulia kitendo hicho kama baraka kwa familia. Alisema hadi sasa watu wawili wamejitokeza wakitaka kumnunua kwa kiasi kinachofikia Sh milioni 10, lakini bado amesisitiza kutomwuza.
   
 2. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Acha kukashif imani za watu.
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu ndo imekuwa hivyo..
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,045
  Likes Received: 6,487
  Trophy Points: 280
  nimepita hapa.
   
 5. Donkey

  Donkey JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 673
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 80
  Mpaka leo bado unawaza uislamu na ukristo, acheni hizo badilikeni, waafrika si waislamu wala wakiristo----------------utumwa wa nini mpaka leo, hakuna kiumbe kinachoweza kuzaliwa na maandishi, maandishi si nature, kama elimu yako finyu unaweza amini hiki, huu ni usanii wa watu fulani kwa maslahi yao, ukweli utajulikana tu
   
 6. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Kitabu Kitukufu cha Korani kilishushwa mwezi wa Ramadhani!
  Hapo napo sijui....
   
 7. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hivi hata mimi si ninaweza kuchora mchoro wa Nyoka Likatokea andiko la kiarabu?
   
 8. Gbollin

  Gbollin JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 589
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kuna vitu ambavyo hatuitaji upeo mkubwa sana kufikiria, hivi kikombe cha babu kimeishia wapi? Nasisitiza hakuna kitu kama hicho na huyo kondoo hajazaliwa na hilo neno bali ni changa la macho tunapigwa. Uongo ukiongelewa sana hugeuka ukweli.
   
 9. B

  BILLY2TRY Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Lugha ya kiarabu ni tofauti na Uislamu
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kiarabu <> Ki-Islam!
   
Loading...