Kondoo wa Koran agawanya familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kondoo wa Koran agawanya familia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Aug 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SAKATA la kondoo aliyezaliwa akiwa na maneno ya Kiarabu yenye maana ya neno Yasini, neno ambalo ni moja ya aya katika Koran Tukufu, limechukua sura mpya baada ya familia inayomiliki kondoo huyo kugawanyika.

  Wakati habari iliyoripotiwa na gazeti hili katika toleo lake la Jumapili (juzi) ikieleza kuwa familia hiyo ya kijiji cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, inayomiliki kondoo huyo ni ya Kikristo, ameibuka mmoja wa wanafamilia, Said Massawe na kusema si kweli kwamba familia hiyo ni ya Kikristo bali ni mchanganyiko wa Wakristo na Waislamu.

  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Massawe alisema hatua ya kusema kuwa familia hiyo ni ya Kikristo pekee, imesababisha manung’uniko ndani ya familia kwa vile haijawatendea haki wanafamilia Waislamu.

  “Familia yetu ni ya mchanganyiko wa dini mbili za Uislamu na Ukristo. Pale nyumbani alipo yule kondoo, mwenye mji ni marehemu babu yetu Mzee Said Massawe, ambaye mimi ndiye nilirithi jina lake. Babu alikuwa Mwislamu na hata marehemu mkewe, yaani bibi pia alikuwa Mwislamu jina lake ni Mwanaidi Massawe.

  “Si hao tu, hata baba mkubwa Khalifa Said Massawe anayeishi Monduli ambaye alikuwa pale nyumbani, baada ya kuzaliwa kwa kondoo yule, ni Mwislamu. Alikuwapo pia marehemu baba yetu mkubwa marehemu Suleiman Massawe, ambaye ni Mwislamu.

  Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Waislamu ndani ya familia tupo wengi tu ingawa na Wakristo pia wapo,” alisema Massawe.

  Alisema mama yake anayeishi katika makazi hayo kwa hivi sasa ambaye ndiye aliyelieleza gazeti hili, kuwa familia yao ni ya Kikristo, Grace Eliumini Massawe (55), alizungumzia imani yake yeye binafsi, kwani ni Mkristo, lakini hiyo haina maana kuwa wanafamilia wote ni Wakristo.

  “Hivi sasa baada ya tukio, baba mkubwa (Khalifa), ametutaarifu wanafamilia wote lakini kwa vile tukio limetokea wakati wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, tumekubaliana kwamba baada ya funga, wakati wa Sikukuu ya Idd wote tuwe Moshi ili tusome Dua na kumaliza kila kitu kwa jambo hili la ajabu lililotokea,” alisema Massawe.

  Arnold Swai, aliyepo Hai anaripoti kwamba mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu kutoka nje ya Wilaya ya Hai na Mkoa wa Kilimanjaro, wamezidi kumiminika kwa wingi katika kijiji hicho, ili kumshuhudia kondoo huyo wa ajabu aliyezaliwa akiwa na maandishi hayo ya Korani.

  Kondoo huyo aliyezaliwa Julai 6 amekuwa kivutio kikubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu, ambapo hadi sasa watu kutoka mikoa ya Dar es Saalam, Tanga na Arusha wamefika kushuhudia maajabu hayo.

  Akizungumza na HABARILEO, Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, alikiri kumshuhudia kondoo huyo na kueleza kuwa maandishi yanayosomeka ubavuni mwa kondoo huyo ni sahihi kama yanavyosomeka katika Kitabu cha Koran.

  Alisema maandishi hayo ya Kiarabu ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili ni Yasini, moja ya aya muhimu katika Koran pia ni moyo wa Kitabu hicho.

  “Aya hii ni moyo wa Kitabu Kitakatifu cha Koran, kinaelezea mambo mengi makubwa hususani nyakati za mwisho … inaonesha ishara kuwa hizi ni siku za mwisho za kiyama,” alisema Shehe Mallya.

  Alisema aya ya maandishi hayo katika Koran ni moja ya sura zinazoeleza mambo mazito, pamoja na kueleza kuwa Kitabu hicho kinazungumzia siku za mwisho za kiyama, hivyo kila mtu atengeneze maisha yake.

  Aliongeza kuwa hiyo ni ishara kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu, kwa sababu Kitabu Kitakatifu cha Koran kilishushwa Mwezi wa Ramadhan, hivyo ishara hii katika kipindi cha Mfungo Mtukufu wa Ramadhani ni kubwa.

  Pia Shehe Mallya aliongeza kuwa neno Yasini ni jina lingine la Mtume Muhammad (SAW) alilopewa na Mwenyezi Mungu, na kueleza kuwa hiyo ni miujiza na bahati kwa dini hiyo.

  “Haya maandishi katika aya ya Kitabu cha Koran yamejikita zaidi kuonesha hizi ni siku za mwisho za kihama, hivyo wakati huo midomo haitaongea tena ila mikono itasema na miguu itashuhudia, hivyo Mungu akipenda jambo lake liwe linakuwa,” alisema Shehe Mallya.

  Katika hatua nyingine, Shehe huyo alisema walihitaji kumnunua kondoo huyo kwa lengo la kuwa mfugo wa Msikiti, lakini imeshindikana baada ya mmiliki kukataa kumwuza.

  Akizungumza na HABARILEO nyumbani kwake, mmiliki wa kondoo huyo, Grace, alieleza historia ya kondoo aliyemzaa na kusema alimpata kama mahari kwa binti yake wa pili, na ndama huyo ni uzao wa pili.

  Grace alisema katika familia yake yenye jumla ya watoto watano, watatu ni Wakristo na wawili ni Waislamu ambao waliolewa na kubadili dini, na hapo awali mumewe ambaye ni marehemu alikuwa Mwislamu na kubadili dini na kuwa Mkristo.

  Alieleza sababu za kukataa kumwuza kondoo huyo, akisema bado familia haijajua nini maana ya tukio hilo na kwamba inachukulia kitendo hicho kama baraka kwa familia.

  Alisema hadi sasa watu wawili wamejitokeza wakitaka kumnunua kwa kiasi kinachofikia Sh milioni 10, lakini bado amesisitiza kutomwuza.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  wa GALA matata sana

  sasa mpaka kondoo naye wanataka ku monopolize!
   
 3. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Mi nawasihi waislamu wenzangu.... tuangalie mambo mengine!! huyu kondoo sio mungu!! .. kama ni mawaidha yameshafika!...

  waislam tusiende mbali kumsahau mungu na kuanza kumuabudu huyu kondoo, maana nijuavyo kuna maustadhi wengine wataanza kuomba dua kupitia kondoo na mwishowe watakuwa wamefanya shirk moja kubwa sana..

  kama vipi wamnunue toka kwa wenyeji (wamiliki) wa huyo kondoo, akikua achinjwe.. nyama wapewe yatima! "case solved"
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hii mambo ya koolani kuwa Kondoo ni maskhara na kufru tupu.
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  HabariLeo halina tofauti na Al Nuur na pua Huda!
   
 6. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Not all the time we are supposed to comment -vely about others faiths. Hebu kua ebo!
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Na huu ni uchuro mwingine unaofuata baada ya lile la tiba ya vikombe,...imani kwenye kondoo ni upuuzi na ujonga mwingine inaonyesha tusivyo na makini
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kufuru kuliko Mungu kuwa na mtoto au kuwa na marafiki (trinity) ?
   
 9. araway

  araway JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 498
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  wapi picha za kondoo mwenyewe ? mandishi yapo apande gani ya kondoo??mkiani,kichwani au ulimini?
   
 10. doup

  doup JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
Loading...