Kondomu za kike zageuzwa vipuri vya magari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kondomu za kike zageuzwa vipuri vya magari!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BornTown, Sep 18, 2010.

 1. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kondomu za kike zageuzwa vipuri vya magari Saturday, 18 September 2010 08:39 Editha Majura Source: Mwananchi

  BINADAMU ana akili nyingi; kila kitu chaweza kutumiwa kwa malengo tofauti na yalivyokusudiwa.
  Ndivyo ilivyo katika matumizi ya kondomu za kike, maarufu kama Lady Pepeta, ambazo zilikusudiwa kutumika kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, lakini sasa zinatumika kama vipuri vya magari makubwa ya mizigo na abiria, Mwananchi imebaini.
  WAKATI kampeni za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kwa kutumia kondomu zikiwa zimeshika kasi, imebainika kuwa mipira inayotumiwa na wanawake dhidi ya janga hilo, maarufu kama Lady Pepeta, inatumika kama vipuri vya magari makubwa ya mizigo na abiria.

  Uchunguzi wa gazeti hili umeona utundu zaidi wa binadamu baada ya kubaini kuwa kondomu hizo na nyingine aina ya Care, pia zinatumika kutengenezea urembo kwa ajili ya kinamama.
  Kondomu hizo za kike ziliongezwa kwenye vita dhidi ya Ukimwi kutokana na ugonjwa huo kushika kasi na kuendelea kudhoofisha nguvu kazi kubwa ya dunia, na hasa nchi maskini kama Tanzania.
  Takwimu za kisayansi zinaonyesha kuwa maambukizi ya ukimwi kwa wanawake ni makubwa ikilinganishwa na maambukizi hayo kwa wanaume.

  Kupitia kitabu cha viashiria vya kijinsia cha mwaka 2010, serikali imeeleza kuwa maambukizo ya Ukimwi kwa wanawake nchini ni asilimia 6.8 na wanaume asilimia 4.7.

  Lakini pamoja na kiwango hicho cha maambukizi, binadamu amegundua matumizi mengine ya silaha hizo dhidi ya Ukimwi, ugunduzi ambao kwa kiasi fulani unaweza kuongeza bei ya kondomu hizo kutokana na mahitaji kukua.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa baadhi ya mafundi wa magari makubwa jijini Dar es Salaam wamekuwa wakitumia mipira ya duara iliyopo mwanzoni na mwishoni mwa kondomu hizo kama vipuri vya kutengenezea njia za upepo za magari hayo pale zinapoharibika.

  Baadhi ya mafundi hao waliliambia gazeti hili kuwa mipira hiyo inatumika kama vipuri mbadala wa vile vinavyoingizwa kwenye kifaa kiitwacho air valve controller, kidhibiti cha hewa.
  Vipuri halisi vinavyotumika kwenye valve hizo huuzwa madukani kwa kati ya Sh80,000 na Sh400,000 kulingana na ukubwa na aina yake.

  “Huwezi kupata breki au kuwasha gari kubwa ikiwa njia ya upepo ina matatizo. Control valve ikivujisha upepo lazima inunuliwe mpya ambayo ni kati ya Sh80,000 na Sh400,000,” alieleza mmoja wa mafundi hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.

  “Hii mipira inasaidia sana kwa sababu ikitumiwa kuziba O-ring huzidi kubana kadri inavyopata joto.”
  Wakati mafundi hao wakitumia kondomu hizo kama vipuri vya magari, baadhi ya wafanyabiashara huchukua mipira hiyo na kutengeneza urembo hasa bangili ambazo baadaye huuzwa kwa mafungu kwa kati ya Sh200 na Sh500.

  Uchunguzi umebaini kuwa bangili hizo huuzwa kwa wingi maeneo ya Ubungo na soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
  “Nimezinunua sokoni Kariakoo, lakini zinapatikana kwa wingi zaidi Ubungo nyakati za jioni," alisema mkazi mmoja wa Dar es Salaam ambaye alikuwa amevaa bangili hizo.

  Meneja Mipango wa Shirika la Population Service International (PSI) nchini, Dk Alex Ngaiza aliiambia Mwananchi kuwa tangu usambazaji wa kondomu za kike aina ya Care uzinduliwe mwaka 1998, mahitaji yamekuwa yakiongezeka.
  “Kwa mwaka tunasambaza kondomu 576, lakini mwaka huu 2010 tutasambaza kondomu 720. Hii inamaanisha kuwa mahitaji yanaongezeka ingawa ni dhahiri kwamba uhamasishaji zaidi unahitajika,” Dk Ngaiza alieleza.

  Akizungumzia matumizi ya kondomu hizo kinyume na malengo, alisema “inawezekana yakawepo lakini ni vigumu kuthibitisha suala hilo".

  Alidokeza kusema: "Hata chroloquine ilitengenezwa ili kutibu ugonjwa wa malaria, badala yake wengine walizitumia kujiua. Hizo ni changamoto ambazo kwa ujumla tunahitaji kukabiliana nazo.”
  Utafiti wa matumizi ya kondomu za kike uliofanywa na PSI mwaka jana katika mikoa mikoa mitatu ya Lindi, Dar es Salaam na Arusha ulibaini kuwepo na utengeneza vifaa vya urembo hasa mkoani Lindi kwa kutumia silaha hizo za kuvaana na Ukimwi.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa mwanzoni mwa Septemba, kikwazo cha matumizi ya kondomu ni umma kutoelewa jinsi ya kuzivaa.

  “Mijadala kuhusu kondomu za kike imejikita zaidi kuhusu nafasi yake katika kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. Lakini suala la kwamba kondomu hizo zinapatikana wapi na jinsi mtu anavyoweza kuzitumia halipewi nafasi kabisa,” inasema taarifa hiyo ya utafiti wa PSI.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya watumiaji wanaziona kondomu za kike kama kitu kinachowadhalilisha na kuwakerehesha tofauti na kondomu za kiume ambazo uvaaji wake ni rahisi.

  Mkuu wa Kitengo cha taarifa, elimu na ushauri (IEC), cha Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk Bennet Fimbo alisema kwa sasa haujafanyika utafiti wa kiwango cha uelewa wa jamii kuhusu matumizi ya kondomu za kike ingawa suala hilo litazingatiwa katika utafiti unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.

  Afisa mawasiliano wa kampuni ya T-Marc Ltd ambayo ni msambazaji na mhamasishaji wa matumizi ya kondomu aina ya Lady Pepeta, Daniel Sempeho alisema anawasiliana na vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo ili kupata taarifa sahihi kuhusu hali ya bidhaa hiyo sokoni.

  "Tukimaliza kufanya mawasiliano hayo na kujua nini kinafanyika, tutaijulisha jamii," alisema.
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Yep! RECYCLING au REUSING? Hazina soko, kuliko kuziacha ziharibike ni sawa tu kuzitumia kwa matumizi mengine! Mbona bidhaa nyingi tu zina matumizi mbadala!
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Bila shaka watengenezaji watafurahi na kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji yote - ya akina mama na ya magari.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  He!...kama hiyo condom inafanya kazi sawa na kifaa cha thamani ya 80,000 hadi 400,000/=, basi watengenezaji watapandisha bei fasta!

  Wabongo bana,...how could one even start imagining of such miserable innovation!..huh!
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Editha Majura

  BINADAMU ana akili nyingi; kila kitu chaweza kutumiwa kwa malengo tofauti na yalivyokusudiwa.
  Ndivyo ilivyo katika matumizi ya kondomu za kike, maarufu kama Lady Pepeta, ambazo zilikusudiwa kutumika kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, lakini sasa zinatumika kama vipuri vya magari makubwa ya mizigo na abiria, Mwananchi imebaini.
  WAKATI kampeni za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kwa kutumia kondomu zikiwa zimeshika kasi, imebainika kuwa mipira inayotumiwa na wanawake dhidi ya janga hilo, maarufu kama Lady Pepeta, inatumika kama vipuri vya magari makubwa ya mizigo na abiria.

  Uchunguzi wa gazeti hili umeona utundu zaidi wa binadamu baada ya kubaini kuwa kondomu hizo na nyingine aina ya Care, pia zinatumika kutengenezea urembo kwa ajili ya kinamama.
  Kondomu hizo za kike ziliongezwa kwenye vita dhidi ya Ukimwi kutokana na ugonjwa huo kushika kasi na kuendelea kudhoofisha nguvu kazi kubwa ya dunia, na hasa nchi maskini kama Tanzania.
  Takwimu za kisayansi zinaonyesha kuwa maambukizi ya ukimwi kwa wanawake ni makubwa ikilinganishwa na maambukizi hayo kwa wanaume.

  Kupitia kitabu cha viashiria vya kijinsia cha mwaka 2010, serikali imeeleza kuwa maambukizo ya Ukimwi kwa wanawake nchini ni asilimia 6.8 na wanaume asilimia 4.7.

  Lakini pamoja na kiwango hicho cha maambukizi, binadamu amegundua matumizi mengine ya silaha hizo dhidi ya Ukimwi, ugunduzi ambao kwa kiasi fulani unaweza kuongeza bei ya kondomu hizo kutokana na mahitaji kukua.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa baadhi ya mafundi wa magari makubwa jijini Dar es Salaam wamekuwa wakitumia mipira ya duara iliyopo mwanzoni na mwishoni mwa kondomu hizo kama vipuri vya kutengenezea njia za upepo za magari hayo pale zinapoharibika.

  Baadhi ya mafundi hao waliliambia gazeti hili kuwa mipira hiyo inatumika kama vipuri mbadala wa vile vinavyoingizwa kwenye kifaa kiitwacho air valve controller, kidhibiti cha hewa.
  Vipuri halisi vinavyotumika kwenye valve hizo huuzwa madukani kwa kati ya Sh80,000 na Sh400,000 kulingana na ukubwa na aina yake.

  “Huwezi kupata breki au kuwasha gari kubwa ikiwa njia ya upepo ina matatizo. Control valve ikivujisha upepo lazima inunuliwe mpya ambayo ni kati ya Sh80,000 na Sh400,000,” alieleza mmoja wa mafundi hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini.

  “Hii mipira inasaidia sana kwa sababu ikitumiwa kuziba O-ring huzidi kubana kadri inavyopata joto.”
  Wakati mafundi hao wakitumia kondomu hizo kama vipuri vya magari, baadhi ya wafanyabiashara huchukua mipira hiyo na kutengeneza urembo hasa bangili ambazo baadaye huuzwa kwa mafungu kwa kati ya Sh200 na Sh500.

  Uchunguzi umebaini kuwa bangili hizo huuzwa kwa wingi maeneo ya Ubungo na soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
  “Nimezinunua sokoni Kariakoo, lakini zinapatikana kwa wingi zaidi Ubungo nyakati za jioni," alisema mkazi mmoja wa Dar es Salaam ambaye alikuwa amevaa bangili hizo.

  Meneja Mipango wa Shirika la Population Service International (PSI) nchini, Dk Alex Ngaiza aliiambia Mwananchi kuwa tangu usambazaji wa kondomu za kike aina ya Care uzinduliwe mwaka 1998, mahitaji yamekuwa yakiongezeka.
  “Kwa mwaka tunasambaza kondomu 576, lakini mwaka huu 2010 tutasambaza kondomu 720. Hii inamaanisha kuwa mahitaji yanaongezeka ingawa ni dhahiri kwamba uhamasishaji zaidi unahitajika,” Dk Ngaiza alieleza.

  Akizungumzia matumizi ya kondomu hizo kinyume na malengo, alisema “inawezekana yakawepo lakini ni vigumu kuthibitisha suala hilo".

  Alidokeza kusema: "Hata chroloquine ilitengenezwa ili kutibu ugonjwa wa malaria, badala yake wengine walizitumia kujiua. Hizo ni changamoto ambazo kwa ujumla tunahitaji kukabiliana nazo.”
  Utafiti wa matumizi ya kondomu za kike uliofanywa na PSI mwaka jana katika mikoa mikoa mitatu ya Lindi, Dar es Salaam na Arusha ulibaini kuwepo na utengeneza vifaa vya urembo hasa mkoani Lindi kwa kutumia silaha hizo za kuvaana na Ukimwi.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa mwanzoni mwa Septemba, kikwazo cha matumizi ya kondomu ni umma kutoelewa jinsi ya kuzivaa.

  “Mijadala kuhusu kondomu za kike imejikita zaidi kuhusu nafasi yake katika kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. Lakini suala la kwamba kondomu hizo zinapatikana wapi na jinsi mtu anavyoweza kuzitumia halipewi nafasi kabisa,” inasema taarifa hiyo ya utafiti wa PSI.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baadhi ya watumiaji wanaziona kondomu za kike kama kitu kinachowadhalilisha na kuwakerehesha tofauti na kondomu za kiume ambazo uvaaji wake ni rahisi.

  Mkuu wa Kitengo cha taarifa, elimu na ushauri (IEC), cha Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Dk Bennet Fimbo alisema kwa sasa haujafanyika utafiti wa kiwango cha uelewa wa jamii kuhusu matumizi ya kondomu za kike ingawa suala hilo litazingatiwa katika utafiti unaotarajiwa kufanyika siku chache zijazo.

  Afisa mawasiliano wa kampuni ya T-Marc Ltd ambayo ni msambazaji na mhamasishaji wa matumizi ya kondomu aina ya Lady Pepeta, Daniel Sempeho alisema anawasiliana na vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo ili kupata taarifa sahihi kuhusu hali ya bidhaa hiyo sokoni.

  "Tukimaliza kufanya mawasiliano hayo na kujua nini kinafanyika, tutaijulisha jamii," alisema.

  Chanzo: Kondomu za kike zageuzwa vipuri vya magari
   
Loading...