Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 202
- 1,588
Baada ya "sintofahamu" ya muda mrefu hatimaye leo Moshi Vijijini imempata mgombea atakayepeperusha bendera ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla. Ni ndugu Anthony Kalist Komu mkurugenzi wa fedha na utawala CHADEMA taifa.
Baada ya kikao cha leo mjini Moshi, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe hatimaye makubaliano yamefikiwa kuwa Anthony Komu awe mgombea Moshi vijijini. Mgombea aliyeshinda awali na baadae kukatiwa rufaa Mhe.Lucy Owenya nae amekubaliana na maamuzi hayo. Lucy pia ameshinda ubunge wa viti maalumu Moshi mjini.
Nitumie fursa hii kwanza kumpongeza Komu kwa kupata nafasi hiyo, kumpongeza Lucy Owenya, lakini pia kuwapongeza wagombea wote 9 tuliokuwa tukiwania kiti hicho kupitia CHADEMA.
Zaidi sana niwakuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki, kwa kuniunga mkono tangu nilipotangaza nia ya kugombea Moshi vijijini. Mungu awabariki kwa namna mlivyoguswa na kujitolea kwa ushauri, mawazo na wengine fedha. Siwezi kuwalipa lakini nawaombea baraka.
Nishukuru pia wanachama na wapenzi wa CHADEMA Moshi Vijijini kwa namna walivyokua wavumilivu na watulivu baada ya chaguzi zote mbili kuingia dosari (ule wa kwanza na wa marudio baada ya kushinda rufaa). Sasa tofauti zetu zimekwisha na mgombea wetu rasmi ni Anthony Komu. Tumuunge mkono aweze kushinda.
Binafsi bado ni kijana na nina safari ndefu kisiasa. Mungu ameona mwaka huu bado hadi baadae. Kwa hiyo nitaendelea kukipigania chama kwa nguvu zaidi kama ambavyo nimekuwa nikifanya siku zote ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani na tunapata ukombozi wa pili kama taifa.
Hii ni nafasi yangu ya kuendelea kupigania zaidi maslahi ya watanzania kupitia siasa. Nitashiriki kampeni za ubunge Moshi Vijijini kuhakikisha Komu anashinda. Lakini nitashiriki pia kampeni katika majimbo mengine kuwaunga mkono wagombea wa UKAWA. Hii ni nafasi pia ya kujijenga na kujiimarisha zaidi kiuchumi, na kijamii ikiwa ni pamoja na kufikiria kuanzisha familia na kuimarisha NGO yangu.
Niwaombe wanachama, wapenzi, mashabiki, na wafuasi wote wa CHADEMA Moshi Vijijiini tuungane kwa pamoja, tusahau yaliyopita, tumuunge mkono Anthony Kalist Komu aweze kushinda nafasi ya Ubunge Moshi vijijini.
Mungu ibariki CHADEMA, Mungu ibariki Moshi vijijini. #TWENDE_NA_KOMU_2015