FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
KOMBORA KIOTANI
(VITA KUU)-1
Book 2
Boniface Birage
Tone la umande lilitua kwenye paji la uso.Mwili ulikwisha shtuka dhidi ya baridi kali iliyokuwa ikifyonzwa kwenye ngozi yake na kuzama ndani kutikisa hali joto ya mwili wake.Baridi ilikuja na yeye kuipokea kisha akumbatie maumivu yake.Wazo la kishujaa kwenye maumivu ndo hapo ushindi!Aliwaza.Matone kadhaa yalizidi kutua kwenye mwili wake.Harufu ya pori kijani kibichi cha uoto wa ardhi ya Kiota ilimjia katika pua zake.Ardhi ya taifa lake.Pengine angekuwa katika pori hili akitalii au kulinda kama angekuwa kwenye kitengo chake.Lakini sasa yupo hapa kwenye msitu mnene hata kama angepiga kelele wasingemsikia hata kidogo.Alikuwa katika upweke wa baridi hii na kutafunwa na unene wa msitu huu.
Alikuwa amepigishwa magoti huku mikono ikifungwa kwa nyuma kwa kamba nene kama ile aliyonyongewa Saddam Hussein.Hatua zilisikika kwa nyuma bila shaka watesi wake walikuwa tayari kwa hatua nyingine.Moyo ulimuenda mbio akijua mwisho wake umefika.Tayari alikuwa na jeraha kwenye paji la uso.Ni teke alipigwa zito.Mwili ulisisimka muda hata muda na ukali wa baridi ulikuwa kama ganzi kwa majeraha yake.Msitu ulikuwa mnene na tayari kwa kumeza sauti itakayosikika.Alijua kwanini yupo hapa!Wengi waliofika hapa hawakubahatika kutoka salama.Kama ulifikishwa hapa kwenye msitu huu bahati ilikuwa kama mshumaa kwenye upepo mkali.
MSITU WA FUVU.Uliitwa hivyo na wengi waliojua siri za msitu huo.Wengi waliojaribu kutengeneza makazi maeneo hayo walizuiwa na serikali nakuhakikisha hawapati mwanya wowote wakuwawezesha kugusa sakafu ya msitu huu!Kulikuwa na mitazamo pamoja na hadithi za kufikirika kwamba msitu huo ulikuwa na mambo ya kutisha.Wengi waliokwenda walishindwa kusonga ikisemekana walikutana na mabaki ya mifupa ya binadamu au miiili ilioachwa kuoza na hakuna aliyepata ripoti miiili hiyo ilifikaje maeneo hayo.Hata waliotoa ripoti kwenye vyombo husika hakuna hakuna hatua zilizochukuliwa nap engine mtoaji ripoti angepatikana siku ya pili kaokotwa maiti au kupotea kabisa!Wachache walijua waraka wa MSITU WA FUVU!Hao wajuaji walikuwa watekelezaji wa kazi maalum za msitu huu!
Shunie kwa tasnia yake ya ushushushu alijua endapo mwenye pumzi akipelekwa pale ni nadra sana kutoka akiwa hai.Mwili usingepatikana na bila shaka ripoti yake ingekuwa AMEPOTEA,HAJAPATIKANA!Kelele zingepigwa lakini wapi hakuna ambaye angejitokeza.Hata kupelekwa katika msitu ni wachache walijua!
Kamba zilizofungwa mwiilini kuna wakati alihisi ni misumari imepigiliwa kwake!Lakini leo ni leo!Hakutaka mwisho wake uwe hapa!Sehemu yenye sifa za kuchukua maisha ya watu haikuwa sahihi kwake wala haikumtosha kumshusha ardhini.Pengine nduguze wasingejua alifia wapi?Mwili ungeachwa kwa vijidudu kuushambulia hadi kuoza nakuwa mbolea!Shunie alihuzunika sana na hata ule ujasiri aliokuwa nao kuna wakati ulimpwaya kabisa akaona hana thamani tena ya kuishi!Wasiwasi ulimpapasa moyo nafsi ikasisimka!
Vishindo vilisikika tena vya hatua za ujio wa watu.Alijua muda umefika!Watu hao walisogea mbele yake akafanikiwa kuziona sura zao zenye uzitoo!
Alivuta pumzi ndefu nakuzitoa kwa pupa hali iliyoonesha kiwango cha wasiwasi kilishindana na ujasiri huku mwili ukimtetemeka bila mpangilio.Siku ya utakaso wa roho kabla ya kuonja umauti.Upepo ulivuma kwenye kanianga na presha ilikuwa yakupanda muda hata muda.
“Unajidai wewe ndo mzalendo sana?”ilikuwa sauti ya bwana aliyekuwa nyuma yake.
Alizishika nywele zake nakuzivuta kana kwamba anataka kuzichana.
“Nimesoma faili lako Shunie ni ofisa mzuri kwa taifa lakini inatakiwa tujue utiifu wako uko wapi?You know too much…sio busara kukuua!”alisema mtu huyo mwenye sauti kavu aliyepanda hewani.Alikuwa amevalia nguo nyeusi pamoja na koti la kujikinga na mvua.
“Uzalendo wangu ni kwa taifa na utiifu ni kwa rais Kilua.”alijitutumua kusema hayo yalikuwa maneno yake afisa huyu wa serikali.
“Wengi walisema kama wewe lakini wakaishia kuzimika.Kilua tumemuondoa madarakani tunaikomboa nchi hii lakini tunahitaji jambo toka kwako.”
Shunie alielewa saikolojia ya mtesi wake alikuwa akihitaji ushirikiano wake.Hilo lilitosha kumuweka kwenye utayari kwamba hawa wanataka jambo toka kwake na wakisha lipata kuna uwezekano wakaendelea kumtumia au kumfutilia mbali ikiwa tayari Kilua kasha tikiswa bado nyumba inateketea na kila mu anatafuta kuinusuru.Wengi wanaendelea kukamatwa nakutwa nguvuni wakisubiri hatma yao.
Ni kawaida wangefutilia mbali wote waliokaribu na Kilua wakianza na yeye kama moja ya maofisa watiifu waliokuwa wakifanya kazi kwa Kilua.
“Sina cha kuwasaidia.”alisema Shunie kwa kiburi.
“Hahaha!”alicheka kidogo.
“Unajua upo wapi?”
“Msitu wa fuvu.”
“Vyema.”alijibu kisha akajikohoza,”Hakuna anayetoka salama hapa.Kilua na watu wake mna mambo mengi sana na mlikuwa mpo mbioni kuchunguza mambo yasiyo takiwa yafanyike.”
Shunie alitema mate kwa dharau kuonesha huyu jamaa hana kitu chochote.
“Nahitaji ushirikiano wako nataka kujua ni nani aliwapa faili nambari 13:14.”aliuliza huyu bwana kisha akazivuta tena nywele za Shunie karibu kuzichana.Mateso yalishakuwa mengi sana.
“Utaniambia au la?”
Shunie alihisi ngozi ya kichwa ikitaka kunyofoka!Alijikaza.
Yule bwana alimuachia kisha akarudi nyuma hatua kadhaa akawa kama anaangalia chini kuna nini alisogea tena kadhaa akaona vijidudu vikiwa katika msafara wa kijeshi.Alitabasamu!Ulikuwa msafara mzuri tena ungemfaa kwa kazi yake maalum.
Alimkokota Shunie nakumleta hadi kwenye eneo lile lililo na majeshi ya siafu.
“Utaongea tu!”alisema bwana Yule.Ilikuwa ni kiasi cha nguvu ndogo alizotumia ukilinganisha na kiwango cha uzito wa Shunie.Alimuangusha kwenye msafara wa siafu wale.Alipojaribu kufurukuta alishikwa mikono nakuhakikisha analala juu ya siafu ambao walihisi hatari nakuanza kuupanda mwili wa Shunie.Zilikuwa dakika chache wale siafu wakaanza kuushambulia mwili wa Shunie kwa kasi.Mfadhaiko wa maumivu ulikuwa wa mateso ya hali ya juu alikereka sana nakuhisi mateso ya mwili na saikolojia.Kufungwa kwa mikono nakushikwa miguu kulimfanya ashindwe kujitetea hali iliyoleta maumivu makali sana.Alibaki akipiga kelele ya kuuumia!
“Sema ni nani?”ilikuja sauti nzito ikiuliza.
“Mimi ni afisa usalama!...Nilifunzwa kuhimili mateso!”alisema Shunie huku akikumbuka siku zake akiwa chuoni akifunzwa kustahamili mateso na mwili kuwa na ukomavu wa hali ya juu!Leo ilikuwa siku yake!
“Utasema maana wewe ni miongoni mwa wachache mliojua uwepo wa siri ile>”
“Sijuiii!”
“I want names!”aliuliza bwana Yule kwa hasira.
Kwa hali kama hii lazima Shunie ategemee mateso pamoja na vitisho vya haja!Mateso huwa tofauti na hutegemea na kila mmoja anaweza kuvumilia kiasi gani mateso haya.Alichowaza ni kutoka katika mikono hii nakuhakikisha anawalipiza visasi vya hakutosha.
“Noo!”alisema.Pengine awaaminishe anajua kitu waendeelee kumtesa?Alijiuliza.Kule kuteswa hakukupendeza kabisa kulimfadhaisha sana!
“Tunajua una mafunzo ya hali ya juu.Hilo halina ubishi lakini inategemea ni kiasi gani cha maumivu mwili wako unaweza kuhimili.Zaidi yanakuja!”Alisema bwana Yule kisha akazidi kumbana miguu akimzuia asifurukute kuwakwepa siafu.Dalili za kuuawa kwa siku ile zilionekana kama kuishiwa nguvu!Alimwinua huku akimshika kwa umakini akihakikisha nay eye hapatwi na siafu wale.
Alimkokota hadi kwenye uwazi kidogo.Kulikuwa na vijana wengine waliokuwa wakivuta bangi asubuhi ile.Moshi ilifuka kwenye misokoto yao.UUngewaona walitosha kukuogopesha.Uzito wa msitu wa fuvu ulitosha kumuogopesha hata mwendawazimu.
“Tumpe teso bembea.”alisema Yule mtu aliyemshikilia Shunie.
Walimfungua kamba zile.Shunie alijua kinachofuata kujikuna aondoe wale siafu mwilini lakini waliwahi =kuishika mikono yake kisha walileta kipande cha mbao ya mviringo waliipitisha juu ya kifua chake na mikono yake ikapita juuu ya mbao akawa ameibana mbao mwilini kisha wakamfunga kamba kuizunguka mbao.
Mwili ulikuwa hoi!Ile mbao ilishikwa huku na huku wakaitundika kwenye nguzo mbili walizokuwa wameandaa ni kama walitundika nyama mikono yake ilianza kupata maumivu makali sana!Ile mbao iliyopita kifuani kutenganisha mikono ndo iliyokuwa mateso yake wakawa waanamsuka mbele nakumrudisha nyuma!Maumivu yalikuwa makali sana!
“Aaaah!”ukasikika ukelele mkubwa kama mtu amechomwa mkuki wa tumbo!Msitu ulimeza sauti ya ukulele ule!Yalionekana mafuvu kadhaa kwenye eneo lile yakiwa chini huku harufu kali ya miili kuoza ikizizima eneo lote!Shunie alikuwa katika wakati mgumu sana kuliko zote alizowahi kukutana nazo!
***
Maili kadhaa toka fukwe za Kiota kulikuwa na nyambizi ya kijeshi iliyoitwa KIOTA MAN OF WAR KMW.Wanajeshi waliendelea na shughuli zao katika manowari hiyo iliyokuwa na uwezo wa kubeba silaha kadhaa za maangamizi na ilikuwa tayari kwa vita muda wowote.Siku kadhaa walipokea amri kutoka kwa amiri jeshi mkuu wao kuwa tayari hasa ukizingatia mzozo uliopo kati ya mataifa mawili Kiota na Savannna Land.Viwango vya usalama vilikuwa vikipandishwa na utayari wao kuingia vitani ulikuwa upo sawa.
Kaptein Sadoki alikuwa msimamizi wa manowari hii kamanda mkuu wa kutoa amri katika meli hii.Alikuwa na kikosi cha kutosha chenye weledi yeye alipenda kuwaita malaika wa bahari kwa jinsi vijana wake walivyojitoa na kuwa na uzalendo wakulitumikia taifa lake.Kundi lake lilikuwa maalum na alijivunia kuwa nalo.Alikuwa akizunguka katika manowari alisogelea hadi kilipo kituo cha mawasiliano kuona kama kuna lolote.Mwanajeshi aliyekuwepo kitengo hicho alikuwa makini akiangalia kioo cha tarakilishi kikiwa na program maalum kwaajili ya mawasiliano.
Muonekano wa program ile kwenye kioo ulikuwa na nakshi mbalimbali zilizochakata taarifa ambazo mhusika wa kituo alitakiwa kuzitambua nakuzitolea maelezo.Manowari hii ilikuwa na rada maalum ya kijeshi kwaajili ya kujilinda.Wakiwa katika uangalizi ghafla kioo cha tarakilishi katika ile program anayotumia kuna taa iliwaka kwenye moja ya mistari ya kutumia ishara(signal)Iliwaka kwa mwanga wa kijani halafu ikafuatia aina Fulani za tarakimu.
Mwanajeshi kwenye kituo chake akashtuka!Macho yote yakawa kwenye kioo cha tarakilishi.
“Distress call code green valley!”alisema mwanajeshi Yule.
Kapteni Sadoki aliona jambo lile.
“Kuna tatizo…”
“Signal tumepokea hivi punde.”
“Ok nataka tuwe tayari signal kama hizi jumbe za kuomba msaada ni mtu mmoja tu anaweza kutumia chaneli hii kutuma ishara ya kuomba msaada na huyu ni rais mwenyewe katuma distress call!”
“Kwanini rais atume distress call wakati kama huu?”walijuliza wote bila kupata majibu.
“Ikitokea hivi ina maana ni sisi pekee tumeweza kupokea distress call hii vyombo vingine havijapata ujumbe huu.”alisema kaptein Sadoki akizidi kutafakari hatua ya kuchukua.
”Embu piga simu ikulu nataka kuzungumza na rais mwenyewe.”
“Kaptein lakini kama distress call ni ya rais ina maana usalama wake upo hatarini itakuwa vyema kweli kupiga simu ikulu?”
“Haijawahi kutokea hata siku moja chaneli hii kutumika na distresss call kutumwa na rais aliyeko madarakani.Hii ni mara ya kwanza na ina maana imani kwa majeshi yetu ipo hatarini.”
“Lakini imetokea.”
“Hebu fungua mawasiliano ya meli nzima.”alisema kaptein.Kisha afisa wa mawasiliano akafungua mawasiliano kupita ndani ya manowari yote kupitia kipaza sauti.
“Attention all units of KMW SHIP Ni kaptein Sadoki.”sauti ilipita kila pembe ya manowari ile.