vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,373
- 2,513
Ni kama vile timu kubwa zinawekewa vipaumbele kwa kila namna zipate kufuzu hatua zinazofuata. Mechi ya Senegal dhidi ya Uingereza, kabla hata Uingereza kupata goli kulikuwa na tukio la wazi la mchezaji wa Senegal kuchezewa foul ndani ya 18 lakini mwamuzi na watu wa V.A.R wakamezea. Jana pia waamuzi wakaiharibu mechi ya Brazil dhidi ya Korea kusini kwa kutoa penati ya uonevu kabisa.
Korea wana roho ngumu sana ya kupambana, pamoja na kufungwa lile goli moja ni wazi kabisa lilionekana kuwa uwezo wa kuchomoa na kufanya comeback. Hivyo Brazil, wakabidi wabebwe ili kuidhoofisha kabisa Korea.
Ile haikuwa penati kabisa kwasababu mchezaji wa Korea ndiye aliyekuwa anaumiliki mpira kisha lengo lake ilikuwa kuubutua mpira lakini mchezaji wa Brazil kamtokea kwa nyuma. Jambo ambalo mchezaji wa Korea hakumuona.
Korea hao hao walichezewa faulo ndani ya 18 kwa kuzibiwa njia lakini hakuna cha V.A.R kucheck wala nini. Wanatuharibia radha ya mchezo japo wao lengo lao lipo kibiashara.