Kombe la Cecafa Senior Challenge 2009

ni kweli zanzibar imeitoa zambia kwa mikwaju ya penati, baada ya golikipa wa zenji kuokoa mchomo mmoja wa penati

The truth golikipa ameokoa michomo miliwi ya penati.(Mambo live ndani ya KBC)Vijana have done as proud.Baada ya Kenya kupoteza moja bila kwa Uganda ni ZNZversus UG nusu fainali.Sjui reli ipo salama kibera.Ha ha ha
 
Zanzibar Yaibanjua Zambia 4-3, Yatinga Nusu Fainali

Timu ya soka ya Zanzibar imefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe la Chalenji linaloendelea nchini Kenya baada ya kuitupa nje ya mashindano timu ya taifa ya Zambia kwa kuilaza kwa magoli 4-3. Timu ya soka ya Zanzibar imewatupa Zambia nje ya mashindano ya kombe la Chalenji kwa kuifunga magoli 4-3 katika maguu 12 ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kufungana kwenye dakika 90 za mchezo huo uliochezwa jioni hii.

Hadi dakika 90 zinaisha hakuna timu iliyofanikiwa kuliona lango la mwenzake na kupelekea mechi hiyo iamuliwe kwa penalti.

Alikuwa ni golikipa wa akiba wa Zanzibar Mohamed Khamis aliyepeleka chereko kwenye visiwa vya Zanzibar kwa kuokoa penalti mbili za Zambia.

Akiongea baada ya kipigo hicho, kocha wa Zambia alieleza kusikitishwa na kutolewa kwa kikosi chake ambacho kitashiriki kombe la mataifa ya Afrika mwezi ujao nchini Angola.

Naye kocha wa Zanzibar, Mmoroko Hemed Abdelatif alikipongeza kikosi chake kwa uwezo mkubwa waliouonyesha kwenye mechi hiyo.

"Nawapongeza wachezaji wangu kwa kuweza kuwadhibiti wachezaji wa Zambia na kuonyesha ubora wao, Zambia ni timu bora katika mashindano haya na tunajivunia tumecheza vizuri sana katika mechi dhidi yao", alisema kocha wa Zanzibar.

Katika mechi nyingine ya robo fainali, wenyeji Kenya walitupwa nje ya mashindano na mabingwa watetezi Uganda kwa kutandikwa 1-0.

Zanzibar sasa itapambana na Uganda siku ya alhamisi kwenye mechi ya nusu fainali kuwania nafasi ya kucheza fainali ya kombe hilo kubwa kwa nchi za Afrika Mashariki.

Source: www.Nifahamishe.com
 
hongereni sana wakuu na furaha yetu itatimia zaidi mkituletea kombe nyumbani iwe zawadi kwa yale yaliotokea ya kuweka hali safi ya kisiasa zanzibar iwe chachu ya kila mzanzibari kujituma kwa kuleta heshima ya zanzibar iliopotea
 
Kocha wa Zanzibar Heroes anaitwa "Hemed Morocco" na wala sio Mmoroco kwa maana ya raia wa Moroco kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyoeleza.
Wadau mnasemaje game inayofuata na Waganda,,,,kaaaazi kweli kweli
KILA LA KHERI KILI STAR,,,funga hao eritrea wakapigane vita.
 
Kocha wa Zanzibar Heroes anaitwa "Hemed Morocco" na wala sio Mmoroco kwa maana ya raia wa Moroco kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyoeleza.
Wadau mnasemaje game inayofuata na Waganda,,,,kaaaazi kweli kweli
KILA LA KHERI KILI STAR,,,funga hao eritrea wakapigane vita.
Na hii hapa chini imekaaje?

Zanzibar's coach Hemed Abdelatif of Morocco was understandably elated.
 
kwa kuwa Maximo ni kocha wa TANZANIA,endapo kili starz ikitolewa basi aende akaongeze nguvu kwenye benchi la Zanzibar(mapinduzi star)


Asilete Nuksi kwenye timu yetu. Hatutaki waalimu wa nidhamu sisi.

Tunataka soka tu.
 
Inaonekana kweli Zanzibar iliyoko chalenji wanapiga soka la uhakika..huwa nasikia tu lakini mpaka wameitoa Zambia timu yenye kiwango cha juu, napata picha jinsi vijana walivyo jipanga...kila la heri Zanzibar kombe libaki nyumbani.
 
kwa kuwa Maximo ni kocha wa TANZANIA,endapo kili starz ikitolewa basi aende akaongeze nguvu kwenye benchi la Zanzibar(mapinduzi star)

lini uliwahi kuona karume akisafiri shein anaenda kukaimu zanzibar?
hii ni tanganyika na zanzibar,
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=hdRBfLOPkUk[/ame]

Enjoy!
 
leo tukichapwa hata mie nitaona maximo sasa anaharibu
..Hakuna cha Maximo mazee, wachezaji wetu vilaza wale. Hata ungemleta Ferguson au Ancelloti wale mbona uwezo wao umefika mwisho? Hili Jambo hata marehemu Zacharia Kinanda "Sachi" alipokuwa akifundisha Taifa Stars aliwahi kusema!!! Ngoja Stars wajaribu lakini hata kama tukishinda ile timu bado sana, na usishangae Eritria wakituduwaza leo!!!
 
Labda tutaponea kwenye matuta kama ndugu zetu jana! Kwani bado dakika ngapi ngoma ilale?
Tuombe Mungu nasi tupopoe hayo matuta!
 
Back
Top Bottom