Kombe la Cecafa Senior Challenge 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kombe la Cecafa Senior Challenge 2009

Discussion in 'Sports' started by bnhai, Nov 28, 2009.

 1. b

  bnhai JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Chipolopolo beat Kenya

  The Chipolopolo boys this afternoon beat Kenya’s Harambee Stars in the opening match of the Orange Cecafa senior Challenge Cup at Moi Kasarani Stadium in Kenya.
  Zambia beat the hosts 2-0
  Former president Fredrick Chiluba and Kenya’ s current president Mwai Kibaki met the two teams before kick off.
  According to information received, Chiluba took time to encourage the Zambian team.
  Chiluba is on his way from Nigeria but his itinerary passes through Nairobi
   
 2. b

  bnhai JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kesho na sisi tunanyolewa, Uganda wako vizuri saana. nadhani Maximo safari imewadia
   
 3. Kilakshari

  Kilakshari JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kipigo iko ni dalili tooosha kwamba Kenya awalichukui kombe ili, and therefore Kilimanjaro Stars ni la kwao 2009! Kili Stars,kesho mkipiga mashuti ya mbali kama lile la Kigi Makasi, Misri; mtawafunga mengi sana hawa waganda, hawana kipa hao, wameninginiza shati golini!
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi nilitamani kweli tupangwe na Zambia tushindiliwe migoli ya adabu ili maximo ajiuzuru maana mbishi sana huyu kocha..
   
 5. Kilakshari

  Kilakshari JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nyie ni wakimbizi toka burundi nini? kwanini hamna uzalendo? yaani mko tayari taifa lishindwe ili ati kocha atimuliwe? ajabu sana!!!!
   
 6. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  kama kuna atakayekuwa na updates zozote tunaomba atujurishe wadau, timu ni yetu hata tukifungwa magoli 20 bado itabaki palepale kuwa ni timu ya taifa, so kilichobaki ni kuendelea na kile kilichoanzishwa na sio kukandia.
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  bado timu yetu inasusua kufuatia kipigo cha Timu timu chovu ya Uganda, mimi niulize Tatizo ni wachezaji ama kocha ?
  nasikia kocha kampanga Tegete muda mwingi, huku akimnyima nafasi Mussa hassani Mgosi, kweli huyu Bambuucha yupo serious?, nashangaa, sio kila mbrazil ni mwalimu, huu ni mkenge, ni madudu.
   
 8. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Uganda 1 Tanzania 0
   
 9. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Duuuh...tunashukuru mkuu Nurujamii
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sasa kitachachofuata hapo ni Mr. Marcio kujisifia jinsi alivyojitahidi na kafungwa goli moja tu!
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Stars ya Maximo ishafungwa 2-0
   
 12. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  duh, kazi kwelikweli
   
 13. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  game limeisha au bado linaendelea?
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  du 2:0????
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  natamani zanzibar watufunge piaa
   
 16. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Vipi, mechi imeisha au inaendelea...mawili! Heeeeee.......Zanzibar watufunge, sasa tutawafunga nani, labda Djibouti
   
 17. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WTF! Count me out. Masatu kakujibu vema hapo chini.

  Hapa masika tunakubaliana mia kwa mia. Mimi nasema kamnyima Kaseja nafasi kwa sababu alifurahia kufungwa kwa timu basi na anifungie na mimi pia kwani ninafuraha kupita kiasi timu yake imekiona kilichomtoa kanga manyoya
   
 18. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  huyu maximo si analindwa kapewa kazi sio kwa kuangalia matokeo jamaa yeye yupo yopo tu anakula maisha bongo kisa mbrazil.
   
 19. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  WAKATI timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes' jana ilianza kwa kishindo michuano ya Kombe la Chalenji kwa kuinyuka Burundi mabao 4-0, wenzao Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' walichapwa mabao 2-0 na Uganda ‘The Cranes'.


  Ndio kwanza safari ya mashindano hayo imeanza, lakini inaweza kutoa picha angalau ya wapi wawakilishi hao wa Tanzania mashindano hayo watafanya mwaka huu.


  Kombe la Chalenji mara ya mwisho kuchukuliwa na timu za Tanzania ilikuwa mwaka 1995, lakini tangu hapo limekuwa likija nchini pale mashindano hayo yanapofanyika hapa na timu za nje zimekuwa zikiondoka nalo zinavyotaka.


  Katika mchezo wa jana wa Stars na Uganda uliofanyika Uwanja wa Mumias mjini hapa, ambao ulitanguliwa na ule wa Zanzibar na Burundi kwenye uwanja huo huo, ulitawaliwa zaidi na Uganda hasa kipindi cha kwanza kabla ya Stars kuzinduka dakika za mwisho za kipindi cha pili.


  Uganda ilipata bao la kwanza dakika ya pili, mfungaji akiwa Kasule Ousen akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Daniel Wagaluka aliyefanyiwa madhambi na beki Kelvin Yondani.


  Wachezaji wa Uganda Steven Bengo anayechezea Yanga na Wagaluka anayechezea Azam zote za Dar es Salaam walikuwa hatari kwa beki za Kilimanjaro Stars zilizoonekana kupata tabu namna ya kuwakaba.


  Kwa nyakati tofauti waliingia kwenye eneo la hatari, lakini walipiga mashuti ambayo ama yalikuwa dhaifu na kudakwa na kipa Muharami Mohammed anayechezea Ferroviario ya Msumbiji au yalitoka nje ya lango.


  Kipa huyo, jana ulikuwa mchezo wake wa kwanza kuchezea timu ya Taifa, ambapo alionesha uwezo mkubwa, ingawa kuna wakati alikuwa akilaumiana na mabeki wake hasa Shadrack Nsajigwa, ambaye pia kwa nyakati tofauti alikuwa akizozana na beki mwenzake wa Stars Salum Sued ‘Kusi'.


  Stars inayonolewa na Mbrazili Marcio Maximo, kipindi cha kwanza ilifanya mashambulizi ya nguvu langoni mwa Uganda mara mbili, dakika ya 11 wakati shuti la Kigi Makasi lilipotoka nje na dakika ya 37 shuti hafifu la John Bocco lilipodakwa na kipa Hamza Muwonge.


  Muda mwingi katika kipindi hicho walikuwa wakicheza kati au kufanya kazi ya ziada kuhakikisha hawafungwi na kuonekana kana kwamba wanacheza nusu uwanja.


  Watanzania waliohudhuria mchezo huo waliingiwa na simanzi dakika ya 38 pale mwamuzi Michele Kasingua wa Rwanda alipomuonesha kadi nyekundu kiungo Juma Nyoso kutokana na kumchezea madhambi Wagaluka.


  Awali alioneshwa kadi ya njano kwa kosa pia la mchezo mbaya.


  Stars ilicharuka zaidi dakika za mwisho kipindi cha pili hasa baada ya kutolewa Shaaban Nditi, John Bocco na Kigi Makasi na kuingia Henry Joseph, Mrisho Ngasa na Jerry Tegete, lakini umaliziaji haukuwa mzuri.


  Bao la ushindi la Uganda lilifungwa dakika ya 88 na Serumaga Mike aliyepiga mpira wa adhabu na kutinga moja kwa moja wavuni.


  Baada ya mchezo huo, Maximo alisema hawezi kuwalaumu vijana wake na kwamba wameonesha kiwango kizuri na bado wana nafasi kubwa ya kufuzu robo fainali kwani wamempa matumaini makubwa.


  Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Cranes, Robert Williamson, alisema mechi ilikuwa ngumu kwao, lakini wanashukuru wameshinda na kwamba haogopi timu yoyote bali wanaziheshimu.


  Stars: Muharami Mohammed ‘Shilton', Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Salum Sued, Juma Nyoso, Danny Mrwanda, Shaaban Nditi, John Bocco, Kigi Makasi na Nurdin Bakari.


  Cranes: Hamza Muwonge, Simeon Masa, Geofrey Walusimbi, Joseph Owino, Andrew Mwesigwa, Kasule Ousen, Daniel Wagaluka, Tonny Maweje, Geofrey Massa, Peter Senyonjo na Steven Bengo.


  Katika mchezo wa Zanzibar, timu hiyo ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0. Zanzibar ilipata bao la kuongoza dakika ya 16 mfungaji akiwa Aggrey Morris kufuatia kona ya Nadir Haroub ‘Cannavaro', kabla ya dakika mbili baadaye Burundi kujifunga wenyewe pale beki Hakizimana Hassan alipotumbukiza mpira wavuni kwake.


  Beki huyo alikuwa katika harakati za kuokoa, lakini akajikuta mpira unamzidi nguvu kipa wake Vladmir Nyonkuru anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.


  Zanzibar Heroes inayonolewa na makocha wazalendo Ally Kiddy na Hemedi Moroko, ilipata bao la tatu dakika ya 25 mfungaji akiwa Selemani Kassim kufuatia krosi ya Ahmed Malik.


  Burundi walijaribu kubadilika kipindi cha pili kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini idadi kubwa ya mabao ya kipindi cha kwanza yalionekana kuwanyong'onyesha.


  Baada ya kosakosa za hapa na pale, Zanzibar ilipachika bao la nne dakika ya 67 baada ya Mbazumitima Henry kujifunga alipokuwa akijaribu kuokoa shuti la Selemani Kassim.


  Vumbi linatarajiwa kutimka kesho wakati Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes zitakapoumana katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute.


  Mara nyingi timu hizo zinapokutana matokeo huwa hayatabiriki, hivyo ni wazi kesho itakuwa vita ya aina yake uwanjani kutokana na baadhi ya wachezaji kujuana kwa
   
 20. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wakuu,
  Mi binafsi Maximo sujawahi kumuelewa hata kidogo... Mara yuko kwenye matangazo ya Serengeti, mara yuko kwenye maigizo ya akina Kanumba, huo muda wa kuandaa timu ya taifa anaupata saa ngapi?
  Huyu mzungu/burushi ni commedian tu hana lolote zaidi ya kuendekeza majungu..
  Muda wake sasa umefika.. full stop
   
Loading...