Komba hoi

Nikisema nchi haina viongozi na vyombo imara vya usalama wengine humu povu linawatoka kwa kutetea, hivi hawa tiss/uwt wao hawashangai mtu kwenda kufanyiwa checkup india wakati tuna hospitali za kutosha hapa? Inawezekanaje daktari mzalendo kutetewa na wabunge wanao cheki afya zao nje kwa gharama za serikali? Nawasihi ccm warekebishe mambo yao mapema maana wameanza kukosa uhalali wa kutawala kwa wananchi, kwa maana nyingine wananchi wako tayari kutawaliwa na chama chochote kuliko ccm kwaajili ya mambo kama haya.
 
MBUNGE wa Mbinga Magharibi Kepteni mstaafu, John Damian Komba anadaiwa kuwa yuko hoi nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu, Risasi Mchanganyiko lina mkoba uliojaa habari hii.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa Mhe. Komba aliondoka nchini wiki iliyopita.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Tanzania One Theatre (TOT) alikwenda nchini humo kwa ajili ya kucheki afya yake lakini amelazimika kufanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kushauriwa na madaktari.

“Awali alikuwa amekwenda kwa lengo la kuangalia afya yake lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi akagundulika kuwa ana matatizo ya nyonga, hivyo akatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana,” kilisema chanzo chetu kimojawapo.

Mmoja wa ndugu wa karibu na Komba, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile yeye siyo msemaji wa familia, alithibitisha hilo.

Huyu hapa anazungumza: “Ni kweli mzee amekwenda India. Tunashukuru Mungu ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri. Muhimu kwa Watanzania ni kumuombea dua apone haraka.”

Hii ni kuthibitisha kuwa tuna Serikali ya majuha na watu waliochoka kufikiri. Kwamba wamekataa kuboresha maslahi ya Madaktari sambamba na vitendea kazi kwa sababu maalumu!

Hapa Watanzania ndiyo wanatakiwa wazinduke na kujua ni serikali ya aina gani tuliyonayo. Kwamba wako tayari kukataa madai halali ya Madaktari.kuwafukuza na kuwaua ikiwezekana maana WAO WATAENDA ZAO NJE KUTIBIWA! Ndiyo maana hili swala la Madaktari limeonekana halina uzito wowote na Spika akaamua kulizuia lisijadiliwe Bungeni!

Hata hivyo nina swali la kizushi: Kwamba Captain Komba amefanyiwa operesheni ya Nyonga.Je,hii itakuwa imesababishwa na professional yake ya KUKATA VIUNO kwenye band yake ya TOT?
 
Si tunge hekeza tu huko tukajenga MUHIMBILI yetu?

jamani tusionee hili gamba.wananchi mnaochagua gamba kama hili kulipeleka mjengoni mtatibiwa na waganga wa kienyeji mpaka mshike adabu.sina dhambi juu ya uchaguzi wa mbunge wangu cause anachapa kazi.keep it up kaka yangu mbowe.
 
MBUNGE wa Mbinga Magharibi Kepteni mstaafu, John Damian Komba anadaiwa kuwa yuko hoi nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu, Risasi Mchanganyiko lina mkoba uliojaa habari hii.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vimeeleza kuwa Mhe. Komba aliondoka nchini wiki iliyopita.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa za Maonesho la Tanzania One Theatre (TOT) alikwenda nchini humo kwa ajili ya kucheki afya yake lakini amelazimika kufanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kushauriwa na madaktari.

?Awali alikuwa amekwenda kwa lengo la kuangalia afya yake lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi akagundulika kuwa ana matatizo ya nyonga, hivyo akatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka sana,? kilisema chanzo chetu kimojawapo.

Mmoja wa ndugu wa karibu na Komba, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini kwa vile yeye siyo msemaji wa familia, alithibitisha hilo.

Huyu hapa anazungumza: ?Ni kweli mzee amekwenda India. Tunashukuru Mungu ameshafanyiwa upasuaji na anaendelea vizuri. Muhimu kwa Watanzania ni kumuombea dua apone haraka.?

source Risasi mchanganyiko!!!
Kama ni kweli basi tunamwombea uponyaji wa haraka!
 
Halafu ndo uwagomee watu kama hawa! Ndo maana hawasikii. Tutazidi kuumia wanyonge tu!
 
Hii ndiyo sababu wabunge hawapiganii kuboreshwa kwa huduma za afya; check up India kwa nini isiwe Muhimbili?

Chama
Gongo la mboto DSM

Now u a talking!hata ww umeliona hilo......ss muhimbili atachekiwaje wakati hakuna vifaa?
 
Virusi vimeanza pa kutokea!! Amewatafuna na aliwatafuna sana waimba taarab wa TOT Taarab ambao wengine ni marehemu na wengine kazaa nao, mmoja wapo anaishi Kawe(nje ya ndoa) na wengine kawatelekeza Mwananyamala. In short you dont have to be a genius to understand this. Ila utasikia ni pressure, kisukari, cancer, etc. Ifike mahali tuwe wawazi!!!
 
Naomba kujua kama mh mbunge wa Rombo alipopata ajali serikali ilikuwa iko tayari kumpeleka India? au kwa sababu kutoka chama cha upinzani?
 
Mi nilijua kaenda kufanyiwa upasuaji ili asilale tena bungeni... anyway Get well soon sir ili uje ushuhudie chama chako kinavyokufa " mgeni amelala mgeni, mgeni.... mgeni huyu mgeni..."

Unataka kusema kuwa mgeni aeshaingia chumbani kwa baba na mama??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom