Koffi Annan na Rais Kikwete: Ukweli Uko Wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Koffi Annan na Rais Kikwete: Ukweli Uko Wapi?

Discussion in 'International Forum' started by Brooklyn, Feb 17, 2010.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia suala hili lakini kwa bahati mbaya nimekuwa nikisikia/kusoma habari zinazopingana . Je ni nani aliyefanikiwa kuwapatanisha Rais Mwai Kibaki na mpinzani wake Raila Odinga? Vyombo vingi vya habari vya Tanzania vimekuwa vikiandika/vikitangaza na kumsifu kwamba Rais Kikwete ndio aliyefanikiwa kuwapatanisha Rais Kibaki na Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga mpaka kupelekea kuundwa kwa serikali ya mseto na kumalizika kwa machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.


  Wakati huo huo ukifuatilia vyombo vya habari vya nje/kimataifa kama CNN, BBC, Sky News n.k. vimekuwa vikitangaza kwenye habari zake kwamba mtu aliyewapatanisha Rais Kibaki na Raila Odinga ni Katibu Mkuu wa zamani wa UN Koffi Annan.


  Nakumbuka Rais Kikwete ameshatunukiwa Shahada ya Juu ya Uzamivu (PhD) kwa kutambua juhudi zake katika kuwapatanisha viongozi hawa.
  Je ukweli ukoje katika suala hili? Nani alifanikisha kuundwa kwa serikali ya mseto? Kama ni Koffi Annan, je degree aliyopewa Mh. Rais ilikuwa ni ya kutambua mchango wake katika jambo gani?


  Mbona Rais mstaafu Benjamin Mkapa ambaye naye alishiriki bega kwa bega na Annan hajatunukiwa hiyo shahada?

  Naomba mnijuze wanaJF!
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Aliyepatanisha ni Annan, alikaa Nairobi zaidi ya siku kumi au zaidi, mkapa naye alikwenda pamoja na Obasanjo. Kikwete alihudhuria baada ya kuwa makubaliano yote yameshafikiwa, yeye aliitwa kushuhudia makubalianao hayo wakati huo akiwa ni mwenyekiti wa African Union, hakushiriki hata kidogo katika mazungumzo/muafaka
  Kuhusu hiyo shahada waliotoa si wanajulikana?? nadhani watakuwa na jibu ni kwanini alipewa, labda kitendo cha kupeleka majeshi Comoro
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Unajua sometimes na sisi wakuu tunapenda sifa zisizo na manufaa..so Zanzibar ni nani kaleta maridhiano?

  I really hate cheap popularity! Hivi tunajenga taifa la kulishwa upepo ama?Hebu nipishe mie!
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,914
  Likes Received: 9,561
  Trophy Points: 280
  Hivi Kikwete anaonekana kama mtu mwenye guts au intelligence ya kuwasomesha watu wawili? Huyo katibu mkuu wake wa CCM Makamba tu anamchachafya, huko Zenj tu hataki hata kutia pua, halafu mnasema Kikwete kapatanisha watu Kenya.

  Mugabe alimtukana Kikwete matusi ya nguoni kama mtoto wake hapo Lusaka, na Kikwete hakusema kitu. Kikwete is simply not the gutsy type, hana spine ya kunegotiate na kivuli chake mwenyewe, achilia mbali Mikenya yenye generations za enmity.
   
 5. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu hata kama Kikwete angelishiriki kikamilifu na kuwaunganisha lkn si unajua tena sikio halizidi kichwa?Koffi Annan ni kichwa na anajulikana zaidi ya kikwete na nakumbuka baada ya yeye kukutanan nao kila kitu kikawa shwari hata kama JK alifanya kila kitu lkn Annan alifagia na kumaliza kila kitu na kazi hiyo sana sana aliifanya kimataifa zaidi ya Kikwete Ki East Africa sijui nimeeleweka jamani....
  Hongera kwa kweli kwa Kikwete...na Kuhusu kaka Ben si unajua tena Kikwete ni RAIS alikuwa kiongozi wa something africa sina uhakika..
  maoni yangu tu
   
 6. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hayo ni maoni yako, lakini yapo mbali sana na ukweli, fuatalia from day one mpaka mwisho wa muafaka
  utaelimika zaidi kuliko kutumia maoni yako kama kigezo cha kuwa kikwete alifanya upatanishi huko kenya
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145

  Basi vyombo vyetu vya habari hapa Tanzania vimekuwa vikipotosha watu juu ya hili. Kwa nini tunampa sifa Rais wetu asiyo stahili?

  Nahisi ndo maana vyombo vya Kenya vinaponda sana vyombo vya Tanzania kwa kumtukuza sana Rais Kikwete!!
   
 8. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nimekupata mkuu!!
   
 9. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager

  #9
  Feb 18, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 135
  You can't be serious!
   
 10. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,837
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Ni kwa mkwara wa GEORGE W BUSH rais wa Marekani wa kipindi hicho ndo maana mazungumzo haya yalifanikiwa.Inaaminika kuwa Bush alimwambia Kikwete waziwazi kuhusiana na mgogoro huu na kumpa ujumbe mzito kwenda kwa Odinga na Kibaki..Kikwete alikuwa mjumbe aliyevaa sura ya usuluhishi.Mara tu baada ya kutoka Marekani,rais wetu mpendwa alitia timu Marekani.
   
 11. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dah!! sasa kama ukweli unaujua kwa nn ulize?
   
 12. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mayenga hujaeleweka kwenye sentensi yako ya mwisho! Pili, kwa nini Bush ampige mkwara Kikwete (kama nimekupata sawasawa)? Kwani Kikwete alihusika vipi na mgogoro wa Kenya? Kama ilikuwa kwa sababu Rais Kikwete alikuwa mwenyekiti wa AU, mbona kulikuwa na migogoro mingine barani Africa mfano Zimbabwe na Kikwete hakutia timu kwenda kusuruhisha?
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,627
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Nadhani kwa bahati nzuri tu Kikwete alikuwa ni mwenyekiti wa Afrika wakati huo na alipomwomba Annan amsaidie alikubali kwa roho moja sasa kwa kuwa ndiye aliyempa hiyo assignmet kama Mwenyekiti wa AU, alibidi awe anaripoti kwake maendeleo mpaka ilipofikia mwisho ilibidi amwite Kikwete kuhudhuria kuwekwa saini mkataba ule wa makubaliano. Annan ameshapata shahada nyingi sana hakuhitaji hiyo ndogo hivyo iliyochukua muda kidogo kuipata, akamwachia "brother". Simple as that!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...