Kodtec Speaker systems

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,033
173,709
Kwa wale Music enthusiasts wenzangu last Weekend katika kuzurura katika viunga vya M.City i came across duka la Kodtec. Hawa jamaa wanauza appliances zao mbali mbali pale zikiwemo Subwoofers.

Kishindo cha mziki wenye vipimo madhubuti ambacho sikukitegemea kilipenya katika ngoma zangu za masikio na Ilibidi nizame chap kuuliza jamaa wanioneshe hicho kitu kinachotoa huo mziki. Cha ajabu ilikuwa ni subwoofer box moja hivi with sleek design.

Ukaguzi uliendelea na kuona ni subwofeer box yenye bass speakers 3! 2 Deep bass 12" Speakers kushoto na kulia wakati mbele kuna 10" Mid bass (woofer)! Hii subwoofer iko accompanied na Speaker ndogo za kupiga mid and high frequencies ambazo zinafanikisha hii Kodtec iwe super clear sound system.

Tukija kwenye wattage hii system ni 300Watts RMS value! Utaona kwamba Peak Music Power Output ni obvious itakuwa around 1200w! The bass effects that come out of this subwoofer ni exceptional you hear both boomy and dynamic bass effortlessly sijui wametumia amplifier aina gani humu ila mziki una sound kama mziki wa gari kabisa 😁😁😁!

Kimsingi nilikuwa naona subwoofer za 2.1 Channel ni utopolo ila sio kwa Subwoofer za Kodtec wazee, naomba niombe radhi kwa wamiliki wote wa Speaker Systems za Kodtec!

KT 2913-a-800x800.jpg

UPDATE: Hii speaker ina bass radiators 2 kushoto na kulia ambazo ndio speaker mbili za ubavuni. Mbele ndio kuna Active Bass Speaker.

Kazi ya Radiators ni ku enrich bass frequency iwe deep bass. Ina maana za ubavuni haziko powered ila zina resonate na mapigo ya active speaker hapo mbele ili kuzalisha ile deep bass.
 
Yeah Clarity ipo, siwezi kuisemea sana kwa sababu alinitestia na manyimbo ya kibongo ya wasafi yale with some Nigerian pop!Simu yangu niliacha ndani ya gari parking so sikuwa na pairing device nikatumia ya muuzaji pale pale.

Ila its clarity is audible mpaka nilimwambia apunguze kidogo mchicha. Mi huwa sipendi mziki wenye mids kali, napenda Bass na highs ziwe juu kidogo na balanced.

Ila kwenye bass department that thing did an exceptional job! Japo nyimbo zilikuwa mbaya ile they sounded great. Haina Flat bass kama misabufa mingine ya kichina ile ya boombass tu! Nafikiri ndio maana wameweka speaker za aina 2 tofauti ku cover Lowest Bass Notes na Mid Bass notes! Kwahivyo unapata full dynamic range effects.
Je sauti yake ipo detailed? (inasikika kila kionjo kilichotumika kwenye production?
 
Mkuu naona umeamua kuwa wakala wa kodtec music maana naona unafanya promo kwa nguvu sana.

Kusema ukweli hapo hamna mziki zaidi ya kelele tu, yaani ni sawa na Sea Piano baada ya mwaka au miezi itaanza kukoroma.
Hahahah mkuu mi sio wakala mimi ni Enthusiast! Naomba weekend kama una muda twende mguu kwa mguu mpaka ilipo hio kitu ukajionee kwa macho na upate kusikia mwenyewe, naamini utakuwa balozi mzuri 😁😁😁

Ubora wake sio wa mashaka!
 
Alaaah! Kwa maelezo(specifications/promo) ya mkuu juu nikajua wana range parefu.

Huwa siamini sana kwa bei nafuu kuuziwa kitu bora huwa na wasiwasi.

Hapo ni umakini ndio unahitajika.
Hamna Subwoofer ya Kodtec ya 90k labda tule tudogo twa zamani twenye 50w! Za kati kwenda kubwa zina range kwenye 200K+!

Nimefuatilia na bei zake.

Hio tu niliopost huipati chini ya 350K mkuu.
 
Kodtec wapo smart kiasi fulani tokea awali enzi za kina Rising ambao nao pia walikuwa vizuri, kwa kiasi fulani naweza kusema wamewazidi kina ouling ,sundar na seapiano ingawa bado hawajafikia zile level za wenyewe.

Sio tu kwa performace, bali hata mpangilio wa circuits zao ndani ni tofauti kabisa na hao sijui kina seaPino.
 
Chief hizo bei sio za hii niliopost mie. Hii ni kubwa af ndio toleo current ina watts kubwa! Mlimani wanauza 450K ila najua stores za Kariakoo 300K wanaachia.
Kuna siku nilikuwa natafuta speaker za desktop nikazikuta hizi hizi kodtec mjini 50k mpaka 100k wakati kkoo ni 20k tu.

Kariakoo mall nafkiri ni madalali wa kkoo wame list subwoofer nyingi za 2.1 za kodtec

 
Back
Top Bottom