Kodi ya Simu: Serikali lazima isikilize kilio cha wananchi

Kodi ya Simu: Serikali lazima isikilize kilio cha wananchi

Nape Nnauye

MP Mtama
Joined
Dec 26, 2012
Posts
99
Reaction score
408
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
 
PHP:
Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Vichekesho!
Kumbe unajua serikali yako hainaga usikivu!
Sasa nyie serikali ya ccm kwanini mlibuni hii kodi in the first place, na kwanini mkagonga mabenchi kuipitisha?
Mnawapelekesha wananchi kwa viini macho vya kitoto ili muonekane mnatetea wananchi!
This time you are totally stuck na hatutawaonea huruma...!
Tumecheka na nyani siku nyingi sana!
 
Umeangalia upepo unakoelekea ndo unaleta propaganda hapa shame on u ccm,wabunge wenu ni maarufu kwa kupigia makofi bungeni kwa hoja zisizo na mashiko

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
serikali ya ccm ni serikali sikivu natumaini itasikiliza tu, hata kama ilikuwa ina faidi kwa nchi siyo haramu kubadilika ili kuwaonea huruma wananchi na kufyeka chaka la chadomo watafute siasa nyingine.
 
Umeangalia upepo unakoelekea ndo unaleta propaganda hapa shame on u ccm,wabunge wenu ni maarufu kwa kupigia makofi bungeni kwa hoja zisizo na mashiko

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Uwezo wako ndipo ulipoishia....
 
hii serikali ya JMT inaonekana inafanya mambo kwa kubahatisha. hauwezekani wabunge wote wa cha tawala , mawazari na raisi wafanye maamuzi kwa pamoja alafu ndani ya muda mchache Nape Nnauye uje na kauli kama hii.
mambo ya msingi kama haya lazima mlijadili na kukubaliana.
ila mmeona wananchi wameamua kuonensha msimamo, na CHADEMA ilishaonyesha msimamo wake, sasa umetumwa wew Nape uje uteke hii ajenda kama mlivofanya kwenye mchakato wa katiba mpya

mimi kama mpenda maendeleo, nashauri serikali ionegeze vyanzo vya mapato kwa wananchi, kodi itaongezeka tu.
serikali imeshauriwa kupunguza misamaha ya kodi, kubana uvuvi haramu unaofanya kwenye bahari zetu na maziwa yetu unaonufaisha nchi nyengine....,zuia fedha kutoroshwa kwenda kwenye ma-acc ya nje, ongeza ajira kwa vijana, wekeza kwenye viwanda vidogo vidogo etc, hapo lazima mifuko ya hazina ijae bila kuumiza wananchi wa Tanzania, na matumizi ya mapato hayo yawekwe wazi ili wananchi washilikishwe na wawezi kuishauri serikali jinsi ya kukuza uchumi endelevu....
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Kama ungekuwa genuine haya maneno ungetakiwa kumuita waziri Mgimwa na kumueleza nini cha kufanya lakini kwakuwa unafahamu kabisa kuwa serikali yenu ya ccm imeziba masikio wala haisikii ndio maana umeamua kuja hapa kutafuta huruma ya wananchi kwa kujifanya mnajali maslahi ya wananchi.

Wakati ccm mnafikiria kuianzisha hiyo simcrad tax at the first place mlitakiwa kufahamu kuwa wananchi wengi hali zao za kiuchumi ziko dhoofu na hawatoweza kuzimudu, na hata kama wapo wanaomudu lakini kuna maeneo mengine ambayo bado serikali ingeweza kujielekeza na kukusanya kodi ya kutosha kujiendesha.
 
Serikali ya CCM inakimbia kivuli chake yenyewe..

Kodi ambayo watendaji wako wameipitisha vikaoni huwezi kuja kuipinga hadharani kwenye majukwaa ya kisiasa, Kama watendaji wa serikali(mawaziri) Makamba na yule wa FEDHA wanabishana katika hili tuatiaminije kuwa serilakali ni sikivu zaidi ya kigeugeu???
 
Uwezo wako ndipo ulipoishia....

Nina uhakika kwa hili mimi nina upeo mpana wa kufikiria kuliko hata wewe na ccm yenu woote.....!!mnatoa discount kwa migodi ya madini,mnaongeza mashangingi ma VX ambayo ni gharama kununua na kuyaendesha kwanini msingebana matumizi huku mkalenga mipango ya maendeleo kwa mwananchi kuliko kuendelea kumbebesha mzigo mkulima wa kawaida,Juzi ujio wa maraisi mmeiba bilion 8,huyo chenge aliye propose mtuhumiwa wa mabilioni ya wananchi pia nyinyi ni watu gani msiokuwa na huruma kwa wananchi ,hapo hii fedha ni mpango wenu wa fedha za kampeni na ulaji wenu mwingine huu-tumeshtuka tumewachoka mnanuka rushwa na damu za watu ccm
 
Sina hakika kama unajua unachokisema...laikini pia inawezekana hujui utaratibu unaotumika kufanya maamuzi ndio maana sijui nianzie wapi kukushauri. Swala likishapitishwa na bunge si swala la wabunge flani ni swala la bunge...

Mangapi yamepitishwa na bunge au serikali na Chama tukayapinga na yakabadilika? Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia nani alianza kulipinga hili kati ya vyama vya siasa nchini.

hii serikali ya JMT inaonekana inafanya mambo kwa kubahatisha. hauwezekani wabunge wote wa cha tawala , mawazari na raisi wafanye maamuzi kwa pamoja alafu ndani ya muda mchache Nape Nnauye uje na kauli kama hii.
mambo ya msingi kama haya lazima mlijadili na kukubaliana.
ila mmeona wananchi wameamua kuonensha msimamo, na CHADEMA ilishaonyesha msimamo wake, sasa umetumwa wew Nape uje uteke hii ajenda kama mlivofanya kwenye mchakato wa katiba mpya

mimi kama mpenda maendeleo, nashauri serikali ionegeze vyanzo vya mapato kwa wananchi, kodi itaongezeka tu.
serikali imeshauriwa kupunguza misamaha ya kodi, kubana uvuvi haramu unaofanya kwenye bahari zetu na maziwa yetu unaonufaisha nchi nyengine...., kuongeza ajira kwa vijana, kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo etc
 
Umezidi kuonyesha ulipoishia upeo wako wa kufikiri...endelea kutuonyesha

Nina uhakika kwa hili mimi nina upeo mpana wa kufikiria kuliko hata wewe na ccm yenu woote.....!!mnatoa discount kwa migodi ya madini,mnaongeza mashangingi ma VX ambayo ni gharama kununua na kuyaendesha kwanini msingebana matumizi huku mkalenga mipango ya maendeleo kwa mwananchi kuliko kuendelea kumbebesha mzigo mkulima wa kawaida,Juzi ujio wa maraisi mmeiba bilion 8,huyo chenge aliye propose mtuhumiwa wa mabilioni ya wananchi pia nyinyi ni watu gani msiokuwa na huruma kwa wananchi ,hapo hii fedha ni mpango wenu wa fedha za kampeni na ulaji wenu mwingine huu-tumeshtuka tumewachoka mnanuka rushwa na damu za watu ccm
 
Uwezo wako ndipo ulipoishia....

Kodi ya internet imeongezwa kimya, kodi ya kupiga simu imeongezwa kimya na simcard tax ndio mmetokea malango wa choon

Akili yako haina tofauti na ya huyu jamaa

Prof.+Maji+Marefu.JPG
 
Unaujua utaratibu wa kulifanya hilo unalolisema? Ndo maana wananchi wanamashaka na uwezo wa chama chako kuongoza nchi kama hata mambo madogo ya utendaji kama hilo unadhani ni swala la kumuita waziri na kuelekeza...

Kama ungekuwa genuine haya maneno ungetakiwa kumuita waziri Mgimwa na kumueleza nini cha kufanya lakini kwakuwa unafahamu kabisa kuwa serikali yenu ya ccm imeziba masikio wala haisikii ndio maana umeamua kuja hapa kutafuta huruma ya wananchi kwa kujifanya mnajali maslahi ya wananchi.

Wakati ccm mnafikiria kuianzisha hiyo simcrad tax at the first place mlitakiwa kufahamu kuwa wananchi wengi hali zao za kiuchumi ziko dhoofu na hawatoweza kuzimudu, na hata kama wapo wanaomudu lakini kuna maeneo mengine ambayo bado serikali ingeweza kujielekeza na kukusanya kodi ya kutosha kujiendesha.
 
"Politics is the art of postponing decisions until they are no longer relevant." Henri Queuille
 
Chadema bhana! Ndo maana watanzania wote wenye akili timamu huwa wanakiunga mkono.

Yaani ccm pamoja na Nape mmesoma alama za nyakati mkaona mpera mpera wa Chadema unaweza kuwaondoa madarakani kabla ya wakati kutokana na tozo la kodi kama ilivyokuwa kwa taifa lile ambalo kijana aliyehitimu chuo kikuu kukosa ajira na kodi kuwa kuwa kubwa na askari wa jiji kuharibu vitu vyake baada ya kuamua kufanya biashara ya umachinga then akaamua kujichoma moto na hatimaye wananchi wakaamua kuanzisha vuguvugu la kuiondoa serikali yao madarakani.

Nakuhakikishia bwana Nape kwa tozo hii ya kodi ingeleta mapinduzi ya serikali hii katili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kabla bunge zima halijajua kuhusu hii kodi mawaziri walijua hili!!
Mawaziri hawa ni wanaCCM wenzako, iliwezaje hata kujadiliwa na kuingizwa katika bajeti kama mnajifanya wasikivu leo?!!

Je ukinikanyaga nikachagua kunyamaza, maana yake sijaumia?!

Je wananchi wasingepiga kelele kuhusu hili ingekuaje?

Jibu rahisi ni kwamba hawajui hali halisi ya maisha ya watanzania wengi!

Ni aibu sana kuwa na viongozi wasiojua hali halisi ya maisha ya wananchi wanaowaongoza!

Kama kawaida yake waziri mkuu Pinda akaingia chaka tena (nimeweka tena kwa makusudi maana sio mara ya kwanza kusema kisha akajuta)! Akaitetea! Kisha akaja Raisi 'akaona' logic katika kuipinga!
Kisha mkaja nyie wachumia tumbo mnaotegea teuzi mkaja kufanya propaganda hapa!

Sijui mnaendeshaje nchi yetu kwa kweli!
 
Umezidi kuonyesha ulipoishia upeo wako wa kufikiri...endelea kutuonyesha

ukweli una tabia ya kuwa mchungu,miaka 50 tangia uhuru mmeshindwa kupeleka umeme,maji vijijini mtaweza kwa laini za simu?sera zenu mbovu na nakuhakikishia kwa sasa mmebakiza nguvu ya dola tu ila wananchi wako pamoja na CDM,mmeshindwa kuwaondolea kero ,kuwaletea mahitaji muhimu na bado mnataka muendelee kutawala mwishowe mnaishia kutumia mabavu,kuwang'oa watu meno,kucha n.k!!huko ni kukoma kwa uwezo wenu wa kufikiria-l
 
Nape Nnauye , maeleze yako yanaonyesha maamuzi yanayo fanywa na chama kupitia bunge na serikali ....wewe kama Nape hushilikishwi ...au chama na serikali havijui shida za wananchi. wabunge wa upinazni walipinga sana hii kodi. kuna mbunge mmoja wa CCM alisema "kata hata TZS 500 kwa siku....hao wanaopinga hii kodi wamechangia nini kwenye nchi yetu".....

sasa wananchi wamechachamaa na mmeona ukweli, ndio mnakuja na matamko ya paragraph moja kila siku tatu......

kwanini msikae mkaitoa hii kodi mara moja? au mnatafuta umaarufu?
 
Unaujua utaratibu wa kulifanya hilo unalolisema? Ndo maana wananchi wanamashaka na uwezo wa chama chako kuongoza nchi kama hata mambo madogo ya utendaji kama hilo unadhani ni swala la kumuita waziri na kuelekeza...

Wewe unajua nani alianzisha hizi kodi mtoto wa huyu baba chini ndio akamtupia mzee chenge awalishe watanzania

Makamba2(10).jpg

Kama kweli ccm mmezamilia futa kodi zote kwenye mawasiliano simu na internet
 
Back
Top Bottom