Kodi ya nyumba

Mlalahoi Mlalahai

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
399
146
Kwa wale WANAOJITEGEMEA na wamepanga Nyumba au chumba, hivi huwa unajisikiaje pale tarehe za kulipa kodi zinapokaribia na huna kitu mfukoni na ukifikiria mwenye nyumba ni BANDIDU, au hata kama mwenye nyumba ni muelewa huwa kuna KUJISHTUKIA flan hivi kama hujalipa kodi. Na huwa unajisikiaje ukishalipa kodi?
 
Kama hujajipanga kimuhemuhe chake ni kikubwa yani sawa na rejesho... Lakini ukishamaliza hupata ahueni ya ajabu Kama umetua mzigo mzito saana
 
Nilijiapiza kufunga kunywa bia kwa miaka miwili hadi ninunue kiwanja, namshukuru mungu malengo yakatimia,
Nakaa kwangu, cgongewewi kodi ya nyumba ata kama nakula dagaa sana tu
 
Dawa ni kujenga yako uepuke kudaiwa baada ya kila miezi kadhaa

Kaka mkubwa, kujenga sio kazi rahisi ndio maana hata hao wenye nyumba zao Inapofika wakati wa kulipa kodi huwa wanabadilika hata kama mlikuwa mnacheka utashaanga anakununia gafula sababu akikumbuka wakati anajenga hiyo nyumba alikula msoto wa nguvu.
 
Mbaya zaidi kama mwenye nyumba na Familia yake kubwa ndio wanategemea hiyo kodi ili waishi

Usiombe awe anakaa nyuma jirani au nyumba moja. Kila ukirudi yupo kibarazani, unaingiaje? Asubuhi anaamka saa kumi anajiongelesha ili ujue kwamba yuko available...unaweza kujikuta unasusa chumba kwa muda kama hauna familia.
 
Back
Top Bottom