Huwa najiuliza kwanini serikali ya Tanzania isitenge fungu la pesa na kuingia ubia na kampuni ya Toyota kwa kujenga kiwanda cha uundaji wa magari ya Toyota hapa Tanzania kwani itafanya nchi nyingine Africa zinazoagiza kutoka Japan na Badala yake itakuwa ni Tanzania.
Sidhani kama Kampuni ya Toyota itakataa hii ofa ya nchi kuwa tayar kwenye kujenga kiwanda chao kwa ubia kwani soko la toyota limeiteka Africa na inabidi twende mbele zaidi kupigania hii fursa.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu
-Mnunua gari chakavu hana uwezo wa kununua gari jipya
-Middle Class population hakuna
-Umeme reliable wa production plant hakuna
-No rule of law...ikitokea dispute yeyote labda kodi au labour au chochote,judicial system ya Tanzania ni takataka
-Tanzania haiwezi kua hub ya kuzalisha magari,sio attractive kama Nairobi Kenya au South Africa
-Miundombinu mibovu,bandari bado ya capacity ndogo,etc
-Political system ni ya hovyo,haitabiriki,haiongozwi na Katiba,executive ni next to God,can not be questioned,siwezi weka kiwanda changu mahali mwanasiasa akiamka asubuhi anaweza unilaterally sema kesho nisiwaone bila hata kupitia hearing mahakamani.Yaani mwanasiasa akiwa na chuki na Toyota Company anaweza iua bila huruma,yaani Tanzania mwanasiasa ana power next to God,sio Mahakama ni mwanasiasa ndio ana nguvu!
-Talent pool ya Tanzania ni hovyo,elimu ni duni,STEM field hazina watu,ufanyaji kazi na utamaduni wake ni regressive sio kama Kenya au SA au Ghana au Nigeria,etc
Nini kifanyike:
-Futa katiba iliyopo,weka kama ya Kenya copy and paste
-Mihimili iwe huru kweli sio kwa utashi wa mtu mmoja kama mawe,hapana,ni well designed government machinery system ndio i-guarantee hii hali.
-Revamp judicial system iwe credible zifanye kazi kwa usahihi,mtu kaonewa mahakama itoe haki bila kuingiliwa na Executive
-Elimu yetu,shika chanachana tupa,chukua Singapore copy and paste
-Industrial training na human capital development,revamp ujinga wote!
-Rule of law,law enforcement ifanye kazi haswa
-Weka umeme na miundo mbinu wezeshi
****Elewa Kenya wana offer yote hayo na ziada
Na ndio maana multinationals zote zipo Nairobi...
Haziendi sababu kuna magorofa Nairobi au Kenyatta kasema,
Wana offer mfumo sahihi wa mahakama kampuni likionewa judicial system inachukua mkondo wake,hiyo inavutia internationals zaidi ya magorofa au chochote kile maana mtu ana uhakika hela yangu ipo salama