KODI NI MAENDELEO, Malalamiko ya KODI ni matokeo ya mazoea ya kukwepa muda mrefu...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Naamini maendeleo ya kweli yanaletwa na Watanzania na Kodi zetu.
Nikisikia kitu kimefanyika kwa pesa yetu, huwa nafarijika kuliko kodi ya mwanadamu wa ulaya kunihudumia mimi na matatizo yangu.
Ujanjaujanja wa kukwepa kodi umetulemaza hadi tunapotakiwa kutoa huku pakiwa hakuna mwanya wa kukwepea tunaona kama ni kuua biashara, Tunahujumiwa au maisha magumu.

Taadhali kwa TRA, Kodi ziwe sanjari na Biashara husika na ukubwa au udogo wake.

Tulipeni Kodi, Ili tushiriki kuijenga nchi yetu wenyewe...
Hapo ndipo tutaona Uchungu wa kukemea kwa Uzito mkubwa matumizi yasiyo ya Uzito nchini.
 
Inaelekea wewe ndio walewale wapiga domo, kama wa Waziri wa Fedha abaye yuko on record kutojua kwa nini biashara zaidi ya 2000 zimefungwa hadi mwanzoni mwa mwaka huu.

Kuna watu mna mentallity ya master~slave kati ya serikali na mfanyabiashara.

Matokeo yake tunayaona wazi, biashara zinafungwa!

Je wajua kuwa ukiajiri mtu, licha ya kumlipa msgahara unakuwa penalised kwa kodi?

Je wajua kuwa pamoja na kodi nyingi za TRA, zina fines nyingii za kukomoa tu wafanyabiashara?

Je wajua kuwa kuna kodi kero nyingi tu za serikali za mitaa za umiliki tu pale unapokaa?

Je wajua kodi nyingi za taasisi za serikali kama FIRE, NSSF,/GEPF, TBS, TMAA, WMA, NEMC, WC(Workers Compensation) etc

Je wajua gharama mbovu kwa wafanyabiashara kutoka service providers kama TANESCO, DAWASA, TFDA etc

Hizo zote ni gharama za biashara yoyote ile.
Sasa mtoa mada fungua hata kiosk lipa kodi zake halafu tumbie unauza nini kwa faida ili baada ya hapo ulipe karo za shule ya watoto wako!

Msiongee kwa mazoea wakati hata fremu ya duka hamjui kuiendesha.
 
Mimi ni mlipa kodi mzuri na nilikuwa napenda kuhamasisha watu, ila ujinga unaofanywa na watu wa TRA kwenye kukadiria ni majanga unakuta wanakuambia" kodi za watu wa biashara fulani ni hiii" bila kujali tofauti kwenye mtaji" mtu mwenye mtaji wa milioni kijijini anaweza pewa kodi sawa na mwenye milioni 20 mjini.
 
Sawa tumeshakujua unafanya kazi TRA.asubuhi njema.
 
Sijawahi kusikia mtu akiajiliwa muajiri anakuwa penalized. Toa mfano na kwa mazingira wapi au ndio kuajiri Bila kufuata taratibu za sheria za kazi?

Kwa nini mfanyabiashra apigwe faini wakati anacomply na ulipaji kodi, wacha kulalamika weka ni mazingira gani upigwe faini.

Kuhusu kero za halmashauri au mitaani Naunga mkono, nazo kodi ndogo ndogo ziliahidiwa kushughulikiwa

NSSF /GEPF hizo sio kodi mkuu usichanganye mambo.

Matatizo ya Tanesco na Gharama zake au dawasco sio kodi pia, tusichanganye changamoto za biashara na kodi

Kuhusu kufungua kioski, unapaswa kulipa kodi kulingana na unachouza. Kama Kuna mabadiliko au hali mbaya nadhani Kuna utaratibu wa kukadiliwa upya kama Kuna urasimu tra tuulani sio kulaani kodi au kulipa kodi.

Nchi ya Tanzania inaendelea kwa kodi za watanzania sio misaada ya kodi za raia wa ulaya.
 
Unamiliki biashara gani mtoa hoja??
Tunazungumzia kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yako. Sio aina ya biashara ambazo tunazo.
Kama kodi ni kikwazo kwa ukuaji wa biashara yako pendekeza ufanyeje ili kodi ulipe na biashara iendelee.

Tanzania inaendelea kwa mapema kwa kodi zetu sio kodi za wazungu na biashara zao huko ulaya.
 
Mimi ni mlipa kodi mzuri na nilikuwa napenda kuhamasisha watu, ila ujinga unaofanywa na watu wa TRA kwenye kukadiria ni majanga unakuta wanakuambia" kodi za watu wa biashara fulani ni hiii" bila kujali tofauti kwenye mtaji" mtu mwenye mtaji wa milioni kijijini anaweza pewa kodi sawa na mwenye milioni 20 mjini.
Hilo ni tatizo kubwa, na mimi limeshawahi kunipata, mama mmoja pale tra vingunguti, analazimisha mauzo kwa siku anayotaka yeye wakati uhalisia mauzo ni nusu ya Anachokisema. Juhudi zote kadilio la mauzo kwa siku kwenye uhalisia huwa linafanikiwa mara moja kwa wiki. Siku nyingine zote ni chini ya alichokadilia. Cha ajabu katika usukununu Mule ndani nilikuta Kuna wengine wamekadiliwa mauzo yaleyale ambayo mimi aliniambia kama ni hayo unatafuta tin ya nini sasa? Nikaona kama Kuna usanii mwingi kwenye mambo ya msingi kama yale. Nikaelewa kwa nini mtaa Ule tra wakipita Maduka yanafungwa na nilitaka niwe wa kwanza kulipa kodi mtaa mzima. Nilisitisha zoezi lkn nitawarudia, Kama raia ninaetambua ni wajibu wangu kulipa kodi ila pia siko tayari kulipa kodi ambayo haiko proportional na mapato yangu hiyo ni fact. Yote hayo sio excuse ya kutokulipa kodi.

Hizo ni changamoto za wakusanya kodi ila sio kodi yenyewe. Kwa faida ya Taifa letu Kila mtu ajitahidi kulipa kodi sahihi Bila kukwepa. Wakusanya kodi nao wawe waungwana wasikatishe tamaa watu kwa kuwapangia makodi kwa kuangalia wao tu kutimiza magoli waliyowekewa Bila kujua ni heri mtu alipe kwa term 50,000 mfano kwa miaka yote, kuliko kulazimisha mtu huyohuyo alipe 200000 mfano na biashara ikafa kwa mwaka. Hapo mkusanya kodi atakuwa kaishiwa maono
 
Inaelekea wewe ndio walewale wapiga domo, kama wa Waziri wa Fedha abaye yuko on record kutojua kwa nini biashara zaidi ya 2000 zimefungwa hadi mwanzoni mwa mwaka huu.

Kuna watu mna mentallity ya master~slave kati ya serikali na mfanyabiashara.

Matokeo yake tunayaona wazi, biashara zinafungwa!

Je wajua kuwa ukiajiri mtu, licha ya kumlipa msgahara unakuwa penalised kwa kodi?

Je wajua kuwa pamoja na kodi nyingi za TRA, zina fines nyingii za kukomoa tu wafanyabiashara?

Je wajua kuwa kuna kodi kero nyingi tu za serikali za mitaa za umiliki tu pale unapokaa?

Je wajua kodi nyingi za taasisi za serikali kama FIRE, NSSF,/GEPF, TBS, TMAA, WMA, NEMC, WC(Workers Compensation) etc

Je wajua gharama mbovu kwa wafanyabiashara kutoka service providers kama TANESCO, DAWASA, TFDA etc

Hizo zote ni gharama za biashara yoyote ile.
Sasa mtoa mada fungua hata kiosk lipa kodi zake halafu tumbie unauza nini kwa faida ili baada ya hapo ulipe karo za shule ya watoto wako!

Msiongee kwa mazoea wakati hata fremu ya duka hamjui kuiendesha.
Hongera sana mkuu umenifariji wakipatikana 10 tu nchi nzima kama wewe , hakika tanzania itabadilika kiuchumi bado kuna tatizo kubwa sana la VAT na mfuko mbovu sana wa kiuchimi/kodi unafirisi sector yoote binafsi
 
Tunazungumzia kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yako. Sio aina ya biashara ambazo tunazo.
Kama kodi ni kikwazo kwa ukuaji wa biashara yako pendekeza ufanyeje ili kodi ulipe na biashara iendelee.

Tanzania inaendelea kwa mapema kwa kodi zetu sio kodi za wazungu na biashara zao huko ulaya.
Usidanganye watu hapa "UPENDEKEZE ? ? ? KWA NANI TRA ? ?" jumuiya zeneywe za wafanyabiashara hazisikilizwi hadi viongozi wao wana wekwa RUMANDE kama magaidi, TCCIA hawasikilizwi, yawezekana wewe ni wa TRA maana ndio majibu yao ya karne
 
Sijawahi kusikia mtu akiajiliwa muajiri anakuwa penalized. Toa mfano na kwa mazingira wapi au ndio kuajiri Bila kufuata taratibu za sheria za kazi?

Kwa nini mfanyabiashra apigwe faini wakati anacomply na ulipaji kodi, wacha kulalamika weka ni mazingira gani upigwe faini.

Kuhusu kero za halmashauri au mitaani Naunga mkono, nazo kodi ndogo ndogo ziliahidiwa kushughulikiwa

NSSF /GEPF hizo sio kodi mkuu usichanganye mambo.

Matatizo ya Tanesco na Gharama zake au dawasco sio kodi pia, tusichanganye changamoto za biashara na kodi

Kuhusu kufungua kioski, unapaswa kulipa kodi kulingana na unachouza. Kama Kuna mabadiliko au hali mbaya nadhani Kuna utaratibu wa kukadiliwa upya kama Kuna urasimu tra tuulani sio kulaani kodi au kulipa kodi.

Nchi ya Tanzania inaendelea kwa kodi za watanzania sio misaada ya kodi za raia wa ulaya.
Mkuu unslitazama suska zima kama mwanasiasa na si mjasiria mali.
Leo ajiri watu wanne tu kwa kazi yoyote na ukumbane na kadhia ya kodi zake.

Hatavwawekezaji wakubwa wamelalamika juu ya The Cost of doing business in Tanzania.
Ni prihibitive!
Kwa taarifa yako makato yoyote ambayo ni statutory, hayana tofauti na kodi.
Ni pesa inayotokana na biashara, cost of business.

Hivyo basi ukiajjiri hiusegirl wako, mlipe msharavkiwango cha chhini, mlipie SDL, NSSF, WC etc, pamoja na overtime na likizo ya malipo.
Sisemi hayo mtu asilipiwe, nasema ukiwa sasa na watu 200 pamoja na kodi nyingine zote, kodi hizo hazilipiki.
Huko mawizarani watu wawe creative, ili kuja na kodi na mifumo yake ambayo ni endelevu.
 
Naamini maendeleo ya kweli yanaletwa na Watanzania na Kodi zetu.
Nikisikia kitu kimefanyika kwa pesa yetu, huwa nafarijika kuliko kodi ya mwanadamu wa ulaya kunihudumia mimi na matatizo yangu.
Ujanjaujanja wa kukwepa kodi umetulemaza hadi tunapotakiwa kutoa huku pakiwa hakuna mwanya wa kukwepea tunaona kama ni kuua biashara, Tunahujumiwa au maisha magumu.

Taadhali kwa TRA, Kodi ziwe sanjari na Biashara husika na ukubwa au udogo wake.

Tulipeni Kodi, Ili tushiriki kuijenga nchi yetu wenyewe...
Hapo ndipo tutaona Uchungu wa kukemea kwa Uzito mkubwa matumizi yasiyo ya Uzito nchini.
Mkuu malalamiko siyo kwa sababu ya kukwepa kuzilipa. Kodi zetu sio rafiki. Ni kubwa mno na kuna multiple taxation. Kitu kimoja unakilipia kodi mara kibao. Halafu watanzania sisi vipato vyetu haviendani na hizo kodi. Hivi kwa mfano, unadhani watu hawalipi kodi za majengo kwa vile hawataki? Hapana. Watu ni masikini sana. Nina title deed ambayo ipo kwa jina la ndugu yangu, nimeshindwa kubadilisha jina kwa sababu ya kodi ninayotakiwa kulipa. Hiyo sehemu nimeishadevelop kwa hiyo valuation eti siku hizi inategemea eneo kwa hiyo plus thamani ya hiyo development natakiwa kulipa milions of money. nimeshindwa nasububiri muujiza utokee nipate hizo milioni ndipo nifanye transfer. tatizo ni uwezo wetu mkuu siyo kutotaka kulipa kodi maana kodi ndiyo maendeleo ya taifa letu.
 
The revenues of developing countries like Tanzania depends on service while developed countries depend on industries! Kodi zitokanazo na huduma zote ni kero, nashangaa kusikia mara kodi hii ni kero mara nyingine sio kero. Niwaulize swali, ni mwananchi gani wa tanzania aliyewahi kuridhia kukatwa asilimia 18 (VAT) kila akinunua chochote hata chumvi. Uwe maskini au tajiri ni 18% (VAT). Tutafute namna ya kutegemea mapto kutoka kwenye huduma. Ndio maana sasa hivi polisi wamekuwa kitengo cha TRA!
 
Si kweli kwamba wanaolalamika hawalipi Kodi, Malalamiko ni milolongo ya kodi zisizoeleweka na ambazo hazina uhalisia.

ili uwaambie watu walipe aina fulani ya kodi lazima ufanye uchunguzi wa kina na utengeneze mfumo utakaokuwa wazi kwa kila mtu, mfumo utakaotambua nini maana ya biashara, mfumo utakaokuwa rafiki kwa mlipa kodi na si mlipwa kodi.
Huwezi kutoza mtu kodi kuanzia bandarini mpaka dukani kwake ukiwa hujui gharama halisi za manunuzi, usafirishaji, soko huko dukani likoje na mwisho wa siku faida kiasi gani inapatikana na ndio na wewe uweke kodi kiasi gani na lazima ujue mwisho wa siku huyu mfanyabiashara atapata faida kiasi gani na si kumuacha ajue mwenyewe huku wewe umeshachukua kodi...
 
Sisemi hayo mtu asilipiwe, nasema ukiwa sasa na watu 200 pamoja na kodi nyingine zote, kodi hizo hazilipiki.
Huko mawizarani watu wawe creative, ili kuja na kodi na mifumo yake ambayo ni endelevu.

Asante mkuu, nashukuru hukuwaza kisiasa kama mtoa maada, ila umevaa uhalisia..

CREATIVITY+SKILLS+EXPOSURE = Tatizo kubwa kwa watu wetu.
Lazima tukubali kuna vyeo kwenye taasisi fulani fulani siasa ziachwe, iangaliwe "exposure" kiasi gani mtu anayo iende sambamba na vyeti vya kitaaluma.
 
UWEZO MDOGO KIAKILI KWA WATENDAJI WETU NI TATIZO KWA TANZANIA TOKA 1961 MPAKA 2017, NDIO MAANA TUKO HAPA NA MWENDO UMEKUWA WA KOBE NA KIJANA KAMA WEWE UNAPIGA MAKOFI TU NA KUSHANGILIA..
 
Kodi za nchi hii zimekuwa za kukomoana na kufilisiana, hakuna anae kataa kulipa kodi ila kodi zimekuwa nyingi mno za makadirio bila kujali kiasi cha pesa zilizoingizwa kwenye biashara, utaratibu kwa TRA kutaka kufikisha malengo ambayo hayafikiki ili tu kutimiza MALENGO YAO bila kujali hii kodi inakusanywa kihalali au kuumiza mfanyabiasha ndio inayo udhi.
 
Asante mkuu, nashukuru hukuwaza kisiasa kama mtoa maada, ila umevaa uhalisia..

CREATIVITY+SKILLS+EXPOSURE = Tatizo kubwa kwa watu wetu.
Lazima tukubali kuna vyeo kwenye taasisi fulani fulani siasa ziachwe, iangaliwe "exposure" kiasi gani mtu anayo iende sambamba na vyeti vya kitaaluma.
Huyu mtoa mada ni chair warmer!
Hajawahi kuendesha biashara wala kujua matatizo ya kodi zetu.
Kuna watu wanafikiria nchi itaendeshwa kwa kumkamua mtu mpaka kaburini.
Hawajui huyo mtu anaweza kujiondoa kabisa katika masuala yakibiashara ili asisumbuliwe!
 
Asante mkuu, nashukuru hukuwaza kisiasa kama mtoa maada, ila umevaa uhalisia..

CREATIVITY+SKILLS+EXPOSURE = Tatizo kubwa kwa watu wetu.
Lazima tukubali kuna vyeo kwenye taasisi fulani fulani siasa ziachwe, iangaliwe "exposure" kiasi gani mtu anayo iende sambamba na vyeti vya kitaaluma.

Ha ha ha
Inanikumbusha ati lipeni kodi bila shuruti!!!!
Kodi ambazo kwa ujumla wake hazilipiki kwa vile hao wanaoziplan hizo kodi aidha hawajui au hawana exposure ya effets za kodi hizo katika jamii au biashara.
 
Back
Top Bottom