Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,190
- 27,237
Nimeona wengi wakipiga miluzi kuhusu Kodi zilizoongezwa hasa kwenye Luku, miamala ya simu, kadi za simu na kwenye mafuta (petrol na diesel).
Ilikuwa bado kidogo tu na Mimi niingie mtego wa makamanda kwenye kulalamika.
Kwanza kwanza kabisa yapaswa ieleweke kuwa hakuna nchi duniani inaweza kuendeshwa bila Kodi.
Kwenye kupata kodi serikali huwa hawacheki na kima, ni lazima Kodi ilipwe hakuna janjajanja.
Ni kweli bajeti mpya imeongezwa Kodi kwenye petrol, na miamala. Swali la kujiuliza ilibidi kodi iongezwe wapi ambapo watu hawatalalamika?
Mnataka nchi iende Ila hamtaki kulipa Kodi, itaendaje? Kwa kufanya siasa na hivyo vikao vyenu mnavyofanya kila siku? Hili swali nimelilenga maalum kwa makamanda, hasahasa wale makamanda uchwara.
Mama Samia kwa kadri itavyokupendeza ongeza Kodi kwenye vitu ambavyo vitasababisha wengi watalipa kama ulivyofanya sasa kwenye miamala na petrol.
Wabongo ni walalamishi by nature, wala usisikilize ziba kabisa masikio maana watakupotezea focus alafu baadae ndio wa kwanza kukutukana.
Hawa makamanda wanaolialia humu wanapenda sana dezo na burebure na ndio maana unaona hata baadhi ya viongozi wao wa juu wapo ulaya wao na familia zao wanaishi kula na kulala bure kwa jasho la wananchi wa hizo nchi.
Hizo nchi ambazo wanaishi kwa kula na kulala bure Kuna kodi nyingi na ngumu kuliko hata huku kwetu. MSIPENDE VYA BUREBURE
Ili nchi iendelee lazima tufunge mkanda, hakuna kurudi misri ni lazima tufike nchi ya ahadi.
Miradi yote mikubwa iliyopo ni lazima iishe na ianzishwe mingine kwa Maendeleo ya taifa.
KAZI IENDELEE