Knowing The Unknown | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Knowing The Unknown

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Me370, Jun 28, 2012.

 1. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ok, This is how it was. Nlienda Mbeya kikazi kwa muda wa kama wiki 3 hivi tokea 29th May mpaka 21st June. Muajiri alinilipia Hotel na chakula pale hoteli nlikuwa nikila ninachotaka na ku sign tu. Kabla hata wiki haijaisha nligundua kuwa nahitaji Companion wa kike to get me through the weeks. Nkapiga simu naumwa next day na kwenda kuzurura Town. Katika pitapita zangu mkononi nikiwa na T-shirt 3 kali za mtumba nlizokuwa nimenunua siku hiyo nkamuona binti bomba sana kwa mbali. All was fine mpaka nlivomsogelea nkaona kabeba mtoto mchanga mgongoni, Nkajipa moyo sio wake na kumuingia. Nlimuanza kwa kumshauri amfunike vizuri mtoto kwani hali ilikuwa baridi na upepo mkali. Nlimsifu mtoto alivyo mzuri huku nikiuliza jina la mtoto na kudai kafanana na mama yake. Nia yangu ilikuwa ni kuhakiki mtoto ka ni wake. Alikana na kudai kachukua sura ya baba yake. Anyway Story zilianzia hapo na nliendelea kuongea naye huku tukitembea kwa pamoja. Tulipanda basi moja ingawa nilikuwa siendi anakoenda, aliposhuka nami nkashuka na kupewa namba kwa sharti nsipige usiku.

  Siku iliyofuata Nliripoti kazini na lunchtime nkampigia. Tuliongea kwa kama saa nzima. Alinieleza kazalishwa na mume wa mtu (Mkristo) so hawezi kuolewa naye. Aliendelea kueleza jamaa anahudumia kila kitu kampangishia chumba na anampa elfu 5 per day yaani 150,000 per month pia mtoto akiumwa na hela ndogo kama vocha e.t.c. Tulizoeana kwa kipindi kifupi nkamualika hoteli aje tubadilishane mawazo kama friends na kumtumia tax mida ya jioni akaja. Tukaongea tu ile siku bali jumaamosi ya wiki ile nlishinda hotelini akaja na kuanzia siku ile tukawa wapenzi. Kama kawaida ya mwanaume mimi uongo mwingi nlimmwagia na ahadi kibao fix. Mapenzi yalinoga mpaka akaacha kulala kwake na kuhamia pale hotelini kwangu. Alikuwa ananyonyesha mtoto so nilikuwa najilia tu peku.

  Matatizo yalianza pale Baba wa yule mtoto alipoambiwa na wapambe kuwa nyumba ndogo yake hailali tena nyumbani. Alikuwa na funguo za ghetto la yule demu so akaenda kubeba kila kilicho mle ndani alichomnunulia yule demu. Mwenye nyumba akakabidhiwa chumba apangishe na kurudisha kodi iliyobaki. Tulienda wote kwake nikayashuhudia haya. Baada ya mimi kuona hivo, siku ninayoondoka (21st June) nilimuamishia mrembo wangu guest ya bei rahisi na kumlipia siku 10. Nkamuachia na 50 ya kula siku 10. Nkasepa na kurudi Dar.

  Sasa hapa Kichwa kinaniuma nisaidieni wana JF nifanyeje? Ukichehe wangu umefanya nimejitwisha Limzigo likubwa na mbaya zaidi yule mwanamke kwao waislamu hivyo kuzaa na mkristo na kukubali kuwekwa nyumba ndogo walishamtenga na hili alinambia mwanzo kabisa. So kurudi kwao hawezi maana huwa wanamfukuza tu. Hapa kichwa kinaniuma mawazo hayaishi. Mtoto sio wangu so SIWEZI hudumia milele na kodi ya guest na hela ya kula yule mwanamke vinaisha in 4 days time. Alisharudi kwa baba wa yule mtoto kamkataa na sasa anasema yule mtoto sio wake maana demu malaya. Mpenzi mwenyewe hana ushauri wa maana analia tu siku nizima hata tukiongea kwenye simu kilio tuuu. Nafikiria sijui nimzimie simu au? Please, PLEASE, PLEASE, PLEASEEEEEEEEE Nishaurini Najitoaje humuuuuuuuuuu.
   
 2. a

  anily Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Story yako inatufundisha nn!?
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  linywe, uzuri hujaoa
   
 4. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  huyo dada nae!!!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  i am proud of you kwa kuwa ni jambo linalo kuumiza moyoni

  wengine ingekuwa ndo washasahau bila kujali maumivu kwa mwenzie....

  so far you are doing good....

  hongera
   
 6. s

  shosti JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  jamani jamani du!
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huyo dada kafanyaje?

  unajua thamani ya mwanaume anaetoka DSM mikoani?

  sawa na nyie mkiona wazungu mnavyo chachatika
   
 8. B

  Bankrupt Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suluhisho hapo ni kufanya mipango ya kuishi na huyo dada kihalali. Ila wanawake wanapenda ndoa hadi wapo tayari kurisk maisha yao.
   
 9. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ushauri wangu ni kamchukue huyo binti ukae nae. Kwakuwa alikusimulia kwamba ametengwa na familia yake na huyo bwana aliyezaa nae ndiye alikuwa akimuweka mjini, na kwakuwa wewe ndiye chanzo cha huyo bwana kuacha kumhudumia/kumtunza yeye na mwanae, basi mazee we chukua hilo jukumu kwa roho safi tu.
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kila anaeingia kwenye mchezo wa mapenzi huwa na lengo lake. Lako kama lilikuwa kudanganya basi endelea kwa kukata mawasiliano kwani huna ulichobakisha huko nyuma na kama ulikwenda kwa mapenzi hasa basi beba kwani huo si mzigo wa kushangaza kwani takriban kila mwanamme hufanya mbinu na jitihada kupata mzigo kama huo seuze wewe ulioupata kirahisi, hauna kudai michango ya harusi, hauna baruwa ya posa wala mahari.
  Beba tu kijana.
   
 11. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  uko soo kind,na mie ni singo maza nije kwako?lol:israel:
   
 12. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkulu wewe unaonekana ni mtu mstaarabu kwakizungu wanaita "a good man"

  Hapo una alternative 2. Moja: mwambie ukweli kuwa wewe hauna long term plans na yeye kwakuwa kwa sasa bado hauko in a position ya kuishi na mwanamke. Na kwaajili hiyo ushauri wangu ni kuwa ungemtafutia chumba cha kupangisha huko Mbeya ukamlipia miezi kama 6 (itakuwa kama laki na hamsini tu) then mpe laki ya matumizi for probably a month na umuache kwa amani. Mlikutana kwa amani muachane kwa amani. Ila mueleze ukweli kuwa wewe unaachia ngazi ili ajiandae na future yake. Baada ya muda yule baba watoto atarudisha majeshi please believe me.

  Alternative ya pili: kama dada ametulia na wewe unam fill basi mchukue uishi nae although kwa mujibu wa malelezo yako wewe unaonekana unatafuta njia ya kutua huu mzigo.


  Lakini please usimzimie simu na kum dump bila kumuacha with some kind of direction na msimamo!
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo thatha umechokonoa mzinga wa nyuki,subiri the fairer sex wakushukie!
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  mkuu The Boss umemaliza kila kitu, mtu ukitoka dsm na kwenda mikoani unaonekana wa class nyengine, watu wanajua lazima iko shekeli ya kutosha.
  Sasa ukizingatia kwamba binti mwenyewe ni kama alikuwa katika mazingira magumu, ametengwa na familia yake sasa akajikuta anaangukia katika mikono ya wapendao miteremko sasa limekuwa balaa kwake.

  Kwa mtu asiyependa miteremko asingepoteza muda kutongoza mwanamke mwenye mtoto mchanga kiasi hicho, tena anajisifia kwamba alikuwa anajitafunia kavu kavu!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Thanks Jestina for your observation.
  Hata wewe ukiangalia mazingira ya huyo binti, kuzalishwa na mtu ambaye hana matarajio yoyote naye, kutengwa na familia yake, kisha sasa amekataliwa na huyo bwana aliyekuwa anamuweka mjini, hapo kunahitajika moyo wa ubinadamu japo kiasi kidogo.
  Wakati mwingine tukubali kubeba majukumu yanayotokana na tamaa zetu za kimwili ama uongo wetu.

  btw, ombi lako bado ninalitafakari.:thinking::thinking:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Umeharibu kitumbua cha mwenzio, sasa unadhani ataishije? Kama una mpenda basi oa kwani mtoto si unaatunza tu?Ila nampa pole uyo dada kwa kukuruhusu kula KAVU KAVU, mana health status yako ni UNKNOWN, mhh! Nipe namba yake nimshauri akapime achukue tahadhari mapemaa asije muambukiza mtoto wake bure (in case umeshamuambukiza......)Mh, ila nawewe HUJATULIA KABISAAA!
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Unalo Hilo baba,ungekuja kuomba ushauri kabla ya kumuibia mwanaume mwenzio Mali sake za wizi. Dhulma haidhulumiwi baba
  :eek2::eek2:
   
 18. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mtoa mada mwiziii, Huyo msichana mwiziii, aleyeibiwa mwiziii na baadhi ya wachangiaji hapa ni weziii!
  Wizii mtupu kila kona!


  Mkuu with the decency left in you...Jitoe as sacrifice ili hata Mungu akukumbuke beyond your damage. Jichange urudi ukamkodie chumba kwa kodi ya mwaka(sidhani kama itakuwa kazi sanaa!) kisha umuanzishie hata ka M-pesa aingize income...Think of the innocent child! duh!
   
 19. ThePromise

  ThePromise JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh!ila wewe nae unajitahd!mwanamke ananyonyesha tena mtoto si wako stil ukamparamia!hukumuonea huruma huyo mtoto?unafaham kunakitu kinaitwa kubemenda mtoto?ndicho mlichofanya wewe na huyo mwenzio!wote uelewa wenu uko level moja,its better muoane tu,maana tofaut na hapo mtawasumbua sana wenzenu!..usimuache,muoe!
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  jamani lets be realistic, huyu bidada jamani tukumbuke kuwa anamsongo wa mawazo ya kuwa na ugomvi na familia ambao umempelekea kukosa liwazo kwa baba watoto wake. Pia tukumbuke kuwa anahitaji faraja nafsini na hata kutamani kuwa mke wa mtu awe na all privilege ambazo wanazo wamama wengine kama wake za watu.

  binafsi napenda kusema kuwa kaka mzuri pima moyo wako kama kweli umemfeel just go and take her, muoe awe mkeo kwani umekuwa na mikosi maishani mwake na mwanae. sikupi alternative nyingine yeyote kwaniulikwenda kulichota kwa hiari so ulinywe
   
Loading...