KKKT yakanusha kuzuia ndoa za wanawake waliozaa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
96,225
168,790
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limekanusha kupiga marufuku ufungishaji ndoa madhabahuni kwa wanawake waliozaa.

Barua ya juzi ya Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani Godfrey Nkini, iliyoifikia Nipashe jana iisema hakuna waraka au tangazo lolote la kanisa hilo ambalo liliwahi kutolewa kuhusu suala hilo.

Toleo la mwisho la Jumapili liliandika kuwa KKKT imepiga marufuku ufungishaji ndoa madhabahuni kwa wanawake waliozaa.

Aidha, habari hiyo ambayo chanzo chake kilikuwa tangazo lililodaiwa kutolewa katika Mtaa wa Neema ilidai KKKT imepiga marufuku ufungishaji madhabahuni pia wanawake wenye ujauzito kufunga ndoa madhabahuni kwa maelezo kuwa kufanya hivyo ni kukiuka maandiko ya MUNGU.

Lakini taarifa ya Nkini ilisema; Habari iliyohusisha Mtaa wa Neema, ni ya uongo na imepotosha umma.

Taarifa hiyo pia ilisema hapakuwa na tangazo lolote lilotolewa na KKKT kama ilivyoandikwa.

Alipoulizwa ufafanuzi juu ya tangazo hilo wakatiwa ufuatiliaji wiki iliyopita, Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mchungaji Anta Muro hakukubali wala kutaka kutangazwa kwake badala yake alimwomba mwandishi kuwasiliana na gazeti la Upendo linalomilikiwa na kanisa hilo.

Chanzo kimoja cha habari kiliiambia Nipashe Jumapili kuwa tangazo hilo lilltolewa ibadani katika Mtaa wa Neema wa Mbezi Luis wiki mbili zilizopita.

Chanzo: Nipashe
 
Kwahiyo wanakubali kuwa watafunga ndoa hata watu wakiwa wajawazito?
 
Ndo wanachomaanisha kwa kukanusha. wameona watapoteza waumini(sadaka). Yesu arudi tu haraka
Wamekanusha kutokuwepo kwa tangazo la namna hiyo. Kwa utaratibu wa KKKT, matangazo yote yatolewayo kwa waumini YANAANDIKWA, hivyo bila ushahidi wa maandishi inamaanisha tangazo halikuwepo.

Suala la kufunga ndoa mmojawapo akiwa mjamzito, watu tunaliangalia kwa mtazamo wa nje (kimwili), lakini kiroho, wafungishwa ndoa ndio wanajua WAMETENGENEZA vipi na MUNGU wao. Tusihukumu tusije hukumiwa!
 
Back
Top Bottom