Kizuri kula na mwenzio!!!! itakufaa na wewe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizuri kula na mwenzio!!!! itakufaa na wewe.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by dadam, Apr 21, 2011.

 1. dadam

  dadam Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wapendwa, nimekua nikisoma sana post na coments zenu za humu JF, lakini sijawahi waza kupost Topic au coment kwa sababu ninazozijua...ila leo imenibidi niwashirikishe hili...
  Jamani nina furaha.......nilikua na tatizo na mume wangu kwa takribani miaka miwili sasa. kwa kweli ni tatizo ambalo hata kulisema hapa nilishindwa.. nilishaomba ushauri sana hadi kwa wachungaji na kuombewa ila ilishindikana..kiufupi, mume wangu alikua anapenda sana kujifunua na kuacha sehemu zake nyeti wazi kwa kumuonyesha mwanamke...mara nyingine alikua hadi anawachafua watu kwenye daladala na mbegu za kiume. amini usiamini hadi vitoto vidogo vilikua vinakuja kunilalamikia kua mume wangu anawaonyesha dudu lake. ...alishawahi kupigwa kwa kumchafua dada wa watu ktk daladala ila mimi nilikuja kujua baada ya muda mrefu sana.

  mwanzoni nilikua nikimuuliza anakataa lakini ilifika siku nikamfumania ndipo alipokubali na kuniambia kua asipofanya hivyo hapati hamu ya kufanya mapenzi na mimi. leo kuna muujiza umetokea kwani sidhani kama ni kawaida

  kuna rafiki yangu alinipa namba ya dada mmoja..yaani nikimkumbuka nafurahi hadi machozi yanatoka, huyo dada nahisi alisoma mambo ya saikolojia. tuliongea nae akasema kua angejaribu kuongea na mume wangu. tulifanikiwa kiujanja kumpa namba yake na kumwambia asimwambie kua ni mimi nimempa...
  jamani, baada ya siku tano alinambia ameshakutana na mume wangu.

  aliongea nae na alikua akinambia tusubiri na niwe namfuatilia kujua maendeleo yake. ninavyoandika sasa, nina miezi miwili sijasikia kesi ya namna ile... cha ajabu leo mume wangu kanitoa lunch..(haijawahi tokea kawa miaka miwili sasa) na kikubwa alitaka kunipongeza na kunishukuru kwa kua mvumilivu kwani sasa tatizo lake limeisha. sikuamini...niliruka hadi nikamwaga soda niliyo kua nakunywa..
  leo nimempigia yule dada hapatikani....daaaa natamani nitoboe simu nimpate
  natamani ni jue ni dawa gani alimpa ila alinambia hatonambia chochote isipokua kwa ridhaa ya mume wangu. mume wangu nae nahisi kanificha kwani anasema hajatumia dawa yoyote. eti mimi ndo nilikua dawa.
  ila ndugu zangu wana Jf....naogopa kumwambia mume wangu kua mimi ndo niliemuunganisha kwa huyo dada kwani atahisi nilikua natangaza tatizo lake. natamani sana kujua ni tatizo gani hasa hili...Mungu ni mwema.....yaani nina raha sijui hata nisemeje,...namshukuru mungu kwa kweli...hakuna lisilowezekana kwa mungu chini ya jua kwani naamini sio akili ya yule dada bali ni mungu tuu looo...dada mwenyewe ni mtoto tuuuu alafu hata hafananii...usimjaji usiyemjua ...
  usiku mwema.
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kahiyo mumeo alikuwa dungadunga ? una bahati hajapigwa mawe,pole sana dunia ina siri nyingi.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hongera mwaya!Kama tatizo limeisha na mwenyewe umejiridhisha kwa hilo usianze kuchimbua huku na kule.Mshukuru Mungu ..mshukuru huyo dada alafu rudi kwenye kufurahia ndoa yako.Kama tatizo lake lilikua la kisaikolojia linaweza sana kutibika bila dawa tulizozoea kunywa...
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Hongera kwa uvumilivu mana hilo tatizo mmh!..pia endelea kufuatilia nyendo za mumeo kama kaacha kweli kwa 100% hiyo tabia mana ni habari njema kwenu na ndoa yenu..
   
 5. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Kwani ulitaka ampe dawa gani? Ikiwa unajua kizuri unakula na mwenzio, kula na mwenzio ndio dawa yake? Tatizo limekwisha kwa sababu kampata mtu wa kumuonesha dude lake na kumwagia mbegu zake. Alafu unajua kuwa huyo dada unakula nae kile kitu kizuri, alafu unauliza jibu. Huyo rafiki yako kaona bora amsitiri mumea kwa aibu anayotia mtaani kwa kumtafutia mtu atakae muonesha na kumwagia mbegu zake, zzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz, pole na samahani kama nimekukwaza
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Loh!We Somoe wewe...mbona unataka kumnyang'anya dada wa watu furaha yake?
   
 7. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Inamaana alikuwa na hisia za kifisi maji maana hiyo kali ndo naisikia kwako kutoa dudu hadharani na kuchafua w2 kwenye daladala?? alichofanyiwa na huyo mdada ndo una2ficha haya bana.
   
 8. dadam

  dadam Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mpendwa wangu.. kwa kweli namshukuru mungu..huyo dada aliyeniunganisha na huyo dada aliniambia kua alishamsaidia mama mmoja aliyekua anakojoa kitandani akaacha..kwa hiyo sasa naamini kua hiyo saikolojia ipo na inaweza kusaidia. mwanzo nilikua siamini kwani nilikua nasikia tuu kua wanasaikolojia akikuangalia tuu anajua shida yako
   
 9. dadam

  dadam Member

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Somoe..dada wa watu hakufanya hivyo kwani yeye yupo Dar na Mume wangu yupo Morogoro. aliyewezesha wakutane ni huyu dada aliyeniunganisha nae na walionana siku mbili tuu. (kwa maelezo ya mume wangu na mazingira yenyewe nina uhakika na hili) kwa hiyo hamna namna yoyote ambayo huyo dada angefanya huo ujinga.
   
 10. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  weeeeeeeee!!!!!!!

  hata siku moja usimuapie mwanaume katika maisha yako!!wala usije ukamwamini 100%, utakufa siku si zako ndugu yangu!!! pole weeeeee.

  Eti walikutana siku mbili!!! weweeeee!! ngoja nitoke kwani hata umri wako siujui!!!

  Unasubutu kumwapia mwanaume!!! mwanaume!!! hivi wewe unawajua wanaume vizuri au unawasikia??????????
   
 11. LD

  LD JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ashukuiwe Mungu, aliyeiponya ndoa yako. Hogera kwa uvumilivu. Endelea kumlinda na kumtunza huyo mumeo.
  Wala usihangaike kumuuliza uliza maswali mengi kuhusu hilo, we mwache, akijisikia kukueleza atakueleza.
   
 12. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nimejikuta nafurahi pamoja na wewe mwaya, endelea kumuomba mungu hilo tatizo lisijirudie. Na hongera kwa uvumilivu
   
 13. LD

  LD JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha ha, Susy mamito, si yakale yamepita mpenzi.
  Na wakati huu ni wakufurahi pia mama, badilisha hiyo avatar basi.
  Tunaokomboa wakati wetu, kuwa wakati wa furaha, huku tukiamini wakati wa majonzi umepita.

  Blessing.
   
 14. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  sio siku zote wa mbili havai moja, Susy!!!!!!
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,547
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  mvumilivu kwani sasa tatizo lake limeisha. sikuamini...niliruka hadi nikamwaga soda niliyo kua nakunywa

  mmmhh kwa kufurahia pls kunywa vaisroooooooooooooo niachie invoice r/garden
   
 16. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hongera sana dada kwa uvumilivu wako,
  MUNGU aliona,alisikia kilio chako,
  na sasa amekujibu,
  kupitia mwanasaikolojia.
  Furaha yako iwe ya kudumu,
  pia endelea kumtafuta mwanasaikolojia ila umshukuru ksb yeye ndiye chanzo cha furaha yako,
  Mumeo usimuulize sana maswali kipindi hiki,mpe muda yeye mwenyewe atakwambia kwa muda atakaoona unafaa wewe kuambiwa.
   
 17. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  ha hahaha susy ulivyoongea kwa msisitizo???!!!!,

  Susy nina tatizo na avatar yako kila nikiiangalia NI LAZIMA machozi yanilengelenge machoni mwangu,
  sa sijui kwa nini??, mbona avatar zingine zoote naangalia bila kutokea na hali hii??,

  NTASHUKURU ukinipa ufafanuzi, Asante.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mi nimeshindwa kusoma yote maana ndefu mno.
  Anasemaje hivi?
   
 19. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  dadam,

  Ina maana mumeo ulikuwa "haumfikishi" ndiyo maana akawa Dunga_Dunga!

  Huyo rafikiyo anafahamu jinsi ya kukamua!
   
 20. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Kuna tatizo hapo,uvumilivu noa unahitajika.
   
Loading...