Kizuri Hakikosi Kasoro!!

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
888
1,000
Siku zote MWANAMKE hawezi kumpata Mwanaume aliye mkamilifu maana tupo aina tofauti tofauti.
  1. Ukimpata Handsome_Kichwa chake ni empty.
  2. Ukimpata Genius_Yuko serious masaa 24 na wengi huwa hawako romantic, hawajipendi kihiivyo, wako rafu mno.
  3. Ukimpata Tajiri_ Hawezi kukuheshimu full madharau, utamwambia nini wakati hela anayo bana.
  4. Ukimpata Mfanyakazi hodari_ Hana muda wa kuwa karibu na wewe, muda wote anawaza kazi na kutafuta maisha/pesa.
  5. Ukimpata mnyenyekevu_ Mfukoni huwa ni 0% au salio halisomi
  6. Ukimpata anayekupenda kwa dhati_ Anakuwa siyo type yako, yaani hana sifa unazozitaka, au hana muonekano ule unaoutaka wewe.
  7. Ukimpata msomi_ Hasikilizi ushauri wako anakuona boya tu, huna point za maana mbele yake.
  8. Ukimpata yule Smart_ Ni muongo kupita kiasi na play boy.
Kwahiyo ridhika na yule umpataye na jitahidi kurekebisha mapungufu yaliyopo
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
8,396
2,000
HAPA UMENENA, ILA KWENYE KURIDHIKA NA ULIYENAE NDO TATIZO,
MAANA KILA MTU ANAKUWA NA MATARAJIO MAKUBWAAA KWENYE MAHUSIANO ANATAKA MTU MWENYE MRUNDIKANO WA SURA, TABIA, MUONEKANO KANA KWAMBA ANAMUUMBA YEYE.
 

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,845
2,000
Mtos uzi hebu upe uzoefu wako katika hili; namaanisha wewe ummeshapata wanaume wenye tabia zipi kati ya hizo?
 

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
888
1,000
HAPA UMENENA, ILA KWENYE KURIDHIKA NA ULIYENAE NDO TATIZO,
MAANA KILA MTU ANAKUWA NA MATARAJIO MAKUBWAAA KWENYE MAHUSIANO ANATAKA MTU MWENYE MRUNDIKANO WA SURA, TABIA, MUONEKANO KANA KWAMBA ANAMUUMBA YEYE.
Tatizo kwenye ulimwengu wa sasa nothing is complete perfectly 100%
Dosari na mapungufu hazikosekani. Kikubwa ni kuchukuliana mapungufu na kuvumiliana. Lakini kubwa ni kila mmoja kufanya ADJUSTMENT ili kuweza kuendana na mwenzake na maisha yasonge.
Bila hivyo utamaliza bucha zote kila nyama na kizuri na kibaya chake lakini nyama ni ile ile
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
10,797
2,000
Hiyo no.6 ndio sababu kubwa inayowafanya wanawake kuchepuka wanapokuwa kwenye ndoa,kwani inapokuja akatokea yule ambaye alikuwa wa ndoto yake anachoamua ni kusaliti ndoa yake...
 

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
888
1,000
Mtos uzi hebu upe uzoefu wako katika hili; namaanisha wewe ummeshapata wanaume wenye tabia zipi kati ya hizo?
Kufikia SELF-ESTEEM kwa binadamu yeyote ni jambo gumu sana. Nilishawahi kudate na mdada mmoja hivi ambaye alinichananya kitandani. Lakini baada ya muda akatokea mwingine mzuri sana wa sura ila kitandani sio sana, nikasema hapa nimefika Kigoma lakini baada ya muda nikamchoka huyo na kuanza kuangalia pembeni.

Wanaume wanakuambia wazuri wanazaliwa kila siku, maana yake ni kuwa KUPENDA na KUTAMANI ni swala ENDELEVU. Ni vigumu sana kukidhi mahitaji ya moyo na mwili wako.

Inabidi ifike mahali useme yatosha
 

Use brain Heriel

JF-Expert Member
Nov 3, 2017
2,750
2,000
😂😂 naona mnafarijiana, perfect huwez pata ila siyo kwa traits alizoainisha mtoa mada, nko na vihela, hb,alafu mbona sisumbui ila vihela vinanifanya kuwa mkorofi 😂😂😂
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
1,112
2,000
Acheni ushamba mleta mada sijui kala maharage ya wapi. sikuheshimu tena!

KIZURI DAIMA DUMU;;; hakina kasoro.hata moja na kitaendelea kuwa kizuri tu popote hapa Duniani. hizo kasoro unazoziona ni wewe muonaji ndo unazo tena dhaifu basi... eti msomi anakuona boya! haya! wewe ndo unajiona si kitu mbele zake amesha kuoa tu yatosha kukuthamini.....hata akikubeba mgongoni utasema ''ananifanyia research huyu bwana;; tayari unalianzisha na kusema
'' yaani mmm! umeacha kufanya study research kwa watu wooote hao waja kwangu jamani umenichoka ''

Tajiri naye vilevile akimzika baba yake kwa gharama za juu utaanza ''' mjomba yangu hajaambiwa kuhusu hii taarifa. huyu bwana ana dharau sana.unasononekaaaa! lkn yeye anadunda tu kusaka noti. jioni akirudi umejikunyatta.

SULUHISHO SASA ;;kama unaona hao unaowaita wana kasoro waache waende zao; na mali zao watakutana wasomi kwa wasomi, tajiri kwa tajiri wachache kama mimi ambao tumeoa BRITISH ROYAL FAMILY. tuna raha sana akifoka na mimi nafoka,af tunapena sorry ya kizungu, ngoma draw. si amenipenda bana sasa. mnachefua sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom