Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,300
10,708
Salaam wanaJF!

Tukiwa tunaelekea kutimiza miaka 50 ya uhuru wa bendera wa Tanganyika kumezuka na mwenendo wa serikali ya CCM kutumia nguvu nyingi kutangaza yale yayoitwa mafanikio ya miaka 50 ya uhuru! Tumeona kuanzia bungeni pale wabunge wengi wa serikali (hapa namaanisha wabunge wa CCM) walipokua wakijitaidi kuaminisha wadanganyika kwamba nchi "imethubutu, imeweza na imesonga mbele" kwa kutolea mifano mbalimbali kama wingi wa taasisi za elimu, wingi wa majengo ya zahanati na vituo vya afya, wingi wa wanafunzi wanajiunga na shule (huku kukiwa na wingi wa ongezeko la wasiojua kusoma na kuandika); urefu wa barabara za lami n.k. Msisitizo wa wabunge hao ni kwamba nchi imeendelea sana kuliko ilivyokua mwaka 1961.

Sambamba na hayo tumeona pia wizara, idara na taasisi mbalimbali za dola na serikali zikitumia maonyesho kuonesha mafanikio ya miaka 50 ya uhuru; katika wiki kama mbili hivi tumeona wizara ya ujenzi na idara zake na pia wizara ya elimu na idara zake.

Sasa nimejiuliza hivi si kuna msemo wa kiswahili kwamba KIZURI CHAJIUZA NA KIBAYA CHAJITEMBEZA; hivi kwa mtindo huo wa serikali ya CCM, huu msemo si unaihusu?!

Mambo mazuri iwe maendeleo ya nchi au mtu mmoja mmoja hayapaswi kutangazwa kwa nguvu na gharama kubwa kama inavyojitokeza sasa, haya mambo yanaonekana yenyewe tu...mimi naona wanapoteza muda na pesa bure..hizo pesa si ni bora wangeongezea katika miradi ya umeme kama kule Rufiji, miradi ya barabara vijijini; miradi ya maji n.k.?! Na hii ni trailer, sipati picha hicho kilele hapo 9/12..sijui bajeti yake ni kiasi gani?

Ninafanya mchakato wa kuanzisha petition ya kupinga sherehe hizo zisifanyike, kwani hakuna cha kusherekea katika miaka hii 50 ya giza, njaa na kiu.

Nawasilisha.
Asante.
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,915
9,872
Mkuu hakika umenena vema. Wakati wa kikao cha Bunge Waziri Mkuu alisema serikali itapunguza matumizi kwa kufanya baadhi ya mambo ikiwemo kupunguza sherehe za serikali lakini hapa tunaona sherehe za Uhuru zinaanza mwezi wa nane sijui ikifika mwezi wa kumi na mbili serikali itakuwa imetumia kiasi gani cha fedha kwa ajili ya sherehea miaka 50 ya uhuru!! Ni kwa nini tusingesherehekea kama ambavyo tumekuwa tukifanya huko nyuma? Sijui hii miaka 50 inatofauti gani na miaka 45, 49, 25!! It is just a number.

Nakumbuka wakati niko darasa la saba (nimesoma huko Kantalamba) kulikuwa na Kitabu cha Kiswahili kinaitwa Tujifunze Lugha Zetu Kitabu cha 9, sura ya kwanza ya kitabu hicho ilikuwa inasomeka hivi, "Brown Ashika Tama". Katika sura hiyo kuna mzee alikuwa akimsimlia Mr. Brown juu ya maendeleo iliyoyapata Tanzania miaka 10 baada ya uhuru. (Mr. Brown alikuwa Tanzania wakati wa ukoloni na kuondoka baada ya uhuru kisha akarudi baada ya miaka 10). Sina hakika kama kuna tofauti kubwa kati ya yale aliyokuwa akiyasema yule mzee baada ya miaka kumi na ambayo tunayashuhudia baada ya miaka 50 hasa ukizingatia imepita miaka 40 baada ya Mr. Brown kusimuliwa yale mafanikio!!
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,915
9,872
Miaka 50 ya uhuru wa nchi gani vile?

Ni uhuru wa Tanzania, aah no ni uhuru wa Tanganyika, nimekosea ni uhuru wa Tanzania Bara, hapana mkuu ni uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, noo siyo ni uhuru wa Tanzania na Zanzibar, au ni uhuru wa Tanzania Visiwani na Tanzania Bara!!!?. Duh I am confused!! Majibu yote si sawa. Acha niende library nisome nijue ni uhuru wa nchi gani nitarudi nikuhabarishe.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
1 Reactions
Reply
Top Bottom