Kizungumkuti Cha Lugha ya Kiingeteza; Bunge limenikumbusha mbali leo!!

Elisha Ray

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
323
94
Nimecheka sana leo nilipokuwa naangalia uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki. Nikakumbuka kipindi kile college/university wakati wa presentation ilikuwa ni vituko vitupu!! Wabunge 'to be' walikuwa wanajieleza na kuomba kura kwa lugha ya kiingereza basi kuna walokuwa wanatafuta maneno, etc but kuna mama mmoja wa CUF toka Mbeya alitoa mpya, yeye alikuwa anaongea English sijui ni ya wapi ile akashindwa kuendelea ikabidi aseme ana-withdraw jina lake dah!!
 
sawa mkuu ni lugha ya tatu kwa watanzania wengi now tusiwalaumu walimu kuwa hawajui but hata viongozi wetu
 
Wee unauzungumzia Bunge tu? Mbona husangai Mkuu wao wa Magogoni anavyo Manufacturing Teachers Tanzania. Kuanzaia Mpangaji wa Magogoni mpaka Wabunge ni Vilaza. Nchi ipo ipo tu haina direction.
 
sawa mkuu ni lugha ya tatu kwa watanzania wengi now tusiwalaumu walimu kuwa hawajui but hata viongozi wetu

Ni kweli tusiwalaumu ila kwa kweli ukiachia lugha kuna waliokuwa wanababaika (kwa woga I think) sasa ukichanganya na lugha basi nikakumbuka enzi zileee ambazo ukijifanya mgonjwa unafeli au unakatwa marks yani lazima u-show up then ukawe kituko!
 
Wee unauzungumzia Bunge tu? Mbona husangai Mkuu wao wa Magogoni anavyo Manufacturing Teachers Tanzania. Kuanzaia Mpangaji wa Magogoni mpaka Wabunge ni Vilaza. Nchi ipo ipo tu haina direction.

Hahahaaaa nimekupata....
 
mi kuna mmoja nilimsikia anasema "thank u madam chairman"
yule akipata ipo cku tutamsikia akisema "yesterday I wented"
 
Our MPs with broken english:..it was a disgrace to watch them today..even a secondary student could express himself better
 
Tatizo nililoliona sio wao kushindwa kuongea Kiingereza vizuri, ila kazi ambayo walikuwa wanaiomba inahitaji uwezo wa kumudu hiyo lugha. Shida ingekuwa hivyohiyo kwa kama wangeongea Kiswahili kibovu kwa kuombea kazi ambayo inahitaji ujuzi mzuri wa Kiswahili.

Nilishaandika tena humu jamvini kuwa ujuzi wetu wa lugha umepungua sana, hasa pale unapokuta mtu anachanganya Kiswahili na Kiingereza. Hata hivyo ukimuambia aongee lugha mojawapo kati ya hizo, hawezi kuongea vizuri. Tatizo hili lipo kuanzia viongozi wetu hadi wanafunzi wa shule na jamii kwa ujumla. Nilieleza pia kuwa, mojawapo ya sababu ambazo zinafanya ujuzi wa matumizi ya lugha kuwa duni, ni kushuka kwa kiwango cha elimu ambapo lugha hazifundishwi vizuri. Sababu nyingine ni kwa serikali yetu kutokuwa na nia/sera ambayo inathibiti matumizi ya lugha sahihi.
 
Tatizo letu wa-TZ,ni kukumbatia vya wenzetu na kuviona bora..

Yaani kama ni kucheka ningeweza kucheka lakini si kumdharau aliyechapia lugha ambayo asili yake hasa ni watu wenye ngozi, ama walioumbwa na ngozi nyeupe..

Mtu anacomment eti,"a disgrace"... Wabongo bana!

Mwingine anacomment kuwa viongozi ni vilaza,kigezo kimojawapo ni kutoweza kujieleza kwa Kiingereza kwa ufasaha.. Watu bana!

Nendeni radio za FM,huko mtakuta waongeaji wa Kiingereza wengi tu na hawana certificate nyingine yeyote ya maana... Na hata hesabu ya Simultaneous Equation hawajui!
 
challenge is the better practice 2 reach the gentleman stage, So 2sichekane.After row learning is the continous process.
 
Yes, I saw them today speaking very much english broken blah blah..........................LOL
 
Nimecheka sana leo nilipokuwa naangalia uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki. Nikakumbuka kipindi kile college/university wakati wa presentation ilikuwa ni vituko vitupu!! Wabunge 'to be' walikuwa wanajieleza na kuomba kura kwa lugha ya kiingereza basi kuna walokuwa wanatafuta maneno, etc but kuna mama mmoja wa CUF toka Mbeya alitoa mpya, yeye alikuwa anaongea English sijui ni ya wapi ile akashindwa kuendelea ikabidi aseme ana-withdraw jina lake dah!!

siamini nilichookiona......nilikuwa nikiskia mtu ana elimu ya degree,masters,diploma na phd nikawa ninajua maekamilika lugha zote kumbe hata kiingereza chao ni cha kawaida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom