Kizungumkuti cha lugha duniani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizungumkuti cha lugha duniani!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mtambuzi, Dec 30, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,751
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Lugha zilianza vipi, ni jambo ambalo halifahamiki. Labda rejea pekee ni kwenye Biblia na kisa cha mnara wa babeli. Hakuna anayejua hasa, Adam na Eva walizungumza lugha gani. Huenda ni vigumu kujua hasa lugha zilianza vipi. Maandishi hata hivyo, yana historia, ambapo yalianzia kule bonde la Mesopotania, yaani Wababeli, ndiyo ambao pia waliigawa siku katika dakika na saa.

  Turudi kwenye lugha, ni kwamba, leo hii tuna jumla ya lugha 2,700ambazo zinazungumzwa hapa duniani. Kuna vilahaja au vilugha vilivyojipachua kutoka lugha kuu vipatavyo 7,000. Kule Indonesia huenda ndiko ambako lugha nyingi huzungumzwa. Nchini humo kunazungumzwa lugha 365. Bara ambalo linazungumza lugha nyingi ni afrika ambapo jumla ya lugha 1,000 zinazungumzwa.Je, lugha ngumu kabisa kujifunza ni ipi? Kwanza ni vyema kujua kwamba, kuna rahisi zaidi kujifunza kutokana na sarufi yake na kuna lugha ngumu sana kujifunza.

  Lugha ngumu kabisa katika kujifunza ni Basque, ambayo huzungumzwa kaskazini Magharibi mwa Uhispania na Kusini Magharibi mwa Ufaransa. Lugha hii ni ngumu kujifunza kwa sababu haina uhusiano na lugha nyingine yoyote duniani.
  Kama mjuavyo lugha za kibantu zinahusiana na zile za Nilotiki, lakini lugha hii haina uhusiano na kundi lolote la lugha hapa chini ya jua.

  Lugha inayozungumzwa zaidi duniani ni Mandarin ikifuatiwa na Kiingereza. Lakini kama lugha ya nyumbani, Kihispania ndiyo lugha inayozungumzwa zaidi hapa duniani.
  Je lugha changa? Lugha changa kabisa hapa duniani ni Afrikaans, inayozungumzwa nchini Afrika Kusini. Kumbuka wale wanaoitwa Makaburu ni Waprotestanti wa Kijerumani na Kidachi ambao walikimbia kunyongwa na Kanisa Katoliki kwenye karne ya 17, wakaenda kuishi kwenye Rasi ya Tumaini Jema kule Afrika Kusini. Kufikia karne ya 20 watu hawa waliunda lugha hii ya Afrikaans, kutokana na Kidachi na Kijerumani. Katika kipindi cha miaka 100, lugha hii imekuwa lugha ya pili kwa ukubwa huko Afrika Kusini, ikiwa nyuma ya Kizulu.

  Kunazaliwa lugha mpya kila tamaduni zinapochanganyika. Kwa mfano kuna lugha tofauti 700 zinazozungumzwa jijini London. Kwenye baadhi ya viunga vya jiji hilo Kiingereza kimekuwa nil lugha ya pili badala ya kuwa lugha ya kwanza. Hali iko hivyo kwenye miji kama New York, Los Angeles, Miami na Singapore.Vatican ndiyo nchi ndogo zaidi duniani na ndiyo nchi pekee ambayo inatumia Kilatini kama lugha rasmi.

  Somalia ndiyo nchi pekee duniani ambako lugha inayotumika ni moja tu- Kisomali tu.

  Kabila la Berbers huko Afrika Kaskazini, ndilo pekee ambalo lugha yake haiandikiki.
   
 2. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli hiki ni kizungumkuti cha lugha, hivi Kisandawi kinaandikika kweli?
   
Loading...