Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,500
- 86,042
Mwezi uliopita SEKOMU walivamiwa na watu wanaosadikika kuwa ni "Majambazi" na kumuua Mlinzi pamoja na kuharibu mali nyingine. Watu hao wenye nia ovu walikimbilia kusikojulikana japo baadhi inasadikika walikamatwa na juzi kulikua na taarifa za majambazi kuuwawa Lushoto.
Baada ya tukio lile, kizuizi cha Askari ambacho kipo Kilomita chache kutoka Mombo ukipanda milima ya Usambara kiliondolewa au tuseme kilifungwa na Askari kuondoshwa. Nilijaribu kufuatilia sababu za kuondoshwa kwa kizuizi hicho, nikaambiwa kuwa ni kwa sababu "hawakuonekana kufanya kazi yoyote ya maana hadi jamaa kupita na silaha na wao wakiwa wapo hapo".
Kwa wanaofahamu barabara ya Mombo- Lushoto ni bara bara ambayo kwanza iko kando kando ya Milima, ni nyembamba na eneo kubwa halina network kutokana na geography yake. Kwa hali hii, miaka ya nyuma eneol hili limekua sio salama hata kidogo hasa ukichelewa kupita na ukabahatika kupita nyakati za usiku. Jamaa wakikuweka kati huna pa kukimbilia, huna msaada na uhai wako unabaki mikononi mwao. Kuna matukio mengi ambayo yamesharipotiwa hadi pale Mwanajeshi mmoja aliyewahi kumuua jambazi mmoja maeneo hayo hayo. Binafsi nilipita usiku maeneo yale week mbili zilizopita kwa kweli kunatisha na bahati mbaya kwakua ni usiku basi mtu anakuona unavyozunguka kona zote zile.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba muda mfupi (usiozidi miezi miwili) tangu kuondolewa kwa kituo hicho tayari kumekua na ujambazi tena maeneo hayo. Hivyo basi, TUNAOMBA kiuzuizi kile kirudishwe, kilisaidia kidogo kupunguza ujambazi maeneo yale japo pia ilikua ni rsik sana kwa askari wale, naomba kiboreshwe na ulinzi uimarishwe.