Kizimbani kwa kumvunja kidole bosi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizimbani kwa kumvunja kidole bosi wake

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Mar 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  Kizimbani kwa kumvunja kidole bosi wake

  Imeandikwa na Flora Mwakasala; Tarehe: 4th March 2011 @ 08:36 Imesomwa na watu: 163; Jumla ya maoni: 0
  MKAZI wa Mbezi Fatuma Abdalah (38), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kumvunja kidole bosi wake.

  Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kinyage, Mwendesha Mashitaka Neeme Haule alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari Mosi mwaka huu saa 1:00 asubuhi katika mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam.


  Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa kwa makusudi alimjeruhi Harishanker Joshi anayedaiwa ni bosi wake kwa kumvunja kidole chake cha mkono wa kushoto na kumsababishia maumivu.


  Mshitakiwa alikana mashitaka na kudai kuwa siku ya tukio hakufika kazini kwa kuwa alikuwa nyumbani kwa miezi mitatu na alipofika ofisini alikuta barua ya kufukuzwa kazi.


  Alidi kuwa kutokana na kitendo hicho alitaka kwenda kumshitaki bosi wake kwenye vyombo vya dola kwa kuwa amemfukuza kazi kinyume cha sheria. Upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa.


  Hakimu Kinyage aliahirisha kesi hiyo mpaka Aprili 14 mwaka huu, itakapotajwa tena.


  Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana bada ya kutimiza masharti yaliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini hati ya Sh 300,000.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,012
  Trophy Points: 280
  Mahusiano yanapodorora haya yakuvunjiana viungo yawezekana..................................
   
Loading...