Viongozi wa kitanzania wanahimiza maadili ya kitanzania. Je wao wanayaishi maadili hayo ya kitanzania?

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Dec 26, 2022
9,473
12,866
Imefikia wakati viongozi wetu wawe wakweli tu.Wanasisitiza maadili ya kitanzania wakati wao hawaishi katika maadili ya kitanzania.

Je viongozi wetu mnaishi kwa maadili hayo mnayoyaita ya kitanzania ambayo mnasisitiza vijana wetu wayafuate.

Viongozi ni binadamu kama sisi na tuko nao kila siku humu humu Tanzania na nje ya Tanzania na maisha yao tunayaona kila siku.Chondechonde msiwachanganye hawa vijana wa kitanzania kuwataka waishi kimaadili wakati nyie wenyewe hamuishi kimaadili.

Mnawalaumu bure hawa vijana wa kitanzania kwa kukosa maadili wakati nyinyi kama vioo vya jamii na viongozi hamuishi maadili hayo.

Vijana wa kitanzania hawajui maadili ya kitanzania ni yapi. Vijana wa kitanzania wamezaliwa na kukulia mazingira ambayo wazazi wao na viongozi wao hawaishi maisha ya kimaadili ya kitanzania afu mnataka kuwalaumu.

Chonde chonde kabla hamjawanyoshea hawa vijana vidole mjitizame nyinyi kwanza. Hii nazungumzia viongozi wa familia na viongozi wa kidini na viongozi wa kiserikali tuliowapa dhamana ya kuiongoza jamii yetu katika ngazi zote.

NB: UNAFIKI NI SUMU KWA KIZAZI KIJACHO TUBADILIKE
 
Back
Top Bottom