Kizazi cha nyoka ni kipi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,648
698,192
Ni jambo la kawaida kabisa Sikh hizi kusikia watu wakisema hiki ni kizazi cha nyoka! Ama huu ni uzao wa nyoka?
Kwanini asiwe mnyama mwingine yoyote? Kwanini awe nyoka?
Kwani ni kweli kwamba hiki ni kizazi cha nyoka?
Kilianza lini?
Kizazi cha nyoka kikoje?
Kinyume cha kizazi cha nyoka ni kipi? Au mbadala wake!!!
Majibu ya maswali yote haya yanaturudisha pale Eden kwenye tunda la mti wa kati, na wahusika wale watatu Nyoka,Eva na Adam
Tafsiri ziko nyingi kuhusiana na Siri ya tunda la mti wa kati kama tylivyoona kwenye mada zilizotangulia
Moja yenye kutoa ufunuo kwa akili za kitafiti za kibinadamu ni kwamba Eva alianza kuzini na nyoka na alipoona ni jambo jema akamshirikisha na Adam
Ni katika ngono hiyo ya kwanza ndipo mimba ya Kaini (Cain) ilitungwa!
Kwamba Kaini si mtoto wa Adam wa kumzaa...na wakati wanafukuzwa kutoka Eden tayari Eva alikuwa ni mjamzito wa Kain (uzao wa nyoka?)
Baada ya Kaini kuzaliwa, Eva alibeba tena mimba ya Abel ambayo sasa hii ni OG ya Adam na kwakweli Adam alikuwa na furaha na huyu mtoto
Tufupishe yaliyopita mpaka pale kufika kutoa sadaka kwa Mungu!
Kwanini Kain matoleo yake yalikuwa dhaifu na hayakupokelewa na Mungu?
Je ni kwa vile hakuwa uzao halisi wa Adam bali wa nyoka hivyo hakuona umuhimu kutoa kwa 'babu wa kambo?'
Je hili halipo hata leo hii? Kwamba kwenye mambo ya dhambi tunatoa zaidi na kwa furaha kuliko kwa Mungu?

Abel alitoa kama Mungu alivyoagiza na akabarikiwa...alifanya hivyo kwakuwa alijua kule ndio asili yake isiyo na mawaa achilia mbali laana kwa wazazi wake tu?
Kain kwa hasira alikuja kumuua mdogo wake na kumzika kondeni na kudanganya kuwa hajui ndugu yake yuko wapi
Tangu hapo dhambi ya kuua kuharibu na kudanganya viliingia ulimwenguni
Tangu hapo kumekuwa na vizazi viwili kizazi cha Mungu uzao wa Adam kupitia Abel na uzao wa nyoka kupitia Kaini
Unaweza kuniuliza nani aliendeleza uzao wa Abel wakati aliuawa na ndugu yake bila kuacha mtoto? Kumbuka roho haifi! Hapa dhana ya reincarnation unaweza kuona jinsi inavyojipenyeza
Enyi kizazi cha nyoka mwawezaje kusema mambo mema hali ninyi ni waovu...?(Mathayo 12:34)
Hiki ni kizazi cha nyoka....!!!
 
Nimebaki na maswali.
1. Nyoka anamiliki ubo? if not walinjunjuanaje?
2. Nyoka anaweza kumpa ujauzito mwanadamu na akazaa binadamu na si nyoka?
rubii my dia nyoka wa eden sio huyu wa leo...huyu wa leo ni yule aliyelaaniwa kuwa ataenda kwa tumbo
Pia ujauzito huanza na kimiminika
Mwisho Siri ya Eden bado ni fumbo ambalo bado linatatiza wengi
 
But kama kumbukumbu zangu ziko sawa uzao wa kaini uliisha nadhani kwenye safina. Coz Nuhu ni uzai halisi wa Adam.
Sema mwanae mmoja mke wake ndio bloodline ya kaini kama sijakosea. So si wote duniani ni bloodline ya Kaini.
Ni kweli kabisa unajua kwanini siku hizi hiki kinaitwa kizazi cha nyoka na mambo ya ajabu ajabu mengi yanaongezeka? Uzao wa nyoka unazaana na kuongezeka kwa kasi
 
kizazi cha nyoka ni hiki
 

Attachments

  • Insta-image-4.jpg
    Insta-image-4.jpg
    40.4 KB · Views: 97
who cares. Mafundisho ya kizungu kabla ya adam kulikuwa na nyani mweusi Afrika na nyani akawa mtu that enough
 
Ni kifungu gani cha biblia kinasema eva alizini na nyoka??

Mi najua eva alipewa tunda na nyoka sasa huko kizini na nyoka kuliandikwa wapi mkuu??
 
Back
Top Bottom