Kizazi cha nyoka ni kipi?

Kizazi cha nyoka ni kipi?

Ukisikia kizazi cha nyoka sasa utawaachaje hawa??
f444d2f9619daec838894473b1fb43da.jpg

6510817edc0bb884db54c460bee595c8.jpg

3299932585649187adf6f3bdd06f6e64.jpg

e92c67bead7d4f1ef4ad71f82c22444c.jpg
 
Ni kifungu gani cha biblia kinasema eva alizini na nyoka??

Mi najua eva alipewa tunda na nyoka sasa huko kizini na nyoka kuliandikwa wapi mkuu??
Ndugu unaelewa dhima yako ya kuwa hapa JF? Unapaswa kufikiri zaidi ya kufikiri jus be part of great thinkers....Bible ina mafumbo mengi....hupaswi kuisoma kama novel
 
Ni jambo la kawaida kabisa Sikh hizi kusikia watu wakisema hiki ni kizazi cha nyoka! Ama huu ni uzao wa nyoka?
Kwanini asiwe mnyama mwingine yoyote? Kwanini awe nyoka?
Kwani ni kweli kwamba hiki ni kizazi cha nyoka?
Kilianza lini?
Kizazi cha nyoka kikoje?
Kinyume cha kizazi cha nyoka ni kipi? Au mbadala wake!!!
Majibu ya maswali yote haya yanaturudisha pale Eden kwenye tunda la mti wa kati, na wahusika wale watatu Nyoka,Eva na Adam
Tafsiri ziko nyingi kuhusiana na Siri ya tunda la mti wa kati kama tylivyoona kwenye mada zilizotangulia
Moja yenye kutoa ufunuo kwa akili za kitafiti za kibinadamu ni kwamba Eva alianza kuzini na nyoka na alipoona ni jambo jema akamshirikisha na Adam
Ni katika ngono hiyo ya kwanza ndipo mimba ya Kaini (Cain) ilitungwa!
Kwamba Kaini si mtoto wa Adam wa kumzaa...na wakati wanafukuzwa kutoka Eden tayari Eva alikuwa ni mjamzito wa Kain (uzao wa nyoka?)
Baada ya Kaini kuzaliwa, Eva alibeba tena mimba ya Abel ambayo sasa hii ni OG ya Adam na kwakweli Adam alikuwa na furaha na huyu mtoto
Tufupishe yaliyopita mpaka pale kufika kutoa sadaka kwa Mungu!
Kwanini Kain matoleo yake yalikuwa dhaifu na hayakupokelewa na Mungu?
Je ni kwa vile hakuwa uzao halisi wa Adam bali wa nyoka hivyo hakuona umuhimu kutoa kwa 'babu wa kambo?'
Je hili halipo hata leo hii? Kwamba kwenye mambo ya dhambi tunatoa zaidi na kwa furaha kuliko kwa Mungu?

Abel alitoa kama Mungu alivyoagiza na akabarikiwa...alifanya hivyo kwakuwa alijua kule ndio asili yake isiyo na mawaa achilia mbali laana kwa wazazi wake tu?
Kain kwa hasira alikuja kumuua mdogo wake na kumzika kondeni na kudanganya kuwa hajui ndugu yake yuko wapi
Tangu hapo dhambi ya kuua kuharibu na kudanganya viliingia ulimwenguni
Tangu hapo kumekuwa na vizazi viwili kizazi cha Mungu uzao wa Adam kupitia Abel na uzao wa nyoka kupitia Kaini
Unaweza kuniuliza nani aliendeleza uzao wa Abel wakati aliuawa na ndugu yake bila kuacha mtoto? Kumbuka roho haifi! Hapa dhana ya reincarnation unaweza kuona jinsi inavyojipenyeza
Enyi kizazi cha nyoka mwawezaje kusema mambo mema hali ninyi ni waovu...?(Mathayo 12:34)
Hiki ni kizazi cha nyoka....!!!
Mshana, pamoja na Kaini na Habil, Adamu alikuwa na wana wengine wake kwa waume. Hivyo dunia ya sasa ni matokeo ya watoto kadhaa wa Adam
 
Ni kweli kabisa unajua kwanini siku hizi hiki kinaitwa kizazi cha nyoka na mambo ya ajabu ajabu mengi yanaongezeka? Uzao wa nyoka unazaana na kuongezeka kwa kasi
Yeah hapo uko sawa kabisa. UZao wao unazaana sana. Maana hata mwanzoni ile bloodline ya adam walikatazwa kuzaliana na uzao wa kaini.
 
Mkuu mshana nakuelewa sana, hilo neno huwa nalisikia sana pale ambapo vijana wa siku hizi wakifanya vitendo visivyo na maadili ndio Wazee watasema Hiki ni kizazi cha Nyoka
 
Back
Top Bottom