Kizazi cha jakaya!

Kizazi cha jakaya!

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
Mtoto mmoja alipewa sarafu mbili za shilingi 200 kila moja.Akaambiwa moja ni ya sadaka na nyingine ni ya Ice cream.Katika michezo yake njiani akadondosha sarafu moja katika sehemu ambayo hawezi kuitoa kirahisi.Akaendelea na safari huku akisema;Mungu nisamehe bure,nimedondosha sarafu yako ya sadaka,nimebaki na sarafu yangu ya Ice-cream.>>>>>>Mtoto mwingine alichelewa kufika shule.Mwalimu akamwuliza kwanini amechelewa,Mwanafunzi akajibu:Kuna jamaa alidondosha noti ya sh.5000. MWALIMU:Kwa hiyo ukaendelea kumsaidia kuitafuta. MWANAFUNZI:Hapana,niliikanyagia kwa kiatu mpaka akaondoka.>>>>>>>>>:ZERO:Hawa majirani zetu masikini sana. TINA:Kwa nini?. ZERO:Jana nimemshuhudia yule mama akimpiga bakora mwanae eti kisa kameza sarafu ya sh.100 tu!
 
ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, nimefurahi sana
 
Kizazi cha dot com hicho, Ice cream muhimu kuliko kutoa sadaka! Ama kweli tunaangamia.
 
huyo aliyekanyaga pesa ni soo, lol...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom