Kiza hutengeneza maumbo?

Kiza hutengeneza maumbo?

Angalia vizuri kushoto mwisho
Kitaa cha hapo juu na kwachini hapo Kafuniko hako

Sent using Jamii Forums mobile app
1579826978639.jpeg

Jr
 
Ulishawahi kutembea kizani kwenye giza totoro? Ulishawahi kulala chumba chenye giza mwanzo mwisho? Ulishawahi kuona yale maumbo ya watu na viumbe vya ajabu?

Unatembea kwenye barabara yenye miti vichaka na majani unaona mbele yako au pembeni kuna vitu kama watu au wanyama tena vinatikisika au kutembea au kuongea kwa sauti ya chini

Au unahisi kabisa nyuma yako kuna mtu anakuja anakufuata unatamani ugeuke uangalie au utimue mbio nywele zinasimama kabisa moyo unaenda mbio mambo yanakuwa magumu kweli
Kuna story za vibwengo na vinyamkera vingi hujitokeza kwenye maeneo kama haya lakini si mara zote kila kitu ni hivyo viumbe

Waganga makanjanja wajanja sana hutumia giza na makaburini na sehemu zenye miti na misitu au vichaka kukupiga anakuandalia mazingira kabisa ya wewe kuwaona hao viumbe

Kinachofanyika na ubongo wako mwenyewe kupitia macho yako....unawaza kuhisi na kuhusu vitu vya ajabu kizani kisha unatengeneza picha zake automatically majani yakicheza tu kidogo ile sura na umbo ulivyoviumba akilini vitakujia live...hapa ndio ishu ya vinyamkera na vibwengo hujitokeza, akili yako ndio inakuchezea michezo kulingana na mawazo yako

Fanya jaribio hili usiku wa leo zima taa zote mpaka ile ya nje inayoingiza mwanga kupitia dirishani kisha anza kuwaza kuhusu vibwengo mashetani majini vinyamkera na mizimu nk ...wallah nakuambia utaviona live....

Makaburini kuna story nyingi sana za namna huyo lakini nyingi hazina ukweli na hata hao marehemu tunawasingizia tu
Maisha ni safari ndefu hujui ni lini na wapi unaweza kukutana na hili usibabaike wala kubabaishwa...matukio mengi ya namna hii ni own mind creations...
Kuna ukweli hapa, huwa tunajitekenya na kucheka wenyewe!
 
Hii nimindset ya waganga wanatumia kukula vinoti vyako.

Nimewahi kuwa kuli wa mganga Dar miaka fulani ujob-Less sio poa,mimi na mganga wangu wote tulikuwa maprosoo tu hamna kitu ila kuku tulikuwa tunakula daily,mama mwenye nyumba alikuwa anafahamu kama sisi majambazi.

Lakini alikuwa anatupenda sana kwasababu uhakika wa kula kuku daily ulikuwepo ilifika kipindi hata kodi akawa hadai kabisa

# Asikwambie mtu kitu mganga wa kweli ni mungu pekee,na kwa waganga wetu hawa wa kigoma amini unavyokwenda ndivyo jinsi unavyopokelewa.
 
Back
Top Bottom