Hahahaha! Mkuu umenikumbusha mbali sana. Iliwahi kutokea nikiwa nasoma Advance. Kuna Jamaa alisimamishwa shule kwa makosa ya kinidhamu. Sasa watu wakawa wanatania kuwa kuna mzimu wake kila siku unazurura hapo shuleni. Sasa siku moja tumetokea darasani usiku kupiga msuli,tumekaa mahali tunajipumzisha huku tunasikiliza redio. Bahati mbaya nikapitiwa na usingizi.
Niliokuwa nimekaa nao wakaenda kutafuta shuka leupe pee,wakaja kunifunika kisha wakawajulisha watu kuwa Leo waje wakamshuhudie mzimu wa Jamaa. Sasa wamejikusanya wakaja wengi,wakaanza kujiuliza eti siyo mzimu. Ile wamesema twendeni tukamfumue,mm nikakurupuka kwa wenge la ajabu .......hahahaha! Watu wote walikimbia mpaka wale waliokuwa wamecheza mchezo. Na mm nilipoona wanakimbia,nikawafata mbio nikijua kuna noma. Bado shuka limenishikilia tu. Shule nzima walitoka mbio wanakimbia. Majamaa na wenyewe hawakuwa na uwezo tena wa kujitutumua. Watu tulicheka Sana siku hyo.