Kiza, Giza Totoro la Mkwere! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiza, Giza Totoro la Mkwere!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Mar 20, 2011.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,432
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Novemba 7, 1988, Jakaya Mrisho Kikwete alipewa Ubunge wa kuteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi na kufanywa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, nafasi aliyoishika hadi mwaka 1990 alipoteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo hiyo.

  Kanali Dr. Kikwete alishikilia wadhifa wa Uwaziri wa Maji, Nishati na Madini hadi mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa Waziri wa Fedha nafasi aliyokuwa nayo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 1995.

  Disemba 21, 2005, Kanali Dr. Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania na baada ya miaka mitano kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba ya 2010 alichaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

  Kanali Dr. Kikwete katika wasifu wake kama Waziri na kuhusiana na suala la Nishati, alikuwa kwenye Wizara mama kwa miaka sita, na kisha kuhamia kwenye Wizara simamizi ya bajeti ya nchi kwa miaka miwili.

  Baada ya hapo, Kanali Dr. Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka kumi, kipindi ambacho kilimpa uwezo wa kutembelea nchi mbalimbali na kujenga mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara.

  Kwa Miaka mitano sasa, Kanali Dr. Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hivyo basi tangu siku ile ya Novemba 7 ya mwaka 1988, ni miaka ishirini na mbili.

  Kanali Dr. Kikwete amekuwa kwenye Wizara nyeti na kuwa na mtazamo wa karibu sana kuhusiana na suala la nishati na uzalishaji wa umeme Tanzania pamoja na miundo mbinu na namna ya kuhamasisha mipango ya ndani ya nchi, kupitia wawekezaji na kusimamia bajeti na kuwa na mamlaka ya mwisho yenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kuwasha umeme kwa muda mrefu na si mwendelezo wa tatizo sugu la umeme ambali limelikabili Taifa la Tanzania kwa miaka zaidi ya ishirini na tano.

  Swali la Mchungaji ni hili, je Kanali Dr. Kikwete ambaye amekuwa na uzoefu wa muda mrefu katika sekta ya Nishati na maamuzi makubwa ya kuimarisha sekta hii na kuhakikisha kuwa Tanzania haikosi umeme, anafanya nini kuhakikisha tatizo hili sugu linatatuliwa au kutatulika si kwa mradi wa miezi mitatu kutunusuru kutokana na kukosekana mvua bali ni mpango wa muda mrefu na wenye maana ambao utaokoa fedha za Taifa na kuliongezea mapato?

  Je Kanali Dr. Kikwete kweli ana uwezo wa kushughulikia na kupatia ufumbuzi tatizo la umeme au matatizo mengine ya Tanzania ambayo yanaimarisha UGUMU WA MAISHA?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,069
  Likes Received: 5,194
  Trophy Points: 280
  Watanzania kadhaa (kwa mamilioni) wanaamini kuwa ana uwezo huo na siku moja atafanikiwa; yaani mambo aliyoshindwa kuyafanya kwa miaka yote hiyo atafanikiwa kufanya miaka mitano ijayo. Ukiwauliza watu hawa kwanini wanaamini hivyo watasema "ni kwa sababu hadi hivi anaangushwa na wasaidizi wake". Lakini hawajui kuwa bado ataendelea na anaendelea tayari kuwa na wasaidizi wengine.
   
 3. M

  Mkubwa Dawa Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sidhani kama atafanikisha kupatia ufumbuzi hili suala la umeme kwani nadhani halimuathiri yeye kama raisi na sidhani kama kashawahi kulala kiza nyumbani kwake tokea apate madaraka Kanali "Dr" Kikwete. Kukubali kwamba ataweza kufanikisha hili sifikirii kwani halimgusi hili tatizo na kwa ungwe hii anayomalizia,kwamwe hatalishughulikia itakuwa ahadi hewa kwani hayo ndio "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" aliyotuahidi wadanganyika!
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,320
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mchungaji na Mwanakijiji,

   
 5. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 965
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kuteua wasaidizi wake wazuri,ikiwa JK anaangushwa na wasaidizi wake basi anapaswa kuwajibika yeye mwenyewe.

  JK hawezi kutatua matatizo yetu maana hata yeye mwenyewe hajui yamesababishwa na nini...
   
 6. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viongozi wetu na mustakabali wa taifa letu...."Mwl J.K. Nyerere"
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,432
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo kwa miaka 22 amekuwa akiangushwa na wasaidizi na hana uwezo wa kusimamia suaa sugu la tatizo la umeme? Je Tatizo ni kweli kuwa ni wasaidizi au ni yeye kama kiongozi mtoa dira, afanyaye maamuzi hana uwezo wa kuwa na dira, upeo na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi?

  Je alipokuwa Waziri wa mambo ya nje na alipojitapa kuwa alikuwa anajiandaa kuwa Rais, hakuliona suala la mgao wa umeme na kukosekana kwa umeme kila mwaka kama ni tatizo kubwa ambalo aliliona akiwa wizara mama?

  Je alijifunza nini alipokuwa Waziri wa Nishati, Waziri wa Fedha, na hata Waziri wa Mambo ya Nje, kuwa leo hii suala hili bado linamtoa kamasi na hakuna suluhisho la kudumu?
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,200
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kikwete hana uwezo wa kuongoza hata wilaya achia mbali nchi, na ugumu wa maisha na migongano katika serikali ni zaidi ya uthibitisho kwa hili ninalolisema
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,432
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Je hili linasema nini kuhusu CCM?
   
 10. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 1,466
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  If it walks like a duck
  , quacks like a duck and looks
  like a duck then it...
   
 11. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Anyone who doesn't take truth seriously in small matters cannot be trusted in large ones either.[FONT=&quot]

  Huyu jamaa amekaa
  kwenye madaraka kwa muda mrefu na historia haionyeshi kum-favor
  [/FONT] kuwahi kutekeleza hata mambo madogo ambayo baadaye yamekuja kuwa makubwa baadaye.

  Kwa mfano rushwa bandarini, drug barons, na mengine mengi. Je hili la nishati ambalo ni moyo wa gurudumu la uchumi na maisha ya nchi??! The same porojos
  halafu eti wasaidizi wake ndo wanamwangusha!
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 25,252
  Likes Received: 7,072
  Trophy Points: 280
  Umeme utawashwa kwa jasho letu..si ndio alivyomaanisha Mkulo?
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,709
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Ngoja niweke comment yangu kabla wale jamaa waliojiunga 22 na 23 Feb 2011 hawajaja hapa na kuingiza udini.

  Japo kama waziri alishiriki hata kusaini mkataba wa IPTL bado naweza kumtetea kwa performance yake ya huko nyuma kabla hajawa Rais kwa sababu wakati huo hakuwa na ultimate authority ndani ya serikali. Kwa nia njema kabisa tunaweza kusema labda hakuwa na madaraka makubwa ndio maana hakuperform vizuri na akaona aingie madarakani ili awe na nguvu ya kufanya maamuzi mazuri kwa taifa.
  Kwa masikitiko makubwa, inaonekana hana nguvu pamoja na kuwa katiba inampa madaraka makubwa sana. Nafikiri as a person hana uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Udhaifu huo unachangiwa na Mtandao uliomuingiza madarakani. Kwa siri walizonazo, ameshindwa kuwatosa wana mtandao ambao anataka kuwalipa fadhila. Wanamtando wenyewe asilimia kubwa ni MAJIZI na wengine ni "viazi" tu-they can't perform.

  Mbali na Ahadi anazoendelea kutoa, Expect Nothing Good for now.
   
 14. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa la nchi kwa sasa,sio umeme,sio maji,miundombinu wala maisha magumu,TATIZO ni mtu mmoja anaitwa Kanali J.KIKWETE,na kampuni yake ya CCM
   
 15. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,752
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kama ccm kwa ufupi hawana la kusaidia mwenyekiti wao,sanasana wameimalisha kitengo cha propaganda za kuwaadaa watanzania kwa hali hii.
  Fikili mkuu,Kiongozi wa nchi anakili kuwa matatizo yaliyopo yaliwashinda viongozi waliopita hata yeye angekaa miaka zaidi 10 awezi kuyatatua.
  Je ulize harakati ya kampeni aliukuwa ananadi nini?
  Je, ukiuliza miaka 5 hiliyopita kafanya nini upati jibu?
  Matatizo yaliyopo ayakuzuka leo yapo na yataendelea kuwepo kama hakuna mbinu ya kuzitatua.
  Je,ninani anamsaidi,Makamba.? Msekwa.? na wengine wengi.?
  Limejitokeza na mtoto wake kumsemea. J e ni sahihi
  Naukumbuka usemi wa baba wa TAIFA wakati wamchakato wakupata wagombea ccm mwaka 1995 Alisema "KIKWETE NI KIJANA MDOGO"
  Mpaka sasa hakuna aliyetafakali kauli hiyo.
  - Angekuwa mdogo asingepata nafasi ya kugombea.
  - Baba wa taifa alimaanisha kuwa "uwezo wake ni mdogo" siyo ndogo kiumli au umbo.
  Sasa what is happening today,?

   
 16. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Najuta kuzaliwa Tanzania!
   
 17. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,752
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Tatizo lingine,wazi ndani ya ccm wanjua fika Jamaa akushinda urais sasa atamkolomea nani hapo.?
  Na yeye kaamua bora liende muda uishe.?
  Juzi waziri wake anawaambia watanzania kuwa kila mtu atakula jasho lake.Maana yake nini kuwa mnyonge ana haki hapa.?
   
 18. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,534
  Likes Received: 1,435
  Trophy Points: 280
  Luteni kanali!!!!!!!!!!!!
   
 19. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ...kwa nini ujute kuzaliwa nchi nzuri kama Tanzania kwa ajili ya Mazumbukuku wachache tu? DO SOMETHING about it. Sio Kujuta!!
   
 20. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi kauli ya kusema anaangushwa na wasaidizi wake ina mashiko kwenye suala la uwajibikaji? Yeye kama kiongozi mkuu mwenye upeo mzuri wa kuelewa matatizo yaliyopo hapaswi kusingizia eti wasaidizi ndio wanaomwangusha. Kiongozi aliye makini hukaba kila kona ya uwanja wake na hata hao wasaidizi huogopa kupindisha mambo. Wasaidizi siku zote hupima upepo kuona kama kiongozi mkuu yuko serious na kazi au ni "lazy affair" kind of a leader. Wakishaona mwelekeo wako kuwa hauko makini na kazi hata wao wataiga ili mfanane nao. Kipindi cha marehemu Baba wa Taifa wasaidizi walikuwa wanafanya kazi kwa bidii kwa vile walijua Mwalimu alikuwa anakaba hadi penalty, na alikuwa hakawii kupitisha fagio la chuma kwa wachezaji wazembe wasiojua kukaba au kuzuia mashambulizi ya maadui. Lakini kwa JK mimi naona yupo sawa na mchezaji wa akiba aliyewekwa benchi kwa muda wote wa mchezo na ambaye kwa namna yoyote hawezi kufunga goli au kuzuia maadui (Mafisadi, maradhi, umasikini na ujinga) wasitufunge magoli mengi yasiyo na idadi.
   
Loading...