Kiza, Giza Totoro la Mkwere!

Kiza, Giza Totoro la Mkwere!

Rev.Kishoka,

..kwanza nadhani uwezo wa JK kuongoza ni mdogo.

..lakini kwenye hii sakata ya mgao wa umeme nadhani tatizo ni HUJUMA.

..JK na marafiki zake wameamua kuweka maslahi ya nchi pembeni, na badala yake wanataka kutengeneza utajiri kupitia matatizo ya wa-Tanzania.

..haiyumkini kwanini Tanesco hawapewi ruhusa ya kununua mitambo yao wenyewe, badala yake wanalazimishwa kukodisha kwa Dowans.

..suala lingine ambapo JK na kikundi chake wameamua KUHUJUMU NCHI ni suala la BULK OIL IMPORTATION. ilishauriwa kwamba TPDC ndiyo waagize in bulk, lakini uamuzi huo umebadilishwa na sasa inatafutwa kampuni binafsi.
 
Kwa hiyo kwa miaka 22 amekuwa akiangushwa na wasaidizi na hana uwezo wa kusimamia suaa sugu la tatizo la umeme? Je Tatizo ni kweli kuwa ni wasaidizi au ni yeye kama kiongozi mtoa dira, afanyaye maamuzi hana uwezo wa kuwa na dira, upeo na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi?

Je alipokuwa Waziri wa mambo ya nje na alipojitapa kuwa alikuwa anajiandaa kuwa Rais, hakuliona suala la mgao wa umeme na kukosekana kwa umeme kila mwaka kama ni tatizo kubwa ambalo aliliona akiwa wizara mama?

Je alijifunza nini alipokuwa Waziri wa Nishati, Waziri wa Fedha, na hata Waziri wa Mambo ya Nje, kuwa leo hii suala hili bado linamtoa kamasi na hakuna suluhisho la kudumu?

.....tumbo please niachie mimi Manenge nimbakizie Mandawa nyama choma, supu, mtori aaaah, makande ya nazi, mandazi, soda, mayai, chapti, aah bado kidogo, dagaa, samaki, karanga za kukaanga aah juice ya machungwa aah sasa nala papai tu naona itatosha...aah ache nile ka puding basi sintarudia tena what happened?
 
Alikuwa ayafanye kipindi cha kwanza. Maadam hakuliweza, awamu hii ya mwisho usitegemee chochote zaidi ya kupanga safu ya viongozi watakaochukua nchi 2015 basi! Hana jingine la kufanya.
 
Halafu mbona siku hizi vyombo vya habari havimfagiliii tena kwa jina la DR KIKWETE ?
 
Rev.Kishoka,

..kwanza nadhani uwezo wa JK kuongoza ni mdogo.

..lakini kwenye hii sakata ya mgao wa umeme nadhani tatizo ni HUJUMA.

..JK na marafiki zake wameamua kuweka maslahi ya nchi pembeni, na badala yake wanataka kutengeneza utajiri kupitia matatizo ya wa-Tanzania.

..haiyumkini kwanini Tanesco hawapewi ruhusa ya kununua mitambo yao wenyewe, badala yake wanalazimishwa kukodisha kwa Dowans.

..suala lingine ambapo JK na kikundi chake wameamua KUHUJUMU NCHI ni suala la BULK OIL IMPORTATION. ilishauriwa kwamba TPDC ndiyo waagize in bulk, lakini uamuzi huo umebadilishwa na sasa inatafutwa kampuni binafsi.

Kwenye nyekundu.....sitashangaa kama hatapewa huyu Rahma Al-Kharoos na RBP Oil Technology yake....tayari baadhi ya vyombo vya habari vinamwita ''Mama'' na kama kawaida anajitokeza kufadhili mambo madogo kwa akili za watanzania kama mpira nk....japo hatujui katokea wapi haswa....

Mke+mdogo+wa+Kikwete+2.jpg
 
Novemba 7, 1988, Jakaya Mrisho Kikwete alipewa Ubunge wa kuteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi na kufanywa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini, nafasi aliyoishika hadi mwaka 1990 alipoteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo hiyo.

Kanali Dr. Kikwete alishikilia wadhifa wa Uwaziri wa Maji, Nishati na Madini hadi mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa Waziri wa Fedha nafasi aliyokuwa nayo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 1995.

Disemba 21, 2005, Kanali Dr. Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania na baada ya miaka mitano kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Oktoba ya 2010 alichaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Kanali Dr. Kikwete katika wasifu wake kama Waziri na kuhusiana na suala la Nishati, alikuwa kwenye Wizara mama kwa miaka sita, na kisha kuhamia kwenye Wizara simamizi ya bajeti ya nchi kwa miaka miwili.

Baada ya hapo, Kanali Dr. Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka kumi, kipindi ambacho kilimpa uwezo wa kutembelea nchi mbalimbali na kujenga mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara.

Kwa Miaka mitano sasa, Kanali Dr. Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo basi tangu siku ile ya Novemba 7 ya mwaka 1988, ni miaka ishirini na mbili.

Kanali Dr. Kikwete amekuwa kwenye Wizara nyeti na kuwa na mtazamo wa karibu sana kuhusiana na suala la nishati na uzalishaji wa umeme Tanzania pamoja na miundo mbinu na namna ya kuhamasisha mipango ya ndani ya nchi, kupitia wawekezaji na kusimamia bajeti na kuwa na mamlaka ya mwisho yenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kuwasha umeme kwa muda mrefu na si mwendelezo wa tatizo sugu la umeme ambali limelikabili Taifa la Tanzania kwa miaka zaidi ya ishirini na tano.

Swali la Mchungaji ni hili, je Kanali Dr. Kikwete ambaye amekuwa na uzoefu wa muda mrefu katika sekta ya Nishati na maamuzi makubwa ya kuimarisha sekta hii na kuhakikisha kuwa Tanzania haikosi umeme, anafanya nini kuhakikisha tatizo hili sugu linatatuliwa au kutatulika si kwa mradi wa miezi mitatu kutunusuru kutokana na kukosekana mvua bali ni mpango wa muda mrefu na wenye maana ambao utaokoa fedha za Taifa na kuliongezea mapato?

Je Kanali Dr. Kikwete kweli ana uwezo wa kushughulikia na kupatia ufumbuzi tatizo la umeme au matatizo mengine ya Tanzania ambayo yanaimarisha UGUMU WA MAISHA?

Swala ni uwezo wake wakufikiri na kutokuwa na maono.Leo hii nchi yetu inaingia katika kiza kizito, basi atumie uwezo mdogo kufikiri megawati zinazotumika katika migodi kwa masaa 24 bila mgao ambayo kiuhalisia Mtanzania hafaidiki na mali inayochimbwa moja kwa moja ili atunusuru sisi walala hoi ambao tunategemea umeme katika utendaji wetu.
 
Rev.Kishoka,

..kwanza nadhani uwezo wa JK kuongoza ni mdogo.

..lakini kwenye hii sakata ya mgao wa umeme nadhani tatizo ni HUJUMA.

..JK na marafiki zake wameamua kuweka maslahi ya nchi pembeni, na badala yake wanataka kutengeneza utajiri kupitia matatizo ya wa-Tanzania.

..haiyumkini kwanini Tanesco hawapewi ruhusa ya kununua mitambo yao wenyewe, badala yake wanalazimishwa kukodisha kwa Dowans.

..suala lingine ambapo JK na kikundi chake wameamua KUHUJUMU NCHI ni suala la BULK OIL IMPORTATION. ilishauriwa kwamba TPDC ndiyo waagize in bulk, lakini uamuzi huo umebadilishwa na sasa inatafutwa kampuni binafsi.

,,,Hapo nilipo BOLD ndo muendelezo wa USANII ule ule,enzi zile EDWARD LOWASSA akiwa PM,walikuja na hii idea,lakini leo ni miaka kadhaa,kama kawaida yao hili nalo ni suala linalohitaji MCHAKATO wa miaka nenda rudi,imebaki STORI tu,,,,"oooh tutaiwezesha TPDC uwezo wa kuingiza mafuta kwa wingi baada ya mwaka mmoja tu wabajeti",,ndo ulikua mkakati wa enzi za akina EL,leo miakaa kibao,,,,hii NCHI na hawa jamaa WAKIJANI hata iweje hatutoki katika ZIWA hili KUUUUBWA la umaskini,kwani hawapo kwa ajili ya mie mtanzania wa huku MAKONGOROSI au MATOMBO,wapo kwa ajili yao na familia zao:angry::angry:
 
Sidhani kama atafanikisha kupatia ufumbuzi hili suala la umeme kwani nadhani halimuathiri yeye kama raisi na sidhani kama kashawahi kulala kiza nyumbani kwake tokea apate madaraka Kanali "Dr" Kikwete. Kukubali kwamba ataweza kufanikisha hili sifikirii kwani halimgusi hili tatizo na kwa ungwe hii anayomalizia,kwamwe hatalishughulikia itakuwa ahadi hewa kwani hayo ndio "Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania" aliyotuahidi wadanganyika!

Kwa mtazamo huu tunahitaji msaada sijui kutoka wapi kumpata mtu mwenye mawazo tofauti.Mpaka leo miaka 50 baada ya 'UHURU' tunafikiria kukosa umeme ni kukaa mwenye giza?Kweli tunashangaa viwanda vyetu kufa?Tunashangaa uchumi unashuka?Kama kweli sisi tunaona umeme ni suala la National Security,mbona imepita miaka 50 bado tu tunahangaika?Ina maana basi our national security has been under threat for over 50yrs now.Amazing!!Hivi ni kweli akili zetu haziwezi kufikiria kwa zaidi ya miaka 50 baada ya 'UHURU'?Do we need 100 years to wake up and realize that bila umeme kamwe hatuwezi kuleta maendeleo yeyote(mwenye akili pumba abishe).Inahuzunisha.Halafu tunafurahia nchi za Magharibi kuua wananchi wa Libya kisa eti wana-protect their interests?Inatia hasira sana kama tupo hivi.Tunadharauliwa jamani!
 
Je ni kitu gani kimetufanya Watanzania kuridhika na uongozi wake ambo unanukia harufu ya uhujumu?
 
Watanzania kadhaa (kwa mamilioni) wanaamini kuwa ana uwezo huo na siku moja atafanikiwa; yaani mambo aliyoshindwa kuyafanya kwa miaka yote hiyo atafanikiwa kufanya miaka mitano ijayo. Ukiwauliza watu hawa kwanini wanaamini hivyo watasema "ni kwa sababu hadi hivi anaangushwa na wasaidizi wake". Lakini hawajui kuwa bado ataendelea na anaendelea tayari kuwa na wasaidizi wengine.

Yani tuna safari ndefu. Alafu wakati wa uchaguzi sikusikia kabisa kina Slaa wakiponda utendaji wa huyu bwana! sasa sijui ni siasi gani wanataka kutumia ili waweze kumwondoa! Watu wengi hawana information, na Chadema ijapokuwa wamejitahidi sana kuweka mambo wazi, bado wana sehemu kubwa sana ya kuongeza.
 
Watanzania kadhaa (kwa mamilioni) wanaamini kuwa ana uwezo huo na siku moja atafanikiwa; yaani mambo aliyoshindwa kuyafanya kwa miaka yote hiyo atafanikiwa kufanya miaka mitano ijayo. Ukiwauliza watu hawa kwanini wanaamini hivyo watasema "ni kwa sababu hadi hivi anaangushwa na wasaidizi wake". Lakini hawajui kuwa bado ataendelea na anaendelea tayari kuwa na wasaidizi wengine.

Mwanakijiji...kwa nini wengi wanaamini anaangushwa na WASAIDIZI WAKE???????????
 
Back
Top Bottom