Jitu la-Mtumba
Senior Member
- Mar 20, 2025
- 151
- 349
Habarini wana JF poleni na majukumu ya kila siku. Moja kwa moja ningependa kwenda kwenye maada kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Mimi ni kijana mwenye familia ya mke na mtoto mmoja nayeendelea kupambana kila kukicha katika kibarua changu chenye malipo ya kawaida.
Nimekuwa napata shida kuamua katika jambo ambalo litafaa zaidi kwangu kuanza nalo kuendelea na hatua za mbele, kwa muda nimekuwa nikijikusanya kutafuta kiasi cha pesa ambacho nitakitumia kuanzisha biashara niliyoipanga kuanza nayo kama nitafanikiwa kufikia mtaji wa kuanza nao niliouona utatosha, wazo limekuwa siyo rahisi sana sababu kama mjuavyo maisha yetu ya kitanzania huwa hayajanyooka kwa kiasi hicho japo siyo kwa wote, unaenda hatua sita mbele changamoto inatokea unarudi tena hatua mbili nyuma.
Kiasi cha mtaji nlioupanga nishafikisha nusu mpaka sasa na nusu nyingine inaweza chukua si chini ya miezi mitano mbele.
Kuna muda nakuwa naona kama muda wa kufikia kiasi cha pesa lengwa unaweza ukaongezeka tofauti na malengo au nikapata changamoto mbele nikarudi nyuma zaidi ndiyo napata wazo labda ninunue kwanza kiwanja halafu malengo yangu nianze upya.
Hela iliyopo inaweza tosha kiwanja.
Ningependa kupokea ushauri kwa mtu aliyewahi pitia hii hali au kwa yeyote mwenye mawazo ya kujenga anisaidie kunipa uelekeo utakaofaa. Ahsanteni na karibuni