Kiwango cha Uaminifu na Uadilifu kinazidi kupungua miongoni mwa Watanzania, chanzo ni nini?

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
977
1,528
Tafakari mifano kadhaa ifuatayo na kisha tujadili nini chanzo cha kuporomoka kiwango cha uaminifu na uadilifu kwenye jamii yetu ya Kitanzania.

1) Umetuma fedha kwa njia ya simu kwa makosa, kwa watu watatu tofauti, halafu wapigie simu na uwajulishe kwamba umewatumia fedha kwenye simu zao kwa makosa, na unawaomba na kuwasihi wakurudishie fedha zako. Unadhani miongoni mwa watu hao watatu, wangapi watakurudishia fedha zako?

2) Kuna gari dogo limepata ajali, likiwa na abiria wanne ndani yake, ambao ni majeruhi wenye hali mbaya sana na hawajiwezi, ndani ya gari hilo kukiwa na mizigo yao, kama mabegi, laptops, simu zao za mkononi na fedha tasilimu. Unadhani wananchi watanzania wakifika eneo la ajali, watafanya nini kwanza? Watawaokoa na kuwawahisha majeruhi hospitali haraka? watawapa huduma ya kwanza? Je unafikiri ile mizigo ya abiria itakuwa salama? Ndiyo au hapana...Kwanini?

3) Mara ngapi, ndugu yako/rafiki yako amekuomba umsaidie kiasi cha fedha kama mkopo na kwamba atazirejesha baada 'wiki moja tu' au 'nikishalipwa tu nitakulipa' lakini wiki na miezi kadhaa itapita na kamwe hatarejesha fedha hizo, na huenda akaanza kukukwepa na hata kukusema vibaya kwa watu wengine, wakati wewe ndiye uliyemsaidia. Shida ni nini hapa?

4) Mara ngapi mtu ameibiwa au amefanyiwa uhalifu na watu wabaya, matapeli, vibaka nk, na akaenda kuripoti polisi kuomba msaada wahusika wachukuliwe hatua na haki yake irejeshwe, lakini badala yake, polisi watamwambia atoe chochote ili wapate 'hela ya mafuta' wawatafute wahalifu hao, na kwakweli hawatafanya lolote kuwatafuta wahalifu hao, akiendelea kufuatilia anaweza kujikuta amegeuziwa kibao yeye.

5) Mara ngapi, umesikia kwamba mtu fulani/ofisa fulani mwenye cheo fulani yenye kiwango fulani cha elimu, wakati si kweli, na hata cheti chake cha shule au chuo kikuu ameghushi. Yaani anafanya kazi kama mtaalamu wa fani fulani lakini kiukweli hana sifa za elimu anayodai anayo. Kwa lugha nyingine kuna Degrees, Masters na hata PHD feki.

6) Mara ngapi umemsikia kiongozi wa shirika/taasisi au Waziri fulani au Mkuu wa mkoa/wilaya fulani akitoa kauli ambao ni dhahiri kabisa inaonekana si ya ukweli? Kauli inayoonesha anawatetea wananchi lakini kiukweli ni uongo na anatetea maslahi yake binafsi au ya watu wake wachache.

7) Mara ngapi umepeleka mzigo wa bidhaa kwa wakala au msambazaji wako, kwamba auze mzigo na kisha achukue 'commission yake', lakini cha ajabu, anauza mzigo wote anakula hela zote, commission yake na hata zile zako zote!, ukimpigia simu hapokei na ujumbe hajibu, ukimfuata anakukimbia!!

Una mifano mingine kama hii? Unafikiri hii inasababishwa na nini hasa? Chanzo ni nini na tufanyeje ili tutoke kwenye hali hii?

Tiririka tafadhali.
 
Sababu kuu ni umasikini tu, hakuna jambo jingine... Afrika haina hakika ya maisha ya kesho kimapato
 
Chanzo na asili ya yote haya ni wanasiasa..
Sio wakweli
Sio waaminifu
Wamejawa na hila
Ni wabadhirifu wa mali za uma
Ni wezi na wala rushwa wakubwa
Wamejawa na uongo mwingi na hakuna mtu wa kuwanyooshea kidole wala kuwachukulia hatua

Tumeipa siasa thamani kubwa hivyo vyombo vyote vinawachukulia wanasiasa kama watu wa kaliba ya juu sana na wasiogusika kirahisi

Kwenye hiyo chain hao wanasiasa wana watoto wana ndugu wana marafiki na jamaa, hawa wote wanaona yanayofanyika na kuna wakati ni wafaidikaji pia.. Kwahiyo hapo tayari linatengenezwa tabaka na kizazi kinachoona kuwa hiyo ndio njia sahihi ya maisha

Nyakati za uchaguzi wanaotumika kufanya udanganyifu na wizi wa kura kwa sehemu kubwa ni rika chini ya miaka 30, hawa wanayafanya haya huku familia na ndugu na jamaa wakiona.. Na hakuna hatua zinazochukuliwa
Mwisho kansa inaenea kote na kuharibu jamii nzima

Tufanyeje sasa
1. Siasa ipokwe thamani iliyopewa sasa
2. Taaluma na ujuzi vipandishwe hadhi
3. She ria kanuni na taratibu viwe ndio mwongozo kwenye kila kitu
Walau tuanze na haya machache asante
 
Back
Top Bottom